Ze komedi -vs- Futuhi

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,887
2,771
wadau, hapa nani zaidi? kwa upande wangu nimekuwa nikiwatazama wote ila navutiwa na futuhi kwa mambo kadhaa. kwanza hawatumii lugha kali kama ze komedi, pili wanatumia wanawake katika nafasi za wanawake, tatu ni more creative, nne kuna rika tofauti, n.k. hayo ni yangu sijajua yako
 
Futuhi unaweza kuangalia na familia yote pamoja lakini wale ndugu zangu wa ze komedi huwezi, hasa siku hizi maana lugha wanazotumia si nzuri. Ze komedi wana vipaji sana lakini wanavitumia vibaya. Tunataka kikundi ambacho kitafurahisha na kutoa elimu kwa jamii.
 
ni kweli, ze komedi inafika wakati hutamani kuangalia. nadhani wanajisahau wakati flani
 
wadau, hapa nani zaidi? kwa upande wangu nimekuwa nikiwatazama wote ila navutiwa na futuhi kwa mambo kadhaa. kwanza hawatumii lugha kali kama ze komedi, pili wanatumia wanawake katika nafasi za wanawake, tatu ni more creative, nne kuna rika tofauti, n.k. hayo ni yangu sijajua yako


haswaaa, uko sawa kabisa.
hawa jamaa wanaelimisha jamii sawia kuliko ze komedi. utaelimishaje jamii mambo ya wanawake wakati wewe ni mwanaume?, nyambaf. ujinga mtupu.
segments nyingine za ze komedi hazina maana hasa ile ya 'kina nshomile' huwa sielewi hasa lengo halisi la ile segment.
futuhi wako juu bana ujumbe unafika sawia.
 
Wadau!

FUTUHI ni mchezo unaofanana na Ze Comedy unaorushwa na Star TV kila Alhamisi saa 3.00 usiku.

Walianza taratibu, lakini naona kadiri siku zinavyokwenda wana-improve sana. Kwa upande mwingine, jamaa zetu wa ze comedy naona kama wanaanza kupungukiwa na mapya. Pengine sio vibaya wangeenda mafichoni kwa muda, ili turudiwe hamu ya kuwaona.
 
Futuhi ndo kitu gani? Sijaelewa kitu hapa!

mkuu futuhi ni kipindi cha vichekesho kinarushwa hewani na Star TV siku ya alhamisi kama jana saa tatu- nne usiku.
ni kipindi cha vichekesho kama kile cha ze komedi, actually kipindi hiki kilipata umaarufu kiasi wakati ule ze komedi walipokua wana mgogoro na EATV, yaani jamaa waliibukia juu ya mgongo wa ze komedi ama kweli kufa kufaana!.


Ze comedy juu juu juuuu zaidi.

wako juu lakini pumba nyingi!, mi wananiboa hasa pale wanapoigiza sehemu ya wanawake utakuta dume zima limevaa kike(sawa ni maigizo lakini kimaadili watoto wetu wataharibika bana)
icon10.gif
 
wadau mmenena. hawa jamaa wanahitaji kupumzika kwanza ndipo waibuke tena. tena wafanye vichekesho vyao kiutu uzima zaidi. channel ten walikuwepo wanajiita vimbwanga time kila jmosi saa 2 usiku lakini nao naona chali kama mende
 
Komedi orijino wako juu zaidi. Ile ndo style yao!

Komedy wamefulia haswa!

FUTUHI wako juu sana, vichekeksho vyao vinafurahisha lakini pia vinaibua matatizo halisi katika jamii! Mfano jana ile seen ya Mama kujifungua aliye bebwa na ambulance ya mkokoteni! Hiyo ilikuwa nzuri sana lakini ilibebea ujumbe mzito kwa utawala kwamba hali si shwari, maisha bora ni ndoto! Achilia mbali ile seen ya wamama wanao penda kujiuza ili hali wapo ndani ya ndoa kwa jili ya tamaa, kibwagizo ilikuwa ni ule mtafaruku, wa uteuzi wa mama kuwa mkuu wa Wilaya na jinsi cheo hicho kilivyo vuruga ndoa yao! Kimsingi haya mambo yapo katika jamii ndoa nyingi zimevurugwa kwa ajili ya vyeo vya namna hiyo ambavyo mama hujikuta kazi yuko kaskazini, baba akibaki kusini!

FUTUHI BABU KUBWA huwezi walinganisha na komedi wavaa sketi na blezia!
 
wadau, hapa nani zaidi? kwa upande wangu nimekuwa nikiwatazama wote ila navutiwa na futuhi kwa mambo kadhaa. kwanza hawatumii lugha kali kama ze komedi, pili wanatumia wanawake katika nafasi za wanawake, tatu ni more creative, nne kuna rika tofauti, n.k. hayo ni yangu sijajua yako

Ze comedy (orijino komedi) wamefulia

Futuhi Juu, Juu, Juu zaidi.
 
Ze commeddy wana vipaji BUT wameharibiwa na sifa. Lugha wanazotumia ni aibu, huwezi angalia ukiwa na watoto wako wadhani wote wanaoangalia ni watu wa maskani/vijiweni.

Futuhi wanajitahidi kuwa creative, kuelimisha na kufikisha ujumbe kwa kutumia lugha nuri BUT hawana vipaji, na kama wanavyo viko chini.

Kinachopaswa kufanyika ni ku-merge makundi mawili, ili futhuhi wawe na wenye vipaji na wajifunze sanaa na ili ze comedy wajifunze ustaarabu.

Nikiangalia futuhi nasinzia, nikiangalia ze comedy (Hasa na familia)nalazimika remote yangu niielekeze kwenye TV maana wakati wowote wanaharibu (Mitusi tupu!)
 
Hata interest ya kuangalia ze komedy haipo tena

Futuhi juuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
 
Non of the shows are that entertaining to be honest. The production level is poor, the scripts are poorly written if there is any at all and the acting is mediocre. Ze komedi think they have more talent then they are actually blessed with and futuhi can try to chose it's setting better. But I have to say compared to each other futuhi is better.
 
Back
Top Bottom