Elections 2010 ze komedy waibua mbuge mtarajiwa!

minda

JF-Expert Member
Oct 2, 2009
1,068
65
wakuu,
nimekuwa mfuatiliaji wa karibu sana wa kipindi cha vichekesho almaarufu ze komedy.
huyu jamaa anayejiita bepari la kihaya,(kila sehemu yake ya kujidai inapafika), hakosi kumtaja abdul mteketa; mzee wa kilombero, ( mzee wa english medium...)

japo nililizoea hilo jina hilo bila kufahamu undani wa mhusika; sasa nimepata insight kwamba huyo mteketa, (ambaye amepitishwa na ccm kugombea ubunge kupitia chama hicho kwenye jimbo la uchaguzi la kilombero ), alikuwa na mahesabu ya mbali sana kwani jina lake liliuzika sana kupitia ze komedy.

kama dhana yangu hiyo itakuwa sahihi, basi huyo mteketa atahitaji pongezi zangu(zetu?) kwa kupiga penati ya mbali na kufunga goli ndani ya chama chake bila ya watu kugundua janja hiyo.
 
Hatukubaliiiiiiiiiiiiiiiiiiiii alianza kampeni mapema, takakkuru hawajaona hili? Lazima ahojiwe.
 
SI YEYE TU HATA AMOSI MAKALA kILA BENDI MJINI LAZIMA IMUIMBE
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom