Zawadi za 50tsh kutoka VODACOM!

CHAI CHUNGU

JF-Expert Member
Feb 20, 2012
7,113
930
Wana JF mimi nafsi nakereka sana na hii zawadi,yes zawadi ni zawadi,but hii ya tsh50 siyo.
Mtu unatuma zaidi ya tsh 800,000 kwa M PESA,mara unapokea sms eti umepewa zawadi ya tsh50 kwa kutuma pesa kwa M PESA,kwanini wasitoe zawadi japo ya sms 10 kuliko hako ka tsh50 kao?
NOTE:vodacom itazameni upya hii zawadi yenu bana.
 
Ni kujaziana inbox tu, inauzi sana pale unapokuwa unawaza mambo yako mara sms inaingia eti umepata 50 tsh.
 
binafsi pia nakereka sana na haka ka zawadi kakizushi. Ni bora wakaacha kabisa. Hata hivyo kwa hivi sasa nimehamia airtel money. Huu uzushi wa vodacom tupa kule. Aaaaghaaarr kero tupu.
 
Kumbe tunakereka wengi,ni bora hata wakiondoe hiko ki 50 kao.
 
binafsi pia nakereka sana na haka ka zawadi kakizushi. Ni bora wakaacha kabisa. Hata hivyo kwa hivi sasa nimehamia airtel money. Huu uzushi wa vodacom tupa kule. Aaaaghaaarr kero tupu.
Mkuu na wewe kumbe umehamia huku,yaani hawa vodacom wanatufanya sisi watoto sana,wanakukata transfer fees ya tsh2,000 alafu wanakupoza kwa tsh50.
This is ABUNUWASI STYLE bana!
 
Bora mmenisemea mi ndo hupatwa na kichefuchefu na hiyo 50! Isiyozingatia muamala wa amount ipi uufanyao!
Nahisi kutapika niionapo 50!
K kibuyu zao!
 
Bora mmenisemea mi ndo hupatwa na kichefuchefu na hiyo 50! Isiyozingatia muamala wa amount ipi uufanyao!
Nahisi kutapika niionapo 50!
K kibuyu zao!
Hahaha ha ha ha!
Nahisi kama nakuona umekunja uso vile.
Ka sh50 ata sms hakatumi.
Yani hawa jamaa wanaongoza kwa "ungese"aise.
 
Kama ni wasikivu watakuwa na jukumu la kuondoa hii kero. Ingawa binafsi ninatumia mitandao mitatu ya simu, sijawahi kutumia huduma ya M-PESA kwa sababu zangu ila kama mambo yenyewe ndo hivyo I WON'T USE THAT SERVICE.
 
Kweli inakera sana!!Bora mandieta umeliona hilo!!wanatumalizia charge za simu tu hawa Vodacom
 
Last edited by a moderator:
duh kumbe tupo wengi, bora wangekuwa wanaangalia amount ulotuma wakatoa walau 5% kama bonus. otherwise ni WIZI MTUPU. Afu siku hizi ukituma pesa nawe unakatwa na mtumiaji naye anakatwa. yan balaa square. . . .
 
Inakera kwa kweli, ni afadhali wakaiondoa kabisaa, haina maana yoyote, ni bora hata waangekua wanatoa sms 15 au 20. Huu ni udhalilishaji , sasa ukiwaona wanavyojisifia kwenye Media, eti kazi ni kwako, ***** mtupu!
 
Mie mpaka leo sioni umuhimu wa hako ka sh50 kao afu suala la 25% sjui ya nyongeza ukiweka salio kwa mpesa mie sielewi jamani maana nkiangalia hako ka nyongeza mmh!!!!
 
duh kumbe tupo wengi, bora wangekuwa wanaangalia amount ulotuma wakatoa walau 5% kama bonus. otherwise ni WIZI MTUPU. Afu siku hizi ukituma pesa nawe unakatwa na mtumiaji naye anakatwa. yan balaa square. . . .
Alafu unapozwa kwa 50 lol
 
Back
Top Bottom