Zijue alama na maana za kudhibiti maudhui kwenye muvi

namvumi king

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
733
1,000
Habari wakuu,

Wengi wetu tumekuwa watumiaji wa visimbuzi vya makampuni mbalimbali ili tuweze kupata burudani za filamu,tamthilia na michezo Kwa ujumla ili kuburudika na kuelimika

Kwa watumiaji WA DSTV na visimbuzi vingine mara kadhaa kwenye channel tv zinazoonyesha muvi za action,documentary na vinginevyo kumekuwa na alama za PG VSLN Kwa ufupi hizo ni initial za maneno yanayotafsiri hali ya hiyo filamu Kwa ujumla

Maana ya hizi alama huwa zinakwenda sambamba na Umri sahihi WA mtazamaji anaetakiwa kuangalia hicho kipindi kwa wakati huo ili kuwalinda watoto wetu kisaikolojia na tabia katika kuwalea

Maana ya hizi alama na Umri ni
PG. kirefu chake ni parental guidence maana yake kwenye kuangalia kipindi husika usimamizi wa wazazi utahusika
Umri ni kuanzia miaka 13 na kuendelea

VL violence and language. Maana yake kipindi husika kitaonyesha matukio ya vurugu na lugha mbaya na chafu kwa matumizi ya kawaida ya lugha
Umri kuanzia miaka 15 na kuendelea

VSL violence,sexual and language kipindi husika kitakuwa na maudhui yanayoashiria vitendo vya vurugu,ngono na lugha chafu
Umri ni miaka 18 na kuendelea

VSNL violence,sexual,nudity and language
Kipindi husika kitarusha maudhui yaliyosheheni vitendo vya vurugu,ngono,utupu au uchi na lugha chafu
Umri ni miaka 18+ na kuendelea

SNL sexual,nudity and language
Kipindi husika kwenye kisimbuzi chako kitaonyesha matukio yaliyosheheni ngono,uchi na lugha chafu
Umri ni miaka 18+ na kuendelea

Tuwalinde watoto wetu dhidi ya vipindi vyenye maudhui yaliyojuu ya Umri wao ili kuepuka madhara ya kisaikolojia na malezi

Asanteni
 

balimar

JF-Expert Member
Sep 18, 2015
5,398
2,000
Jukwaa la siasa hii mada haiwezi kutembea ipeleke kule kwenye celebrity labda kama nia yako ni kuelimisha.
Humu ni mitifuano tu ya watia nia na wazee wa mamitama basi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom