Ziito Kabwe ameongea ukweli mchungu

Ziito Kabwe ameongea ukweli mchungu

Zitto Kabwe:
Wakati Biashara zinafungwa mawaziri walikuwa wanasema kuwa wanaofunga ni WAPIGA DILI. Leo nimeshangaa kuona eti Rais anashangaa kwanini Biashara zinafungwa. Eti na maagizo yanatoka kuwa TRA isifunge Biashara za Watu sababu za Kodi. Biashara zaidi ya 200K zimeshafungwa!

Ziito Kabwe:
Leo siku nzima nimefuatilia Mkutano wa Rais Magufuli na Wafanyabiashara kutoka nchi nzima. Nawapongeza Wafanyabiashara waliojitoa bila woga kueleza hali halisi. Yote yaliyosemwa tumekuwa tukiyasema Bungeni na Nje ya Bunge. Fikra zangu kuwa tunahitaji Uongozi mpya zimeimarika

Zitto Kabwe:
Ninawasihi Watanzania kuwa tusipumbazwe na haya ‘mateke ya punda anayekata Roho’. Serikali ya CCM ya awamu ya 5 chini ya Rais Magufuli haipaswi kuongezewa hata siku moja Ikulu. Njia ya uhakika kurejesha Uchumi wetu kwenye Reli sahihi ni kufanya MABADILIKO.

Zitto Kbwe:
Baada ya mkutano ule wa Rais Magufuli na Wafanyabiashara nimetazama makadirio ya makusanyo ya Kodi za Wafanyakazi nchini kwa Bajeti ya 2019/2020 na nimekuta makadirio yameshuka kwa zaidi ya TZS 500 Bilioni. Hii maana yake ni kuwa ajira rasmi zimeshuka sana

Chanzo:Ukurasa wake wa twitter.

My take:
Ipo siku tutakuja kuelewa ukweli huu wakati tukiwa tumechelewa.

CCM ni wajanja sana tumieni akili watanzania(hapa kuna siasa inaendelea).

Kushughulikia watu wachache kwa faida ya chama na kiongozi wao kwao si tatizo.

Maandalizi ya 2020 yanaendelea.

Zitto hana jipya ni opportunist kama walivyo wengine. Yeye ndiyo alieandaa mkutano na hao wafanyabiashara? Tulioangalia tulimsikia Rais akiwasisitizia kutoogopa na waseme yooote ili kama kutatua matatizo yatatuliwe. Zitto ni kati ya watu nisiowaamini na sitowaamini maisha.
 
Pamoja na harakati za kukutana na wafanyabishara hakuna kitu kitabadilika ikiwa tatizo at core halitatatuliwa.TRA ni kisichaka tuu lakini tatizo kubwa ni kufanya miradi isiyo na taji kwenye afya ya uchumi,yaani unajitutumua kufanya jambo kwa pupa lakini kilichokuzidi uwezo mwisho wa siku nusu ya bajeti eti inaenda stiglaz, sgr na Dom as if hiyo miradi ni hitaji kuu la uchumi wa nchi kwa mda mfupi ujao
Unategemea sekta zingine itakuaje? Mzunguko wa pesa utatoka wapi kustimulate uchumi? Tra watatoa wapi pesa ili ili kumfurahisha mkuu kama sio kubambikia watu makodi? Afu najiuliza wachumi wakiongozwa na akina Mpango ndio wanashauri hayo au kila kiongozi wa ccm ni mchumi unajua sielewi
 
Zitto hana jipya ni opportunist kama walivyo wengine. Yeye ndiyo alieandaa mkutano na hao wafanyabiashara? Tulioangalia tulimsikia Rais akiwasisitizia kutoogopa na waseme yooote ili kama kutatua matatizo yatatuliwe. Zitto ni kati ya watu nisiowaamini na sitowaamini maisha.
Ni mara mia bora huyo anayetetea miradi ambayo yeye na wengine tutanufaika kuliko mnaotetea miradi ya kutuzika tukiwa wazima.Nasimama na Zito mradi wa bagamoyo ulikuwa muhimu sana kuliko miradi inayofanywa sasa na kama kulikuwa na masharti msiyoyapenda meza na viti vilivunjika hadi msikae kuraise concern? Hakuna pesa mtaani na wala sio Tra wamesababisha
 
Zitto hana jipya ni opportunist kama walivyo wengine. Yeye ndiyo alieandaa mkutano na hao wafanyabiashara? Tulioangalia tulimsikia Rais akiwasisitizia kutoogopa na waseme yooote ili kama kutatua matatizo yatatuliwe. Zitto ni kati ya watu nisiowaamini na sitowaamini maisha.
Zile zilikuwa ni kiki tu za kisisa.Mengi yalikuwa yanasemwa ila aliamua kukaa kimya ila kwa sasa maji yamezidi unga ndio akaandaa hilo tukio la hapo magogoni kanakwamba taarifa zilikuwa hazimfikii.
 
We

We akili yako iko tenge ntakuuliza swali la ki layman kwani wewe unataka usifaidi uchumi ukinawili? Mbona unaongea kama mlozi?
ukinawili = ukinawiri! By the way umesoma na kuelewa? Haya ngoja nijibu swali lako la ki-layman ambalo ni la ki-layman kweli kweli: Hata mimi nataka nifaidi uchumi kama utanawiri kwani hakuna mtu asiyependa maisha mazuri! Ila dukuduku langu bado liko pale pale: Uchumi wetu haukuwa mzuri hata wakati wa Kikwete. Inakuwaje Zitto anasema ''tuurejeshe'' ulikokuwa? Hakika atakuwa anazungumzia uchumi wake binafsi na siyo uchumi wa nchi!
 
Hayo ya wizi umeyatoa wapi?Kichwani kwako ila sio kwenye maneno ya Zitto!Anazungumzia wastani mzuri wa kukua kwa uchumi,kwa sasa tumeanguka vibaya mno!Ni suala la namba tu ambazo zinareflect uhalisia!
Hayo ya wizi yakwako!
Ya wizi si ya kwangu ila ni ya awamu iliyopita (japo hata sasa bado wizi upo lakini angalau kuna watu wanaoonyesha concern). Nchi ilikuwa inachezewa na waliokuwa wanafaidi ni wachache, Zitto akiwa mmoja wapo. Ndugu zangu, jamaa, majirani na wananchi wa kijijini kule nitokako hawaoni tofauti kati ya uchumi wa sasa na uchumi uliopita!
 
Kuna mijizi kama BASHITE N JIWE?
 
ukinawili = ukinawiri! By the way umesoma na kuelewa? Haya ngoja nijibu swali lako la ki-layman ambalo ni la ki-layman kweli kweli: Hata mimi nataka nifaidi uchumi kama utanawiri kwani hakuna mtu asiyependa maisha mazuri! Ila dukuduku langu bado liko pale pale: Uchumi wetu haukuwa mzuri hata wakati wa Kikwete. Inakuwaje Zitto anasema ''tuurejeshe'' ulikokuwa? Hakika atakuwa anazungumzia uchumi wake binafsi na siyo uchumi wa nchi!
Logic ni kwamba awamu iliyopita pamoja na kuwa haukuwa mzuri lakini ulikuwa bora kuliko awamu hii maana ulikuwa unazalisha ajira,biashara na ustawi kiujumla.Sasa badala ya kurekebisha mapungufu mkaanza kuharibu ili muonekano mko zaidi ya awamu ya nne matokeo yake aibu imewajaa,kila ngumbaru wa ccm ni mchumi na kwa kuwa wa Tzn wengi tunajali matumbo tunaacha bora liende,sitaki kuamini kwamba eti Dr Mpango ndio anapanga bajeti ya nusu ya makusanyo kugharamia miradi 2,,hii haipo dunia yoyote
Imf ilitoa ripoti mkasema eti inafanya propaganda haya bln 500 za PAYE ziko wapi,mliambiwa biashara zinakufa mkasema eti mpya zinaanzishwa sasa mbona makadilio ya Tra yanapungua? Uhalali wa kujiita viongozi uko wapi si mjiudhulu tuu?
 
Mbona ndugu migebuka ameshindwa kutwambie kama tusipo muongezea Magufuli siku ikulu nani tumpe?
Kwani NEC imeshateua wagombea wa 2020?kwetu Sisi ccm uchumi unapaa kwa 12%huku ukichagizwa na ununuzi wa madege, ujenzi wa SGR na hapa kazi tu
 
Ya wizi si ya kwangu ila ni ya awamu iliyopita (japo hata sasa bado wizi upo lakini angalau kuna watu wanaoonyesha concern). Nchi ilikuwa inachezewa na waliokuwa wanafaidi ni wachache, Zitto akiwa mmoja wapo. Ndugu zangu, jamaa, majirani na wananchi wa kijijini kule nitokako hawaoni tofauti kati ya uchumi wa sasa na uchumi uliopita!
Ingekuwa waliokuwa wanafaidi wachache mara wanachezewa sasa je wanyonge wa saizi wanafaidi? Kila sekta hoi ukienda hospitali utaambulia vipimo dawa unakomaa kitaa,kama condom tu shida kipi cha maana wanyonge na nyie wakubwa mnafaidi?
 
Eti nini Zitto anasema? Anasema ''Njia ya uhakika kurejesha Uchumi wetu kwenye Reli sahihi ni kufanya MABADILIKO''. Hivi jamani uchumi wetu ulishakuwa kwenye reli sahihi ili tuurejeshe? Anakumbuka kipindi cha Kikwete alichokuwa anafaidi ndiyo anakiita ''uchumi ulikuwa kwenye reli sahihi''. Huu ni upumbavu na ubinafsi wa hali ya juu. Wanasiasa wa aina hii walaaniwe kwani wanajifikiria wao tu! Kweli kile kipindi cha Kikwete ambacho kila mtu alikuwa anaachiwa kuiba na kufanya hujuma atakavyo ndiyo anasema tulikuwa kwenye reli sahihi?
Kwann huwa mashambulia sana awamu iliyopita? Halafu Mara zote nikiuliza huo wizi umelingaishwa na wizi wa awamu zipi kwa data zipi ukaonekana ndo awamu ya wizi kuliko awamu zote huwa sipewi majibu ya kuridhisha.

Hakuna utawala usio na mapungufu. Utawala uliopita haukuwa wa ajabu saaana. Na uchumi pia haukushikiliwa na wezi kama mnavyosema' sema ulikuwa utawala wa kibepari na utawala wa kibepari lazima waibuke watu wanaoziona fursa na kuzitumia kwa njia yoyote hata za ujanja ujanja.

Mfano wa tofauti ya mfumo wa Ujamaa na ubepari: umefungua duka, ukaajiri mfanya biashara ambaye anajua biashara haswa, anakuletea faida ya milioni tatu kwa siku na yeye anakuibia milioni au umeajiri mwaminifu asiyeiba hata mia Ila anakuletea faida ya laki tano au milioni. Ungechagua yupi? Nchi yoyote ya kibepari wajanja wajanja lazima wawepo Ila maendeleo pia ni makubwa. Mzee kikwete kama sijakosea aliwahi sema ukifungua madirisha upate hewa wataingia na mbu na wadudu. China sijui waliwezaje kufanikiwa kupitia Ujamaa.
 
Mbona ndugu migebuka ameshindwa kutwambie kama tusipo muongezea Magufuli siku ikulu nani tumpe?
Hana alternative!
Yaani, hata CCM ikisema haitaki tena kutawala, hawa wapinzania hawana mtu anayefaa kuwa mkuu wa nchi.
Hawa jamaa ni hovyo sana!
Wapo kama Wasudan.
Sudan wamepigania mabadiliko ila cha ajabu jeshi limekosa mpinzani wa kumpa utawala baada ya El Bashir kuondoka
 
Ingekuwa waliokuwa wanafaidi wachache mara wanachezewa sasa je wanyonge wa saizi wanafaidi? Kila sekta hoi ukienda hospitali utaambulia vipimo dawa unakomaa kitaa,kama condom tu shida kipi cha maana wanyonge na nyie wakubwa mnafaidi?
Nimesema hivi: Wananchi wa kawaida hali ni ile ile. Kwa wakubwa waliokuwa wanafaidi kuna baadhi hali zao ni mbaya. Ila hilo siyo tatizo la wananchi wa kawaida. Ni tatizo lao na familia zao.
 
mzee kuanzia sasa wasikilize wapinzani ndio wanaosema ukweli sasa mnavyowafanyia kule bungeni na nje si sawa nadhani sasa unaweza badilika baada ya kuelewa umuhimu wa bunge live na kukubali kukosolewa
Ni bora awasikilize wadau wa sekta huska. Kama biashara asikilize wafanyabiashara, kilimo asikilize wakulima nakadhalika. Wapinzani na wanasiasa wenzake wa CCM hawajui na hawana suluhisho kwenye jambo lolote zaidi ya kupiga ngonjera.
 
Kwann huwa mashambulia sana awamu iliyopita? Halafu Mara zote nikiuliza huo wizi umelingaishwa na wizi wa awamu zipi kwa data zipi ukaonekana ndo awamu ya wizi kuliko awamu zote huwa sipewi majibu ya kuridhisha.

Hakuna utawala usio na mapungufu. Utawala uliopita haukuwa wa ajabu saaana. Na uchumi pia haukushikiliwa na wezi kama mnavyosema' sema ulikuwa utawala wa kibepari na utawala wa kibepari lazima waibuke watu wanaoziona fursa na kuzitumia kwa njia yoyote hata za ujanja ujanja.

Mfano wa tofauti ya mfumo wa Ujamaa na ubepari: umefungua duka, ukaajiri mfanya biashara ambaye anajua biashara haswa, anakuletea faida ya milioni tatu kwa siku na yeye anakuibia milioni au umeajiri mwaminifu asiyeiba hata mia Ila anakuletea faida ya laki tano au milioni. Ungechagua yupi? Nchi yoyote ya kibepari wajanja wajanja lazima wawepo Ila maendeleo pia ni makubwa. China sijui waliwezaje kufanikiwa kupitia Ujamaa.
China baada ya kukuta wanatumia nguvu kubwa na maumivu makali ya ujamaa wakaachana rasmi na huo ujamaa,ikumbukwe vizuri china imeibuka kuwa taifa la uchumi unaopaa baada ya kufungua milango ya uwekezaji yaani liberalization na privatization na hata wawekezaji wakubwa china ni wageni ndio wakapata fursa ya kuiba na ku copy teknolojia za watu,hadi kesho china ni wajamaa kwenye siasa lakini sio kwenye uchumi.Hakuna nchi yoyote ya kijamaa imewahi endelea duniani hapa haipo
 
Zitto Kabwe:
Wakati Biashara zinafungwa mawaziri walikuwa wanasema kuwa wanaofunga ni WAPIGA DILI. Leo nimeshangaa kuona eti Rais anashangaa kwanini Biashara zinafungwa. Eti na maagizo yanatoka kuwa TRA isifunge Biashara za Watu sababu za Kodi. Biashara zaidi ya 200K zimeshafungwa!

Ziito Kabwe:
Leo siku nzima nimefuatilia Mkutano wa Rais Magufuli na Wafanyabiashara kutoka nchi nzima. Nawapongeza Wafanyabiashara waliojitoa bila woga kueleza hali halisi. Yote yaliyosemwa tumekuwa tukiyasema Bungeni na Nje ya Bunge. Fikra zangu kuwa tunahitaji Uongozi mpya zimeimarika

Zitto Kabwe:
Ninawasihi Watanzania kuwa tusipumbazwe na haya ‘mateke ya punda anayekata Roho’. Serikali ya CCM ya awamu ya 5 chini ya Rais Magufuli haipaswi kuongezewa hata siku moja Ikulu. Njia ya uhakika kurejesha Uchumi wetu kwenye Reli sahihi ni kufanya MABADILIKO.

Zitto Kbwe:
Baada ya mkutano ule wa Rais Magufuli na Wafanyabiashara nimetazama makadirio ya makusanyo ya Kodi za Wafanyakazi nchini kwa Bajeti ya 2019/2020 na nimekuta makadirio yameshuka kwa zaidi ya TZS 500 Bilioni. Hii maana yake ni kuwa ajira rasmi zimeshuka sana

Chanzo:Ukurasa wake wa twitter.

My take:
Ipo siku tutakuja kuelewa ukweli huu wakati tukiwa tumechelewa.

CCM ni wajanja sana tumieni akili watanzania(hapa kuna siasa inaendelea).

Kushughulikia watu wachache kwa faida ya chama na kiongozi wao kwao si tatizo.

Maandalizi ya 2020 yanaendelea.

Mkuu ungemuuliza zzk mbona hajaongelea tena bandari ya Bagamoyo kama alivyobwabwaja kipindi kile! .Kama kweli alifuatilia mkutano wa JPM, maana JPM aliongelea pia sakata la bandari ya bagamoyo but zzk hilo anajifanya hakulisikia.
 
Back
Top Bottom