AXIOM APEX VERBOSE
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 10,177
- 16,334
Wakuu,
Jana Vodacom system ili crash mida ya jioni. Kuna transaction nilifanya mida hio. Sasa nikasubiri labda meseji itarudi hakuna meseji iliyorudi mpaka leo muda huu hakuna meseji hakuna maelezo yoyote hakuna chochote nilichoambiwa km mteja kuanzia jana mida ya saa 11 jioni system ilifeli upande wa Mpesa.
Najaribu kupiga simu asubuhi hii namba 100 huduma kwa wateja kupata maelezo ya kina kuhusu ile transaction niliyofanya jana upande wa malipo yaan lipa, hakuna option ya kuongea na mtoa huduma.
Ukiingia kwenye menu baada ya kupiga namba 100 wanakukatisha yaan hufiki kwenye option ya kuongea na mtoa huduma ili uelezee tatizo lako ni nini na wanakusaidiaje hapo wameweka block nadhani.
Kitu nilichoona mimi ambacho Vodacom pamoja na kwamba ni mtandao mkubwa ila kuna shida ndogo ndogo kabisa niseme shida ya kijinga kuendana na kasi ya technology tuliyonayo hivi sasa wanashindwa kufanyia kazi jambo dogo km hilo inakua km bado tunaishi zama za mawe.
Ipo hivi system ya Mpesa ikifeli yaan inafeli kote nothing comes IN nothing goes OUT, system nzima inakufa kwa muda mpaka waiamshe tena upya.
Sasa hii sio nzuri.
Nitatolea mfano wa mitandao mingine mfano mdogo tu Halotel, system ya Halopesa ikifeli mfano kwenye Halopesa yenyewe tuseme labda kutuma pesa system imefeli na vinginevyo ninafikiri hawa jamaa wana backup ya system ya Halopesa au subsystem ambayo inaendelea kufanya kazi km kawaida ambapo mifumo mingine midogo ndani ya Halopesa km kufanya malipo inaendelea kufanya kazi ila mfumo wa kutuma pesa unakua haufanyi kazi yaan system nzima haiendi chini haifeli yote ni kipande tu cha system ndio kinakua kimefeli.
Ila kwa nilichoona kwa Vodacom haipo hivyo mfumo wa Mpesa ukifeli system nzima ya Mpesa inafeli yaan jana mpaka saa 4 usiku kutoka saa 11 jioni ndio system imerudi na sisi tuliofanya malipo hatujarudishiwa meseji zozote mpaka muda huu na kuna mambo mengine inabidi tuyafanye kwa hizo transaction tumefanya. Sasa hawa jamaa mboni wanatufelisha lakini?
Kwanini Vodacom inakua na mambo ya kizama haiendi na kasi ya technology ya sasa. Just imagine mfumo umezima kuanzia saa 11 jioni unakuja kukubari saa 4 usiku hapo ni masaa mangapi yamepotea na hela wameikalia mpaka muda huu hawatumi meseji kueleza chochote hela haijarudi mpaka muda huu sana sana ukipiga 100 ukienda option ya Mpesa unastopishwa hakuna kwenye kwenye upande wa kuongea na mtoa huduma kwanini wanatufanyia hivi lakini?
Jambo jingine ni customer service au niseme customer care. Niseme wazi mimi niliacha kabisa kutumia Vodacom kwa sababu km hizi yaan poor customer service plus poor customer care. Nikahama, sasa hivi karibuni sijui shetani gani kanirubuni nikarudi tena halafu jamaa wameanza kuniudhi tena upya. Inamaana wananihamasisha nihame tena Vodacom au niache kabisa kutumia huduma ya Mpesa.
Vitu viwili Vodacom inabidi wajifunze kutoka kwenye makampuni mengine na wavifanyie kazi. Haya ni mapendekezo yangu mimi nikiwa km mmoja wa wateja wanaotumia Vodacom.
Moja ni mfumo wao wa Mpesa.
Mfumo ukifeli basi usifeli mfumo mzima km utafeli basi iwe inafeli segment tu ya mfumo yaan ni subsystem tu ifeli ila sio mfumo mzima unaenda chini mfumo mzima unafeli hio ni mbaya sana yaan mfumo hautakiwi wote.
Kwa kasi ya Technology ya sasa unapokua na mfumo wa aina hio ni hasara kwa wateja na kampuni pia, tena sio hasara kidogo yaan mfumo ukipigwa shoti tu ukaenda chini ukafeli wote, jua kuna wateja wengi wanaoingia hasara kwa sababu ya kua na mfumo unaotumia technology ya kizamani.
Cha pili ni kuhusu huduma kwa wateja.
Hapa ndio wanapofeli pakubwa huduma nzuri kwa wateja ndio inayokufanya unakua na wateja wengi ukiwa na huduma mbovu wateja lazima wakukimbie tu lazima wakuhame kwa sababu hakuna mteja anaependa kupatiwa huduma mbovu.
Nimechukia sana.