Ziara za Kinana (Katibu Mkuu wa CCM) Mikoani

Ziara za Kinana (Katibu Mkuu wa CCM) Mikoani

Unamaanisha njaa ipi?
Kama nyie mmeshiba basi mumkumbuke mwenye njaa. Na hilo ndio linawaponza, mmejijali nyie na mwananchi mmemuacha na shida zake!

- Hakuna linalotuponza ila nia magomvi ya sisi wenyewe kwa wenyewe tu ndani ya CCM, lakini sio kwa sababu ya Chadema no way bado ni chama kidogo sana kwetu, bado mna safari ndefu sana mbele yenu kufikia CCM chama dume la mbegu!!

Le Mutuz!!
 
Msinichekeshe jamani,
Ngoja wajaribu tena,
Wakati ule walipopitisha azimio la kujivua magamba kule Dodoma, walirudi na nyimbo hizohizo, Nape akasema chama kimezaliwa upya, wanazunguka nchi nzima kuwaeleza wananchi matumaini mapya, wapinzani wafunge virago.
Walifikia wapi vile!? au tusubiri tathmini ziwe mbili, ile ya mwanzo na hii inayoanza 21.
Ningewashauri waanze na kuwaeleza wananchi ni jinsi gani wanaweka msukumo wa kurejesha mabilioni ya shilingi za wananchi zilizotoreshewa nje na majambazi ili zitumike kwa maendeleo ya wananchi, angalau hata wakiumwa homa wapate panado ya kushusha joto.
Labda hapo kwa mbaaali wananchi wanaweza kuwaelewa, nakujua kwamba wanahusika au hawahusiki!
 
- Sawa sawa bro, mapungufu yapo kila pande za siasa, Chadema mna upungufu wa Demokrasia so is us CCM, Roma haikujengwa in one day Demokrasia ya USA ambayo inakubalika sana Duniani ina umri wa Miaka 300 sasa, walipitia mote humu tunamopitia sasa, CCM tunajua Demokrasia ndio maana mmeshinda viti 46 vya ubunge bila tatizo!

- Kesi nyingi tu mmeshinda za uchaguzi mahakamani sasa unasemaje CCM hatujui Demokrasia, yes nimesema mara nyingi sana kwamba nyie njooni na mabadiliko tokeo Chadema na sisi wengine tutakuja nayo tokea CCM, otherwise angalau una hoja sio wengine wanaandika ujinga ujinga tu!!

Le Mutuz!!

Je? wewe Kama mmoja wa makada wa CCM unahakikisha au unampango gani kuhakikisha kua mapungufu yaliyomo ndani ya chama yanapata ufumbuzi. Na sio hilo unaangalia kwa mtazamo upi gepu lilopo kati ya walio kua nacho na wasio kua nacho.
 
- Hakuna linalotuponza ila nia magomvi ya sisi wenyewe kwa wenyewe tu ndani ya CCM, lakini sio kwa sababu ya Chadema no way bado ni chama kidogo sana kwetu, bado mna safari ndefu sana mbele yenu kufikia CCM chama dume la mbegu!!

Le Mutuz!!
Chadema haiwezi kuifikia CCM alie tangulia katangulia, ila inauwezo wa kufanya yaliyo bora kuliko CCM. Mifano hai ipo mingi inayo onesha kua kutangulia sio kufika.
 
- Hakuna linalotuponza ila nia magomvi ya sisi wenyewe kwa wenyewe tu ndani ya CCM, lakini sio kwa sababu ya Chadema no way bado ni chama kidogo sana kwetu, bado mna safari ndefu sana mbele yenu kufikia CCM chama dume la mbegu!!

Le Mutuz!!
chama dume la mbegu zinazozalisha wala rushwa, watoa rushwa, wezi wa mali za uma, wauaji, , , , , , nisaidieni jamani wanaojua list ya mazao ya mbegu za hilo chama dume!
 
Na nini? chanzo cha migogoro ya nyie kwa nyie.
 
- Unajua ni rahisi sana kwa mlevi kudhani wengine wote ni walevi kama yeye, Chama chenye Wabunge 257, kinawezaje kuita chama chenye wabunge 46 kuwa ni a threat? I mean unasema nini bro huoni hakuna hoja hapo?

- A threat chama ambacho toka kianzishwe hakijawahi kushinda Urais, alianza Mtei, Makani, Mbowe, Slaa wote wakapigwa chini Urais na wananchi wa Tanzania, sasa leo unasema CCM tunakiogopa chama cha kushindwa kila mwaka? Pleaseee!!

- CCM wala hatuna habari kuwa mpo, na jana hamktajwa wala hakuna kiongozi wa CCM anayewweza kupoteza muda na chama mfu, sema mengine lakini sio ya hicho chama chenu yaani kama hakipo!! CCM mwendo ni mdundo bro!!

Le Mutuz!!
Mkuu wewe ni kilaza kabisa

1/Suala la CHADEMA kuwa kitisho(threat) liko wazi kwa kila mtu na mwenyekiti wa CCM amekuwa akifanya reference mara nyingi sana kuhusu CHADEMA tena kwenye mkutano mkuu, if CHADEMA is not a threat to CCM nani basi ni threat kwa CCM kwa sasa?

2/Suala la kulinganisha idadi ya wabunge si sahihi sana, huwezi kulinganisha wabunge 45 wa CHADEMA wenye upeo mkubwa na wabunge 257 wa CCM wenye ''mtindio wa ubongo''
Lakini pia idadi tu sio issue sana, kwa mfano Augustino Mrema alikuwa threat kwa CCM mwaka1995 na alikwenda kwenye uchaguzi akiwa hana hata mbunge mmoja, what about CHADEMA yenye wabunge 45 wengi wakiwa vichwa vya ukweli?

3/Acha kufanya upotoshaji, CHADEMA haikuwahi kusimamisha mgombea urais mwaka 1995 na mwaka 2000 na Mtei na Bob makani hawajawahi kugombea urais hata siku moja.
 
- Talking about kilaza, hebu jisome tena unasema Chama chenye wabunge 45 kinakubalika kuliko chama chenye wabunge 257? yaani hata kumalizia hoja zako mfu nimeshindwa! ha! ha! ha!

Le Mutuz!!
 
chama dume la mbegu zinazozalisha wala rushwa, watoa rushwa, wezi wa mali za uma, wauaji, , , , , , nisaidieni jamani wanaojua list ya mazao ya mbegu za hilo chama dume!

- Chama cha Dume la Mbegu, kinazalisha wabunge 257 na kinatawala miaka 50 bila tatizo na bado 50 mingine!, ndio maana yake!!

Le Mutuz!
 
- Hakuna linalotuponza ila nia magomvi ya sisi wenyewe kwa wenyewe tu ndani ya CCM, lakini sio kwa sababu ya Chadema no way bado ni chama kidogo sana kwetu, bado mna safari ndefu sana mbele yenu kufikia CCM chama dume la mbegu!!

Le Mutuz!!

ukweli wewe ni cerebral celebrity
 
- Unajua ni rahisi sana kwa mjinga kuamini wengine wote ni wajinga kama yeye, Wassira anaitwa Tyson toka akiwa Chadema vipi hukujua kwamba ni foolish age kuitwa Tyson? Viongozi wako wengi wanaitwa Jembe sasa hiyo foolish age ni nani wanaowaita au wewe usiyewaita au wao?

- Mengine ni waste tupu so nitakuchaia mwenyewe! ha! ha1 ha!

Le Mutuz!!
Mkuu uliza ili uelimishwe vizuri, inaonekana hujui matukio kabisa.

Jina la Tyson amepewa Wassira kati ya miaka ya 1995-2005 akiwa ameshatoka CHADEMA siku nyingi.

Mkuu hilo jina(Tyson) Wassira anaitwa na watu lakini hajiiti yeye mwenyewe, infact unaweza hata kugombana naye kama utakuja hadharani na kumwita Tyson, kwani lina sifa mbaya kwake kwa sababu lilitokana na kitendo cha kumkunja mtu na kumpiga ngumi.
 
- Chama cha Dume la Mbegu, kinazalisha wabunge 257 na kinatawala miaka 50 bila tatizo na bado 50 mingine!, ndio maana yake!!

Le Mutuz!

hapo unaharibu kaka! Miaka 50 mingine mnajihakikishia vipi? acha demokrasia ichukue nafasi yake. au mmnanjia mbadala ya kushinda?
 
- Talking about kilaza, hebu jisome tena unasema Chama chenye wabunge 45 kinakubalika kuliko chama chenye wabunge 257? yaani hata kumalizia hoja zako mfu nimeshindwa! ha! ha! ha!

Le Mutuz!!
Nakuacha kama ulivyo, maana sioni mantiki yoyote ya hoja yako.

Suala kama issue ya kuwa threat ni mpaka uwe na idadi ya wabunge wengi, what about NCCR ya Augustino Mrema mwaka 1995 ilikuwa big threat kwa CCM wakati haikuwa hata na mbunge mmoja?
 
hapo unaharibu kaka! Miaka 50 mingine mnajihakikishia vipi? acha demokrasia ichukue nafasi yake. au mmnanjia mbadala ya kushinda?
Mwache ajidanganye tu, wakati mwenyekiti wake kichwa kinamuuma hana cha kufanya, huyu William anatapika ugoro humu.
 
JUMANNE, NOVEMBA 20, 2012 07:05 NA BENJAMIN MASESE, DAR ES SALAAM

*Atangaza kutumia helkopita,
*Chadema nao wakimbilia Karagwe

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimetangaza kuanza rasmi ziara ya kikazi mikoni ili kuangalia hali halisi ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo. Katika ziara hiyo, CCM imepanga kutumia helkopita ili kufikia maeneo yote ambayo imekusudia.

Ziara hiyo,imekuja siku moja baada ya Sekretarieti mpya kuchaguliwa wiki moja iliyopita mkoani Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye alisema ziara hiyo itaongozwa na Katibu Mkuu, Abdurahman Kinana.

Alisema Kinana, ataongozana na wajumbe wa Sekretarieti na baadhi ya mawaziri ambao kila mmoja kwa nafasi yake, atawajibika kuwaeleza wananchi mikakati na mipango ya utekelezaji wa ilani na ahadi za CCM.

"Ziara hii, itaanza kesho katika mkoa wa Mtwara, hapo tutaangalia suala la bandari na korosho, ambapo chama kitakuwa na nafasi yake ya kueleza na mawaziri wanaohusika na bandari na korosho nao watawajibika kueleza wananchi.

"Novemba 22, tutakuwa Sumbawanga na tutajikita upande wa barabara na viwanja vya ndege… kazi itakuwa ile ile ya kukutana na wananchi na kuelezana ukweli,

"Siku inayofuata, tutakuwa Geita huko tutaangalia suala la madini na jinsi wananchi wanavyonufaika, waziri mwenye dhamana ataeleza hatua wanazochukua na mwisho wa ziara yetu itakuwa mkoani Arusha,tutajikita katika uwekezaji viwandani na ajira,"alisema.

Alisema baada ya kumaliza ziara hiyo, watarudi kujipanga tena ili kuandaa safari ya mikoa mingine.

Alisema suala la kujivua gamba bado litaendelea kufanyiwa kazi na kuhakikisha chama kinabaki na wanachama wasafi, wasiopenda na kutoa rushwa na wenye maadili mema.

Akizungumzia suala la kuwapo kwa propaganda za kudai CCM imechukua busara za Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa kutaka elimu ya sekondari kuwa bure na kupunguza kodi katika vifaa vya ujenzi, Nape alikana.

Alisema sula la elimu bure sio jambo geni, lilikuwapo tangu enzi za Hayati Mwalimu Nyerere.

CHADEMA

Wakati huo huo, Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), inatarajia kuanza katika Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganaizesheni, Benson Kigaila alisema M4C wanayoipeleka Karagwe ni mkakati wa chama hicho kuwajengea uwezo viongozi wake kuanzia ngazi ya kata hadi mkoa.

Alisema kuna mabadiliko kidogo ya M4C iliyozoeleka ambayo hufanywa na viongozi wa kitaifa.

Alisema mkakati wa sasa, ni wa kisayansi umelenga kutoa mafunzo kwa viongozi wa ngazi ya mikoa 32,kuanzia Novemba 22 hadi 23.

Baada ya hapo watapelekwa katika ‘shamba darasa' la wilaya nzima ya Karagwe yenye majimbo mawili na kata 32 ili kuwapima kama wameleewa sawasawa M4C.

"Huu ni mkakati mpya wa M4C, tutawakutanisha viongozi 64 wa mikoa yote ya kichama katika wilaya moja ya Karagwe, lengo ni kujenga uwezo wa viongozi wetu wa mikoa yote 32 ya kichama.

"Baada ya siku mbili, viongozi watagawanywa katika timu 10 katika kata 42 kwa muda wa siku mbili, kila moja ili wafanye kwa vitendo yale waliyofundishwa darasani, na baadaye tutawarudisha tena darasani kuona kama wameiva sawasawa.

Ongeza UMAKINI WJM. Unaweza kuwa msaada mkubwa wa CCM humu JF. Wenzako akina Nape wanachungulia kidogo na kuaga. Wakirudi, wanarudi kama "guests". Acha kuhangaika na watu, hangaika na masuala. Watu wanakuja na kupita.
 
Wangekuwa wanakwenda mikoani/wilayani/vijijini kufungua miradi ambayo tayari imeboresha maisha ya wanaichi ingeeleweka. Sasa wanakwenda na maneno matupu. Kule kwa Hawa Gasia baada ya kubinafisha kiwanda cha korosho ambacho sass hakifanyi kazi na wakulima wa korosho kukosa mahali pa kuuza korosho zao watawaeleza nini si wataishia kuzomewa.
 
- Hakuna linalotuponza ila nia magomvi ya sisi wenyewe kwa wenyewe tu ndani ya CCM, lakini sio kwa sababu ya Chadema no way bado ni chama kidogo sana kwetu, bado mna safari ndefu sana mbele yenu kufikia CCM chama dume la mbegu!!
Le Mutuz!!

Chadema chama kidogo wapi wewe wa kushindwa!? vikao vyenu vyote kuanzia NEC hadi mkutano mkuu mlikuwa mnaizungumzia Chadema, mnapanga mikakati na mipango ya kukabiliana na Chadema halafu un ajitoa akili kwamba Chadema ni chama kidogo?

Akili matope kabisa wewe, mbona hatujawahi kusikia mkiizungumzia cuf, tlp, nccr mageuzi, updp ama cck? Sisi hatuhitaji kuifikia ccm kwakuwa imejaa rushwa na uchaguzi wa chama chenu wa hivi karibuni ni ushahidi tosha. Hatuhitaji kuifikia ccm kwakuwa hakuna chochote cha maana ambacho mtu makini anaweza kujifunza toka ccm kwa sasa, vichwa vya kuku ndio bado wanajifunza kwa ccm na bado wana matumaini na chama cha ufisadi.
 
Abdulrahman Kinana atakuwa na maswali ya kuyatolea ufafanuzi katika ziara zake za mikoani; kwa mfano:
1. Laundry machines za hospitali ya mkoa Mt. Meru Arusha
2. Mkataba wa mbuga ya Loliondo na usafirishaji wa wanyama nje ya nchi.
3. Nani mmiliki wa kampuni ya Ortello busines corporation
4. Kifo cha mwandishi Stan Katabaro
5. Kwa nini alizikimbia siasa za Arusha tangu mwaka 1995
6. Kitu gani kimetokea miezi takribani miezi mitatu hivi baada ya kuutangazia umma kwamba anastaafu siasa na sasa amerudi center stage tena?!
7. Kwa nini anafikiri watu wamesahau historia yake hapa nchini na kama haitarudi kumtafuna kisiasa na kumchafua mbele ya jamii na kwa hiyo kumfanya ashindwe kuwa katibu mkuu effective.
8. Je anafahamu nini kuhusu wimbi la kuingiza wasomali hapa nchini,
 
*Atangaza kutumia helkopita,

Kweli ccm vichwa vya nazi, ndio wa kwanza kupiga kelele kwamba Chadema inafuja fedha kutumia helikopta lakini sasa wanaonekana kujua utamu wa kutumia helikopta, kinana naye ameamua apande japo helikopta wakati huu bado anaonekana mpya mpya, huenda kwenye kampeni za uchaguzi mdogo asipate nafasi ya kuwepo.

Kila siku wanapiga makelele kwamba wamejenga barabara za lami kila mkoa kwanini wasisafiri kwa magari ili wajionee kwa macho yao utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa barabara badala ya kwenda kwa helikopta kukagua ujenzi wa barabara.

Hata hivyo janja yao kwisha jua huko Sumbawanga "wanakokwenda kukagua barabara" ni kwamba wanakwenda kufanya kampeni na maandalizi kwa ajili ya kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la sumbawanga mjini.

CCM imechukua busara za Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa kutaka elimu ya sekondari kuwa bure na kupunguza kodi katika vifaa vya ujenzi. Nape alisema suala la elimu bure sio jambo geni, lilikuwapo tangu enzi za Hayati Mwalimu Nyerere.

Kweli nape ni zaidi ya vuvuzela, mara hii tu ameshasahau kwamba wao ccm ndio walikuwa wakitetea sera ya kugharamia elimu kwa kusema enzi za Nyerere ni tofauti na sasa ambapo huduma za kijamii haziwezi kamwe kutolewa bure.

Wao wakubali tu kwamba Chadema ina sera nzuri, wamekuwa wakizitumia na wataendelea kuzitumia, muhimu ni wao ku acknowledge tu. Si ajabu hata hilo la kuondoa kodi katika vifaa vya ujenzi ili kushusha bei yake kuwawezesha wananchi wengi kujenga makazi bora atasema lilikuwepo toka enzi za Nyerere.

"Siku inayofuata, tutakuwa Geita huko tutaangalia suala la madini na jinsi wananchi wanavyonufaika, waziri mwenye dhamana ataeleza hatua wanazochukua

Yaani bila aibu ccm mnakwenda kuwafanyia usanii wananchi wa Geita ambao miaka yote serikali yenu imeshiriki kuwakanbdamiza kwa kuwahamisha/kuwapora maeneo yao bila malipo na kuyakabidhi wawekezaji, kama hiyo haitoshi policcm wamekuwa wakiwapiga risasi na kuwaua wananchi kila siku huko Geita halafu leo bila aibu mnasema mnakwenda kuangalia suala la madini na jinsi wananchi wanavyonufaika. Kwa hali kama hii mkipopolewa mawe huko Geita msijemkasema Chadema ndiyo imewatuma wananchi wawapopoe mawe.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom