Ziito Kabwe ameongea ukweli mchungu

Ziito Kabwe ameongea ukweli mchungu

Ukweli ni kuwa Mh. Rais amefanya makosa mengi sana kwenye uchumi, demokrasia na haki za binadamu.

Tunachoshukuru ni kuwa na yeye ameanza kuyatambua makosa aliyoyafanya lakini kwa bahati mbaya damage iliyofanyika ni kubwa, na ni vigumu sana kuyaondoa madhara yake hata kwa miaka kumi. Leo Tamzania imeingizwa kwenye kundi la risk countries for foreign investments.

Makosa yaliyofanyika katika awamu hii yanatukumbusha umuhimu wa katiba mpya ambayo haimpi mtu mmoja mamlaka ya kufanya chochote anachokitaka bila ya kushirikiana na taasisi nyingine.
Binafsi simkubali kabisa huyu bwana na ni bora tu muda wake uishe aondoke madarakani na ikiwezekana aondoke yeye na CCM yake yote waje watu wengine watuongoze.
 
Wia ini ze raiti traki.

Hamjajua tu jinsi watumishi wanamhujumu huyu Pogba Kwa kuwakandamiza haki zao.Wapo kimya kama wameridhika vile
 
Mi nilishasema ni danganya toto haiwezeakani kwa muda mchache kodi ipande ghafla gafla alafu eti uje kusema kuna mlolongo ni mwingi wa ulipaji kodi inabidi tukae tuupunguze alafu kodi ishuke tena wakati anasema hivyo ni yule anaesisitiza watu walipe kodi ili tufanye maendeleo ya nchi uchumi ukue
 
Zitto Kabwe:
Wakati Biashara zinafungwa mawaziri walikuwa wanasema kuwa wanaofunga ni WAPIGA DILI. Leo nimeshangaa kuona eti Rais anashangaa kwanini Biashara zinafungwa. Eti na maagizo yanatoka kuwa TRA isifunge Biashara za Watu sababu za Kodi. Biashara zaidi ya 200K zimeshafungwa!

Ziito Kabwe:
Leo siku nzima nimefuatilia Mkutano wa Rais Magufuli na Wafanyabiashara kutoka nchi nzima. Nawapongeza Wafanyabiashara waliojitoa bila woga kueleza hali halisi. Yote yaliyosemwa tumekuwa tukiyasema Bungeni na Nje ya Bunge. Fikra zangu kuwa tunahitaji Uongozi mpya zimeimarika

Zitto Kabwe:
Ninawasihi Watanzania kuwa tusipumbazwe na haya ‘mateke ya punda anayekata Roho’. Serikali ya CCM ya awamu ya 5 chini ya Rais Magufuli haipaswi kuongezewa hata siku moja Ikulu. Njia ya uhakika kurejesha Uchumi wetu kwenye Reli sahihi ni kufanya MABADILIKO.

Zitto Kbwe:
Baada ya mkutano ule wa Rais Magufuli na Wafanyabiashara nimetazama makadirio ya makusanyo ya Kodi za Wafanyakazi nchini kwa Bajeti ya 2019/2020 na nimekuta makadirio yameshuka kwa zaidi ya TZS 500 Bilioni. Hii maana yake ni kuwa ajira rasmi zimeshuka sana

Chanzo:Ukurasa wake wa twitter.

My take:
Ipo siku tutakuja kuelewa ukweli huu wakati tukiwa tumechelewa.

CCM ni wajanja sana tumieni akili watanzania(hapa kuna siasa inaendelea).

Kushughulikia watu wachache kwa faida ya chama na kiongozi wao kwao si tatizo.

Maandalizi ya 2020 yanaendelea.

BIASHARA ndio njia pekee ya kukufanya ulinde na kuongeza mtaji wako. Mara nyingi Kufunga Biashara sio kulinda mtaji bali kuupunguza kupitia matumizi.
Wengi hawafungi bali wanabadili na wapo wachache wanaohamisha biashara zao.
Dhana ya wapiga deal ni sahihi kwa zaidi ya 50%..
Hakuna mfanyabiadhara mwaminifu..
Wenyewe wamekiri kutoa rushwa japo wanasababu..
Rais amekuja na ushahid wa makampuni 17000 ya kitapeli.
Wako wenye mauzo bilion wao huonyesha milion 20.
Wako kina Kaluwa wazee wa ganji la bilion 4
Hawa wakifunga kwa nini tusiseme ni wapiga deal
 
Ndiyo matatizo ya kumsukumizia mwendawazimu Ikulu. Na kama ulivyosema na bado, kwani hali ya uchumi ni mbaya sana na mapato ya kodi yanazidi kushuka. Fagio la chuma kwa wafanyakazi wa Serikali liko njiani na sijui kama kutakuwa na pesa za kugharamia uchaguzi mwakani.

Duh hilo la kodi za wafanyakazi kushuka hadi kwa kiwango cha 500bilion ni hatari sana, maana yake tumepoteza watu wengi sana kutoka ajira rasmini. Kwa hali tuwe makini sana na data zetu za makusanyo pale TRA..

Kuna viashiria vinaonyesha mambo hayako sawa, lakini tatizo la watanzania wengi ni kuwa wapenzi wa vyama na si kuishi kwa uhalisia, Unawezaje kusema unakusanya kodi ya kutosha huku kila siku tunabadirisha makamishina wa TRA, unawezaje kujisifia kwenye makusanyo huku mamia ya watu wametoka kwenye ajira rasmi na hakuna ajira mpya zilizozarishwa? Unawezaje kujisifia kwenye makusanyo huku kumbe kuna matatizo makubwa na watu wanafunga biashara??
 
Swaga ya "wapiga deal iko wapi"?
Eti nini Zitto anasema? Anasema ''Njia ya uhakika kurejesha Uchumi wetu kwenye Reli sahihi ni kufanya MABADILIKO''. Hivi jamani uchumi wetu ulishakuwa kwenye reli sahihi ili tuurejeshe? Anakumbuka kipindi cha Kikwete alichokuwa anafaidi ndiyo anakiita ''uchumi ulikuwa kwenye reli sahihi''. Huu ni upumbavu na ubinafsi wa hali ya juu. Wanasiasa wa aina hii walaaniwe kwani wanajifikiria wao tu! Kweli kile kipindi cha Kikwete ambacho kila mtu alikuwa anaachiwa kuiba na kufanya hujuma atakavyo ndiyo anasema tulikuwa kwenye reli sahihi?
 
Mbona ndugu migebuka ameshindwa kutwambie kama tusipo muongezea Magufuli siku ikulu nani tumpe?
MKEO AU MMEO AKIKUSHINDA KTK NDOA UTACHUKUA HATUA MBALIMBALI IKIWAMO KUMUONYA , KUMKUMBUSHA WAJIBU WAKE N.K NA IKITOKEA AKASHINDIKANA BASI JIBU NI KUMPIGA CHINI, HIVYO ZITO YUPO SAHIHI LAZIMA NDULI AKAE BENCHI
 
Eti nini Zitto anasema? Anasema ''Njia ya uhakika kurejesha Uchumi wetu kwenye Reli sahihi ni kufanya MABADILIKO''. Hivi jamani uchumi wetu ulishakuwa kwenye reli sahihi ili tuurejeshe? Anakumbuka kipindi cha Kikwete alichokuwa anafaidi ndiyo anakiita ''uchumi ulikuwa kwenye reli sahihi''. Huu ni upumbavu na ubinafsi wa hali ya juu. Wanasiasa wa aina hii walaaniwe kwani wanajifikiria wao tu! Kweli kile kipindi cha Kikwete ambacho kila mtu alikuwa anaachiwa kuiba na kufanya hujuma atakavyo ndiyo anasema tulikuwa kwenye reli sahihi?
KWANI AMETAJA KIPINDI CHA KIKWETE KTK HOJA YAKE? KWANI NI KIPINDI KIPI UCHUMI ULIWAHI KUWA MCHAFU KAMA AWAU HII?
 
Eti nini Zitto anasema? Anasema ''Njia ya uhakika kurejesha Uchumi wetu kwenye Reli sahihi ni kufanya MABADILIKO''. Hivi jamani uchumi wetu ulishakuwa kwenye reli sahihi ili tuurejeshe? Anakumbuka kipindi cha Kikwete alichokuwa anafaidi ndiyo anakiita ''uchumi ulikuwa kwenye reli sahihi''. Huu ni upumbavu na ubinafsi wa hali ya juu. Wanasiasa wa aina hii walaaniwe kwani wanajifikiria wao tu! Kweli kile kipindi cha Kikwete ambacho kila mtu alikuwa anaachiwa kuiba na kufanya hujuma atakavyo ndiyo anasema tulikuwa kwenye reli sahihi?
Hayo ya wizi umeyatoa wapi?Kichwani kwako ila sio kwenye maneno ya Zitto!Anazungumzia wastani mzuri wa kukua kwa uchumi,kwa sasa tumeanguka vibaya mno!Ni suala la namba tu ambazo zinareflect uhalisia!
Hayo ya wizi yakwako!
 
We

We akili yako iko tenge ntakuuliza swali la ki layman kwani wewe unataka usifaidi uchumi ukinawili? Mbona unaongea kama mlozi?
 
Zito Kabwe njoo na ngonjera zako za bandari ya bagamoyo.

Mnahongwa pesa mtetee ujinga na ufisadi
Watanzania tumerogwa, siyo bure!
Zito Kabwe atahongwa na nani kutetea Bandari ya Bagamoyo? Haiingii kwenye kikao chochote cha maamuzi. Wanaoingia ni MAKADA WA CCM, ambao ndiyo wameingia mikataba yote ya hovyo tangia awamu ya pili.
Kwa hiyo kama yupo wa kumhonga Zito Kabwe, basi ni wale MAKADA WA CCM, walioingia makubaliano ya kifisadi kuhusu Bandari ya Bagamoyo.
Ukweli mchungu ndiyo huu: CCM NI JANGA LA KITAIFA.
Wanaoitetea wote ni WASALITI Wa Taifa letu!
 
Hayo ya wizi umeyatoa wapi?Kichwani kwako ila sio kwenye maneno ya Zitto!Anazungumzia wastani mzuri wa kukua kwa uchumi,kwa sasa tumeanguka vibaya mno!Ni suala la namba tu ambazo zinareflect uhalisia!
Hayo ya wizi yakwako!
Afu cha ajabu yaani awa jamaa wa awamu hii sijui wanamdanganya nani kwamba hawaibi,kwa taarifa yako wizi ni kama wote hivi
 
Back
Top Bottom