Ziara ya Paul Makonda yaingia shubiri Bagamoyo na kuibua mapungufu ya Serikali ya CCM

19 January 2024

WAFANYAKAZI WA UVCCM WAPEWA MWEZI MMOJA KULIPA MADENI WALIYOKOPA BENKI YA DCB Commercial Bank Plc

1705707381122.png

Wafanyakazi hao 132 walikopa jumla ya shs. 600,000,000 .... mikopo hiyo ilichukuliwa miaka 10 iliyopita na mbali ya kufuatiliwa wameshindwa kujitokeza hivyo ndani ya mwezi mmoja majina yao yataanikwa hadharani baada ya njia za chini chini kutunza siri zao kushindikana mkurugenzi mtendaji wa DCB Commercial Bank Plc amewatahadhatisha makada wa UVCCM ...
 
Umiliki ardhi ambayo ndiyo mtaji mkubwa wa wananchi ndiyo tatizo.

Serikali haijaweza kuwamilikisha ardhi wananchi ili waweze kukabiliana na matapeli wapora ardhi ambao ni wana CCM

Wananchi wote wakipata haki miliki za ardhi ni nyenzo kamili ya kubambana na wanaopora au kuwahamisha wananchi kwa nguvu bila fidia stahiki


Katiba mpya inayompa mwananchi mmoja mmoja umiliki wa ardhi kisheria ni muhimu. Hili serikali ya CCM ngazi zote toka TAMISEMI hadi serikali kuu Dodoma imeshindwa.

Bado kuna matatizo mengi mengine kama maji safi n.k nayo CCM imefeli ...
Mbona wenye hati miliki wengi wameporwa Ardhi zao?
Hati miliki nchi hii hazina thamani
Siasa za CCM ndiyo hatamu

Makonda akiamua nyumba ya GSM iwe yake sawa
Wana CCM walivamia shamba la Mo sawa
Wakivamia Ardhi ya Twigs cement sawa
Wakivamia shamba la mstaafu wa CCM mwenzao kule Ndachi dodoma sawa
Yaani Nyani akimula Nyani mwenzake sawa
Kama Taifa tuna kazi kweli kweli kubadili mfumo tulio uachia ukaota mizizu
 
Makonda akiamua nyumba ya GSM iwe yake sawa
Wana CCM walivamia shamba la Mo sawa

Kwa kifupi CCM wameteka nyara mifumo yote yaani mfumo wa jinai haki ( criminal justice system), mfumo wa uchaguzi, mfumo wa demokrasia n.k n.k

Pia chini ya utawala wa chama hiki kongwe, wahalifu wanapewa vyeo ndani ya chama na katika vyombo vizito vya serikalini ...


CCM imeshindwa kubana matumizi makubwa ya anasa ya kuwagharamia viongozi ..... pesa hizo zingeweza kutumika kutoa huduma bora za kijamii kama afya, elimu, maji kwa wote ....

1705713425648.png
 
19 January 2024
Bagamoyo, Pwani

PAUL MAKONDA AKUTANA NA UGUMU ULIOPITILIZA UNAOSHINDWA KUPATIWA UFUMBUZI NA MFUMO WA UTAWALA WA SERIKALI YA CCM


View: https://m.youtube.com/watch?v=om38fxu03Yc

Katibu wa uenezi, itikadi na mafunzo wa CCM Bw. Paul Makando leo hakuamini macho yake kuona jinsi ya mfumo wa serikali na chama dola kongwe CCM usivyosomana


Wananchi wadai toka mwaka 1984 hadi leo mwaka 2024 takribani miaka 40, matatizo yao hayajapata ufumbuzi. Wananchi waonesha mavazi na mashati yao yalivyo na viraka na matobo kama vile yameliwa na panya kutokana na kubakia ktk lindi la umasikini baada ya kuporwa ardhi na mazao yao ..

Ma DC wapya wanaletwa pamoja na wakurugenzi wa wilaya lakini wanaona kuwa wote hao wameshindwa kazi kutokana na kila miaka miwili mitatu wanaletewa viongozi wageni wasiofahamu changamoto zinazohitaji kutatuliwa na wateuliwa hao wa rais .

Vurugu zatokea na katibu ya CCM uenezi, itikadi na mafunzo akimbiwa na watendaji waliowekwa kupitia uchaguzi ulioporwa wa mitaa na vijiji

Wazi inaonesha kuwa hitaji la katiba mpya ya nchi ndiyo itakuwa ufumbuzi wa kuweza kero za wananchi kutatuliwa ngazi ya vijiji, wilaya na mkoa badala ya kusubiri ziara za wageni kama kina Paul Makonda na watendaji wengine wenye makao yao huko Dodoma na Dar es Salaam....

Wazee walilia bima ya Afya tegemezi ya watoto wao kufutwa na kumtaka Paul Makonda kumfikishia ujumbe mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania irejeshwe maana wazee hao sasa hawawezi kupata huduma za afya kupitia bima ya vijana wao ....

Wananchi pia walalamikia hukumu za Mahakama kupuuzwa na viongozi wa kata ya Mapinga Bagamoyo ...

Viongozi wanakimbia wananchi hawataki kabisa kuwahudumia wananchi ....

Na bado! CCM itakufa kifo kibaya
 
Mwembeni, Tanga

MAKONDA AWA MKALI WANANCHI KULAZIMISHWA UJENZI WA KITUO CHA AFYA

View: https://m.youtube.com/watch?v=IzRI8hWUql8

Mkurugenzi wilaya ya Pangani abanwa hakuna kituo cha afya miaka miwili .. zahanati ilijengwa chini ya viwango ikaanguka hivyo sasa juhudi zinafanyika ....

Paul Makonda ambana mkurugenzi ni sheria ipi inayotaka wananchi wachangie ujenzi wakati fedha za serikali tayari zimetolewa ...

Paul Makonda asema kodi inayokusanya ni hela ya wananchi hivyo kuwabana michango tena na halmashauri siyo sahihi kisheria na serikali tayari imetoa fedha nyingi ....
 
Makonda akutana na maswali magumu yaliyomtoa jasho kuhusu mfumo wa bima ya afya

1705809259255.png
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom