Ninafikiri hapa hatuna haja ya kumwandama mtu, tujali hoja. kama hoja imetolewa na mtu mwenye mapungufu na ikaonekana ina faida kwa taifa, hatuna haja ya kumjadili mtoa hoja, bali hoja hiyo ijibiwe kwanza ndipo tuangalie mapungufu ya mtoa hoja.
kinachoonekana sasa ni kutapatapa kwa viongozi wa ccm na serikali yake. lakini wenye akili tunajua nani ana hoja na nani anatapatapa. mfa maji haishi kushikilia hata majani akidhania ni tawi la mti.
CCM wajibu hoja, wakishajibu, walete hiyo ya slaa na ushahidi wa kutosha mfano wa slaa aliyeanika peupee kila mtu anasoma ili nasi tuangalie huo upande wa pili, vinginevyo hizi ni ngonjera za majukwaani. watawapata wasio na ufahamu wa mambo na mashabiki wa ufisadi.