Ziara ya Rais Samia Mtwara Yaanza Kujibu

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Meli iliyobeba makasha 225 ya kampuni ya CMA-CGM SAIGON imewasili katika bandari ya Mtwara kwa ajili ya kusafirisha shehena ya korosho ghafi katika msimu wa 2023/24.

Akizungumza leo Oktoba 22,2023 baada ya kupokea Meli hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mwanahamisi Munkunda, amesema kuna Meli nyingine zaidi ya Saba zinatarajiwa kuwasili katika Bandari hiyo mwezi Novemba mwaka huu, kwa ajili ya kushusha Makasha.

Naye meneja wa Bandari ya Mtwara, Ferdinand Nyathi, amesema mbali na kampuni ya CMA-CGM, yapo mengine mengi yamejipanga kushusha makasha katika Bandari hiyo.


View: https://www.instagram.com/p/Cyu9vwINgi6/?img_index=1
 
Back
Top Bottom