Ziara ya Rais Samia nchini Kenya, Mama anakosea

Shida sio kuuza nje..Tunauza nje kwa faida ipi je sisi wenyewe imetutosheleza kwanza?

Kama uwekejazi wa gas ulitokana na kodi za watanzania basi watanzania hao hao kwanza ndio wafaidike na kodi zao.

Tuuze gas baada ya sisi kuwa imetutosheleza kile kinachozidi (surplus)ndio kiuuzwe.

Viwanda vyetu wenyewe vinahitaji gas lakini gas hiyo hiyo hawapewi..inakuwaje unakwenda kumpa jirani yako!
Hivi unadhani hakuna analysis imefanywa mpaka kufikia uamuzi huu? Muandishi anaelekea anachuki na uongozi uliokuwepo na hata conclusion yake inaonyesha hili pale anapotaja aachiwr Tanganyika yake
 
Napenda kuandika kidogo tu kulingana na uwelewa wangu juu ya Ziara ya Mama nchi Kenya na mikataba mlio tiana sign.

1. Ujenzi wa bomba la gas kutoka Tanzania kwenda Mombasa kwa ajili ya matumizi ya viwanda nchini Kenya,hapa mama unefail pakubwa sana maana yake nikwamba bidhaa za Kenya zitakuwa zinazalishwa kwa gharama nafuu zaidi na kuteka soko la Africa Mashariki kuliko Tanzania. Tutarudi miaka ya nyuma tena kila kitu Made in Kenya.

a. Hii sera yetu ya viwanda itakufa maana hatuweza kushindana tena na product kutoka Kenya na vijana wetu watazidi kuwa wachuuzi wa bidhaa kutoka nje.

b. Kenya itatumia mwanya huu kuvutia wawekezaji kutoka nje kuwekeza Kenya kuliko kuja kuwekeza Tanzania.

c. Tunasafirisha gas kama kuna surplus ya viwanda vyetu na matumizi yetu kama Taifa.Viwanda vyetu bado vinahitaji nishati ya gas lakini bado upatikanaji wake umekuwa mgumu na kwa gharama kubwa

d. Kenyatta amecheza karata yake vizuri katika ujenzi wa gas kuliko Mama sijui washauri wake wamekwama wapi natarajia kuona Kenya ikinufaika zaidi katika utawala wa Mama kuliko kipindi chochote kile katika historia ya Tanzania na Kenya.

2. Ushirikiano wa anga..hapa Kenyatta anatafuta namna ya kuisaidia Kenya airways..inakwenda ku dominate soko na anga tena kama huko nyuma.hapa kumbuka faidia kubwa ya Kenya Airways inatokana na safari za Tanzania. Dsm, Zanzibar na Kilimanjaro.

Hapa tutalajie Air Tanzania ikifa kifo cha mende kutokana kutoweza kumudu ushindani na Kenya airways. Otherwise kufanyike changes za haraka katika Management ya Air Tanzania.

3. Soko la utalii hapa Kenyatta amecheza vizuri kama pele.
Tutalajie kuona vijana wetu wakiwa watazamaji kama kipindi cha nyuma na soko la utalii nikirudi mikononi mwa wakenya tena.(hapa kwenye utalii wenye fan zao wanaweza kudadavua kwanini Kenyatta amecheza kama Pela)

4. Biashara sioni jipya ni yale yale, hapa Mama ametoka 0-0

Note: Mama washuri wake wamshauri vizuri kabla yakwenda kufanya mikataba kwa niaba ya Watanganyika. Otherwise akubali kutuachia Tanganyika yetu!
Mkuu uko vzr,nyongeza ni kuwa mama hajui anakotupeleka,hata njia pia nafkiri hajui ya tunakoenda
 
Bomba la gesi kutoka Mtwara mpaka Kinyerezi unajua gharama zake?? Sasa unavyosema eti tulipeleke kila kona ya nchi hii unadha ni shughuli ndogo??
Bwala la Nyerere ni pesa ngapi? Tumewezaje?

LNG inaenda kusainiwa, ni $30bn, kwaajili ya?

Umewahi kusikia kuwa tuna visima havitoi tena gesi, TPDC wanachimba vingine?

Umesikia kuwa Msumbiji wanayo gesi nyingi zaidi yetu na kwamba mkondo unatiririkia kwao kutoka huku?

Hii ni sawa na kuzungumzia madini, leo hii yanatusaidiaje? Kwenye era hii ya technology unapambana kuuza raw materials?
 
Kunawakati tunapaswa kujadili maswala ya kitaalaam kwa utulivu na weredi ,hadi nimetamani Jf ingelikuwa na kipengele cha mtu kuruhusiwa kujadili hoja kutokana na TAALUMA yake , hapa unakuta mtu kwakuwa tu anajua kusoma na kuandika anajikuta anajadili kilimo huku akiwa hata hajui utofauti wa aina za mbolea ,eneo la Uchumi ni pana Sana na siyo kila mbinu nilazima ianze chino ,zingine ukija kwenye kuwagawia wa NDANI unakuta tayari ushafanya mlipuko mkubwa na wenye tija .

Tanzania iko hapa ilipo kwa makosa mengi yakiwemo tunayojihubiria hapa.

Watu wenye fikra za aina wzeeka ndiyo huwa mnakuwaga wachawi tu , ukiona mtoto wa yuko smart kuliko wa kwako unaona the best option ni kumdedisha tu au umnyime baadhi ya mahitaji ambayo yqtamfanya asongembele zaidi kwakuhisi wakakwako watapoteza u ora nakudharilika which is not true badala ya kufurahia uwepo wake na huku ukiangalia namna nzuri ya kuutumia uwepo wake ili na wa wajamii yako wawe bora hata kumpita .

Hii tabia yakukumbatia tulivyonavyo haiajawahi kuleta matokeo chanya zaidi ya kutudumaza tu kifikra .

Kanuni ya Biashara inatutaka tuuze tulivyonavyo huku tukizielekeza faida kwenye vitu vitakavyotuzidishia faida maradufu .

Kwa wasiyojua sera yetu ya Uchumi haiwezi kutatuliwa kwa uwepo wa gas bali maboresho mazito ya sera yetu ya elimu (kutoka kwenye elimu ya kukarili kwenda kwenye elimu ya utambuzi (creming education to cognitive education) elimu itakayohakikisha haizalishi wategemezi kwa Taifa kama ilivyo sasa kundi la kuanzia darasa la saba kuwa mzigo tu kwa Taifa , wahitimu wa kidato cha nne kutokuwa na sifa siyo tu za kuajirika lakini hata tu wenyewe wakawa hawana uwezo wakujiajiri nje ya kuwa na sifa za nyongeza achilia mbali cheti cha muhitimu wa chuo kikuu kukosa thamani ya kutumika kama collateral itakayomuwezesha walau kukopesheka na kupata mtaji wa kuanzishia ile taaluma ambayo serikali imemuidhinishia ufaulu (refer to China).

Mama anaendelea kufanya vizuri sana hebu tujipe utulivu na tumpe muda .

Tusiishi kwa kukarili ,Dunia inakwenda kasi sana .
Umeongea meengi lkn hujasema lolote,jaribu kufikiri kwa bidii,na uongeze umakini unaposoma mada,sio ukurupuke tuu kuandika na kujibu usichokijua,
 
aaah kiongoz tusitishane hivi ni kweli aweze mkenya nishindwe mbongo ambayo nipo naye hata km ngap haifik
Mkenya inajenga nchi kwenda kuzalisha Umeme uende viwandani..

Sisi tulijenga kutoka Mtwara mpaka Kinyerezi ambako unazalishwa umeme unaouona unatumika viwandani.

Hapo achilia mbali gesi ambayo imefikishwa Mikocheni majumbani mpaka kwenye viwanda ambayo iko kwenye majaribisho. Fuatilieni vitu acheni kuwa nyumbu
 
1. nikwamba bidhaa za Kenya zitakuwa zinazalishwa kwa gharama nafuu zaidi na kuteka soko la Africa Mashariki kuliko Tanzania. Tutarudi miaka ya nyuma tena kila kitu Made in Kenya. hii fikra ya namna gani? kwa hiyo gesi ibaki huko tusiiuze kwa kuwa tu Kenya watafaidika?

a. Hii sera yetu ya viwanda itakufa maana hatuweza kushindana tena na product kutoka Kenya na vijana wetu watazidi kuwa wachuuzi wa bidhaa kutoka nje. Yaani viwanda vyetu vitakufa kwa kuwa kenya itapata gesi na kukuza vyao? Kwanza viwanda vipi hivyo ambavyo vitakufa, vife mara ngapi maana na hii gesi tuliyo nayo vinakufa na vimekuwa vikifa. Hoja mfu sana na imekaa ki wivu wivu tu. Ni kama unauza vitabu then unaamua kuto muuzia mtoto wa jirani kisa eti atafaulu kuliko wako - ujinga sana huo.

b. Kenya itatumia mwanya huu kuvutia wawekezaji kutoka nje kuwekeza Kenya kuliko kuja kuwekeza Tanzania. Dah hizi akili hizi

c. Tunasafirisha gas kama kuna surplus ya viwanda vyetu na matumizi yetu kama Taifa.Viwanda vyetu bado vinahitaji nishati ya gas lakini bado upatikanaji wake umekuwa mgumu na kwa gharama kubwa. hii ndio ikufanye usiuze kenya gas?

d. Kenyatta amecheza karata yake vizuri katika ujenzi wa gas kuliko Mama sijui washauri wake wamekwama wapi natarajia kuona Kenya ikinufaika zaidi katika utawala wa Mama kuliko kipindi chochote kile katika historia ya Tanzania na Kenya. Ulitaka Kenya isinufaike na ujirani ulitaka indoofike, kila nchi inapambana kutumia fursa na Tanzania haijanyimwa kupambana kutumia fursa zilizopo

2. Ushirikiano wa anga..hapa Kenyatta anatafuta namna ya kuisaidia Kenya airways..inakwenda ku dominate soko na anga tena kama huko nyuma.hapa kumbuka faidia kubwa ya Kenya Airways inatokana na safari za Tanzania. Dsm, Zanzibar na Kilimanjaro. Hamna kitu umeandika hapa

Hapa tutalajie Air Tanzania ikifa kifo cha mende kutokana kutoweza kumudu ushindani na Kenya airways. Otherwise kufanyike changes za haraka katika Management ya Air Tanzania. Kwani Air Tanzania kwa sasa iko hai?

Hebu tujaribu kufungua akili zetu na kuacha mambo ya kijinga ya wivu. Pambana na ushindani kwa mbinu za kisayansi na kishawishi sio ujinga ujinga wa wivu wivu tu
 
Bwala la Nyerere ni pesa ngapi? Tumewezaje?

LNG inaenda kusainiwa, ni $30bn, kwaajili ya?

Umewahi kusikia kuwa tuna visima havitoi tena gesi, TPDC wanachimba vingine?

Umesikia kuwa Msumbiji wanayo gesi nyingi zaidi yetu na kwamba mkondo unatiririkia kwao kutoka huku?

Hii ni sawa na kuzungumzia madini, leo hii yanatusaidiaje? Kwenye era hii ya technology unapambana kuuza raw materials?
Hivi unafahamu hata gesi inatumikaje? Gesi inazalisha Umeme ambao ndio huo unatumika viwandani. Sasa niambie ni wapi palitakiwa kujengwa kiwanda ukakosekana umeme..

Au niambie ni wapi nchi hii Umeme haujafika.. Mbona mnakuwa wajinga namna hii??

Kwasasa hatuna shida ya umeme ndio maana REA inapeleka mpaka vijijini huko. Gesi yote hatuwezi kutumia wenyewe, lazima tuuze nyingine itupatie pesa zitakazotusaidia kutoa huduma zingine muhimu kwa wananchi..

Mzalishaji mkubwa wa gesi duniani Russia hatumii gesi yote mwenyewe, nyingi anaiuza kwa mahasimu wake Ulaya. Unafikiri yeye ni mjinga na wewe ni mwerevu sana??

Unavyoongea hapa ni kama hiyo gesi sisi hajatufaidisha chochote of which ni uongo na uzandiki. Zaidi ya asilimia 60 ya umeme wetu Tz kwa sasa unatokana na gesi..
 
WAJAA PITINE HIVI, HAMNA KUPATA BILA KUTOA

BIASHARA YA GESI INAFANYIKA DUNIA NZIMA NA NI BORA TUUZIE MAJIRANI KULIKO KUUZIA TU NCHI ZA MBALI,

FAIDA.
KUIMARISHA UHUSIANO WA KINCHI (BILATERAL RELATIONS)
KUPATA FEDHA ZA KIGENI
BALANCE OF TRADE

JUA GESI ITAYOUZWA KENYA NI JUST FRACTION YA AKIBA TULIONAYO
NA HAWEZI KUITUMIA KUVUTIA UWEKEZAJI WA PETRO CHEMICAL INDUSTRIES AMBAZO TANZANIA ITAZIPATA REF 20B DOLLAR LNG PROJECT
 
Napenda kuandika kidogo tu kulingana na uwelewa wangu juu ya Ziara ya Mama nchi Kenya na mikataba mlio tiana sign.

1. Ujenzi wa bomba la gas kutoka Tanzania kwenda Mombasa kwa ajili ya matumizi ya viwanda nchini Kenya,hapa mama unefail pakubwa sana maana yake nikwamba bidhaa za Kenya zitakuwa zinazalishwa kwa gharama nafuu zaidi na kuteka soko la Africa Mashariki kuliko Tanzania. Tutarudi miaka ya nyuma tena kila kitu Made in Kenya.

a. Hii sera yetu ya viwanda itakufa maana hatuweza kushindana tena na product kutoka Kenya na vijana wetu watazidi kuwa wachuuzi wa bidhaa kutoka nje.

b. Kenya itatumia mwanya huu kuvutia wawekezaji kutoka nje kuwekeza Kenya kuliko kuja kuwekeza Tanzania.

c. Tunasafirisha gas kama kuna surplus ya viwanda vyetu na matumizi yetu kama Taifa.Viwanda vyetu bado vinahitaji nishati ya gas lakini bado upatikanaji wake umekuwa mgumu na kwa gharama kubwa

d. Kenyatta amecheza karata yake vizuri katika ujenzi wa gas kuliko Mama sijui washauri wake wamekwama wapi natarajia kuona Kenya ikinufaika zaidi katika utawala wa Mama kuliko kipindi chochote kile katika historia ya Tanzania na Kenya.

2. Ushirikiano wa anga..hapa Kenyatta anatafuta namna ya kuisaidia Kenya airways..inakwenda ku dominate soko na anga tena kama huko nyuma.hapa kumbuka faidia kubwa ya Kenya Airways inatokana na safari za Tanzania. Dsm, Zanzibar na Kilimanjaro.

Hapa tutalajie Air Tanzania ikifa kifo cha mende kutokana kutoweza kumudu ushindani na Kenya airways. Otherwise kufanyike changes za haraka katika Management ya Air Tanzania.

3. Soko la utalii hapa Kenyatta amecheza vizuri kama pele.
Tutalajie kuona vijana wetu wakiwa watazamaji kama kipindi cha nyuma na soko la utalii nikirudi mikononi mwa wakenya tena.(hapa kwenye utalii wenye fan zao wanaweza kudadavua kwanini Kenyatta amecheza kama Pela)

4. Biashara sioni jipya ni yale yale, hapa Mama ametoka 0-0

Note: Mama washuri wake wamshauri vizuri kabla yakwenda kufanya mikataba kwa niaba ya Watanganyika. Otherwise akubali kutuachia Tanganyika yetu!
Tutazidi kumkumbuka mwendazake kwa uzalendo na uthubutu wake kwa nchi hii.
 
Mama washuri wake wamshauri vizuri kabla yakwenda kufanya mikataba kwa niaba ya Watanganyika. Otherwise akubali kutuachia Tanganyika yetu!
kwa nini maneno haya umeyaweka mwisho wakati ndio kiini cha uzi wako?

ANY WAY

Tanganyika (Tanzania) Tunayo Gesi nyingi tuu, na tunatafuta soko la kuuza nje, kenya wameonesha nia ya kununua Gesi yetu wewe unaanza kufikiria matumizi ya Gesi Viwandani. Hivi unadhani Kuleta Tanzania Ya Viwanda ni kama Kulala na kuamka?

Kenya imekuwa ni nchi ya viwanda tokea Ukoloni, na Tanzania imekuwa nchi ya uzalishaji Malighafi tokea Ukoloni,
Nyerere alijitutumua kujenga viwanda vingi tuu hatimae vyote vimetufia mikononi. Kulikuwa Mwatex,Sugura tex,Urafiki , Kiwanda cha chuma Tanga, Kiwanda cha Mbolea Tanga, KIWANDA CHA KARATASI ,Sao Hill kule Mgololo, Na vingine Vingi ambavyo vimeishia kupigwa mnada na Mzee mkapa,kiwanda cha Kusindika Nyama ya vikopo kawe DSM, General Tire Arusha, Kiwanda cha viatu Bora DSM nk.

Siasa ya Ujamaa iliuwa viwanda vya serikali kwa kukosa uweledi na kukosa Mfumo mzuri wa uchumi wa viwanda.

Sasa kama leo tutanzisha Viwanda TZ si tunayogesi ya kutosha? tutaingia kwenye Ushindani tuu.

Lakini nadhani wewe unamtafutia Mama yetu Soni ili Aonekana kama vile haitakii mema Tanganyika, na kwa muktadha huu unaleta kaubaguzi fulani hivi ka Uzanzibari na Utanganyika kwa mbaaali.
Mwachemama afnye kazi,
Binadamu hatuwezi kuwa na mitazamo inayofanana .
Tupokee tuu mtazamoa wake Kiuchumi.
 
Mwanamke huongozwa na mwanaume! Eti leo hi mwanamke anaongoza wanaume zaidi ya milion, kadili muda unavyozidi kwenda tutegemee kufeli zaidi.
Baba yako Nyumbani anaongozwa nanai? Kama si mama ?
Na wewe umefikia hapo kwa msaada mkubwa w Mama ,
Ki ukweli aliyekosa Malezi ya Mama Mwema hana utu kabisa,
Wacha Watanzania Tulelewe na mama , Wacha Tunyonye kidogo ,tumechoka na Mikaripio ya Baba Yule.
 
Acha kudanganya watu,watanzania wengi tumekuwa masikini kwa sababu ya kutumia nishati duni kama mikaa na kuni. Leo hii umeme ni ghali kwa matumizi ya multpurporse ukija kwenye ges ndo balaa kabisa, laiti kama gesi ingesambazwa majumbani na viwandani tusengekuja hapa kulalamika.gesi ni ya kwetu,itutosheleze kwanza sisi wenye nayo ndo kisha tuitoe nje kama kama itatosheleza . Mfumo ni uleule hatukuwauzia mahindi wakenya kabla hatukujihakikishia kuwa tuna mahindi ya kutosha nchini.
Wewe unachojua ni neno Gas tu mambo mengine hutaki kujua wala kujiuliza yatawezekana vip.unaongea tu porojo za mdomoni ukiambiwa weka mipango mezani ya hicho unachokisema huna chochote unachokijua zaidi ya kukariri tu gas gas.Ili tuweze kwenda mbele lazima kwanza tuondokane na ubinafsi na umaskini wa mawazo.Sasa wewe hela huna unafikiri hicho unachowaza kitatekelezeka vip bila kuuza kidogo ili upate pesa zakufanya mambo mengine au unafijiri kuwekeza kwenye gas ni kama biashara ya mandazi.
 
Back
Top Bottom