Zawadi ya Jumamosi kwa Mh. Rais

Zawadi ya Jumamosi kwa Mh. Rais

Nilini wewe ulisema jambo zuri lililo tendwa na serikali?
Kwa asiye kufahamu atapoteza mudawake .
Mnafiki sikuzote niwakuogopwa sana
Kwa mfano mtu akisema kuwa 'DC na RC ni zigo la bure kwa mlipa kodi' halafu mwaka mmoja na nusu baadaye akaja kuwa DC, tumuogope?
 
Kumbe mtoa mada nae ndio walewale
Ungeeleza kuwa gharama za kushusha na kupakia mizigo bandari ya Dar ni kubwa hivyo watu wanakwepa wanaenda bandari za Beira na Mombasa hapo ningekuelewa

Lakini eti kusema kuwa "TRA Dar wanakadiria kodi kubwa........... Na ndio maana mizigo hamna" mm!
Sheria ya kodi ni ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Hauwezi kupitia Namanga ukakuta kuna Sheria yake au Mtukula kukawa na sheria yake ya kodi

Tafuta njia nyingine ya kupotosha
 
Kumbe mtoa mada nae ndio walewale
Ungeeleza kuwa gharama za kushusha na kupakia mizigo bandari ya Dar ni kubwa hivyo watu wanakwepa wanaenda bandari za Beira na Mombasa hapo ningekuelewa

Lakini eti kusema kuwa "TRA Dar wanakadiria kodi kubwa........... Na ndio maana mizigo hamna" mm!
Sheria ya kodi ni ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Hauwezi kupitia Namanga ukakuta kuna Sheria yake au Mtukula kukawa na sheria yake ya kodi

Tafuta njia nyingine ya kupotosha

Umewahi kupitisha mzigo through Bandari ya Dar na mzigo huohuo ukaupitisha Mombasa kisha ukaingilia border ya Namanga au Holili? Kama bado muulize aliyefanya hivyo atakueleza kisha utatambua mleta mada anamaanisha nini
 
Nilicheka nilipomsikia anataka kufyatua pesa mpya eti wafanyabiashara wameficha pesa, huyu walio karibu yake ni dhahiri wanampeleka siko, wanamdanganya sana. Ivi Tajiri gani afiche madafu?
 
Namshukuru Magu ameondoa fedha za ufisadi mtaani maana tusiokuwa na uwezo wa kuzipata tulikuwa tunadharirika sana tulionekana km hatuna akili ya kutafuta, lakini sasa azilete basi zile halali. Maana makazini huko fedha za deal hazipo na zile za halali pia hakuna!
 
"Afisa forodha kukadilia kodi unayopaswa kulingana na mzigo au biashara unayotaka kufanya" kama ni kweli hapa lazima paangaliwe kwa umakini mh.magufuli. Tutoe hiyo colonial legacy.
 
Sasa wakipitishia beira alafu wanakuja kuuza wap...!?
Wakiwa wanaingiza toka beira hawatalipa kodi...!?
Mkuu Bandari ya Dar ni njia muhimu mataifa yote ya kusini mwa jangwa la sahara.. Na ndio walipa kodi wakubwa nchini... Mizigo iuzwayo ndani ya nchi ni kidogo kuliko iendayo nje
 
Marcus Cicero "HOW TO RUN A COUNTRY" kwanini tufuate ya Cicero wakati mwalimu ni hali halisi tuliyonayo? tutafute majibu sisi wenyewe kwa akili zetu
Hotuba tu za Mwalimu za kuzuia uvunjifu wa katiba leo wanaziogopa, hivyo labda hiki kitabu watakisoma
 
Vipofu na nyumbu hawawezi kuona hayo. Hapa kinachozungumzwa ni kodi si tozo za bandari. Ikipitia Beira, hiyo container itaingiaje Tanzania? Kama sio transit goods lazima iletwe Tz na kodi iko pale pale
Unafahamu ni kiasi gani mzigo inayongia bandarini na kuuzwa ndani ya nchi na ile inayotoka nje?
 
Rais wa Nchi hii ni mmoja tu. Mungu ndie aliemchagua kwa sababu zake maalum na kwa mwendo maalum atakao tutembeza. Kama Mungu asingependa tusingemjua yeye wala ubini wake katika Taifa ili.. Tumuunge mkono kwa sababu amepewa kazi maalum ya kuongoza Taifa ili.. Fikiria tu kwanini hasingekuwa babu yako au baba yako? Ila kawa Mheshimiwa.? Mungu akutangulie mh Rais utekeleze yale unayoona yanafaa katika Fikra zako.. Hakuna anaejua mbinu za mechi zaidi ya Kocha.
Hivi huwa mnakuwa wapi mnapojibu mada zinazohusu taifa?
 
Kumbe mtoa mada nae ndio walewale
Ungeeleza kuwa gharama za kushusha na kupakia mizigo bandari ya Dar ni kubwa hivyo watu wanakwepa wanaenda bandari za Beira na Mombasa hapo ningekuelewa

Lakini eti kusema kuwa "TRA Dar wanakadiria kodi kubwa........... Na ndio maana mizigo hamna" mm!
Sheria ya kodi ni ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Hauwezi kupitia Namanga ukakuta kuna Sheria yake au Mtukula kukawa na sheria yake ya kodi

Tafuta njia nyingine ya kupotosha
Ndugu kama hufahamu mambo ya ushuru wa forodha na mengineyo juu ya tra, tafadhari omba msaada kuliko kurukia mambo
 
Kwakuwa sijui liujazalo moyo wa Rais wangu Magufuli, huenda anadhamiri ya kweli kulipeleka taifa kwenye dunia ya uchumi tenge, ama huende anapalilia utawala uleule wa miaka 55 nyuma.

Niliposikia mzigo bandarini imepungua na huku nikisikia matangazo ya kuongezeka kwa mapato kwamjibu wa TRA, nilijipa jukumu la kufuatilia binafsi. Nilichobaini ni harufu ya hujuma kwa taifa inayofanywa na TRA,

TRA mpaka leo inatumia sheria za kikoloni za kodi, hasa sheria ya forodha ya Afrika Mashariki, Sheria hiyo inamtaka afisa wa TRA kwa matakwa yake tu kumkadiria kodi mlipa kodi kulingana na aina ya biashara au mzigo alionao...

Baada ya kuingia Utawala huu wa Rais Magufuli na kuanzisha oparesheni ya nguvu ndani ya mamlaka hiyo ambayo ilitajwa kuwa ndipo wizi mkubwa upo, Maafisa hawa nao wakaja na msimamo wao, Leo mfano kontena la futi 40 la marumaru (tiles) ambalo kabla ya oparesheni ya Magufuli pale Bandarini ulikuwa ukilipia milioni 20, leo unatakiwa kulipia milioni 80, Yani hii ni matakwa ya Ofisa TRA tu na unaambiwa kodi kwanza mengne baadae....isome namba.. Kinachotokea ni mfanyabiashara kutopitishia tena mzigo wake katika bandari ya Dar, anakwenda Beira au Mombasa.. Sio kwamba anakwepa kodi, bali anakwepa wizi unaofanywa na TRA kwaajili ya kuufurahisha utawala.. Na mwisho Bandari imebaki nyeupe...

Sasa ukija kwenye mapato ya kila mwezi tunatangaziwa kuwa yameongezeka... Lakini ukihoji yameongezeka ukilinganisha na nini? Watakujibu ukilinganisha na mapato ya mwaka jana mwezi kama huu... Hili ni jibu dhaifu la kiuchumi. Kuna taarifa ama tetesi zisizorasmi kwamba TRA inatoa hesabu dhahania tu. Madeni hewa yanawekwa katika hesabu za mwezi ili kukidhi haja ya makadirio.. Jambo hili laweza kuangusha nchi kiuchumi..

Tatizo kubwa la TRA mpaka leo hakuna bei elekezi ya kodi.. Nchi zote Afrika Mashariki zina bei elekezi ya kodi kwa kila bidhaa au shughuli inayotakiwa kupiwa kodi. Nchi za wenzetu Afrika Mashariki hazitumii sheria ile iliyoridhiwa na mataifa hayo enzi za umoja.. Na mtandao wa kihalifu nchini unatumia mwanya huu unaoruhusu afisa forodha akukadilie bei ya kulipia, sasa kama sehemu ya mkakati wa kumhujumu Rais, wao wanaweka bei mara mia ya ile iliyozoeleka miaka yote ilimradi ushindwe kulipa na uondoke kutumia Bandari hii ya Dar.

Rais wangu Magufuli, unapoteza muda mwingi kuhujumu vyama vya siasa, lakini unaowaamini wanakujumu katika uchumi. Huenda washauri wako wa Uchumi wanakushauri vizuri, lakini wanakosea kidogo kufahamu kuwa uchumi wowote huwa hauendelei kama pesa haipo kwenye mzunguko... Kinyume chake utaaminishwa kwamba Wafanyabiashara wameficha hela..... Hakuna mfanyabishara gani nchini afiche pesa ya Tanzania hii shilingi ya madafu. Kuchapisha noti mpya sio kukomoa ama kunusuru Uchumi wa nchi, bali kwa tangazo lako lile huenda likashusha thamani ya shungi na kupandisha dola ya kimarekani.

Njia sahihi ruhusu pesa iingie kwenye mzunguko, toa hela wape wananchi wako... Sio uwape mkoni bali kopesha makampuni makubwa na taasisi kubwa zenye uajiri mkubwa na zikopeshwe bila masharti (riba)... Pesa hiyo itaingia kwenye mzunguko na itakaa kwa mda mrefu kuliko ukiwapa masikini kwa njia sijui milioni hamsini kila kijiji...hizo ukiwapa leo hata wiki haitaisha zitarudi benki hivyo utakuwa hujanusuru uchumi.

Muhimu zaidi rudisha morali ya watumishi wa umma, wanaishi kwa woga mkubwa.... Hawa wanaweza kukukwamisha safari yako.... Bila hawa safari yako ni yakurudi nyuma sio kwenda mbele...

Zawadi yangu muhimu kwako Rais Magufuli, naomba umsome Marcus Tullius Cicero katika kitabu chake "HOW TO RUN A COUNTRY" anaweka misimamo ya kiutawala/kiuongozi katika uga mpana zaidi....

Kitabu hiki ni zawadi yangu kwako Mh mtukufu sana rais wangu Mh John Pombe Magufuli, kitakuwa na mafaa kwako na taifa litachekelea..

View attachment 392741

TRA wanatumia tariff yaani asilimia ya bei iliyoko kwenye ankara ya bidhaa. Wanakadiria kodi iwapo tu bei iliyoko kwenye ankara iko chini sana na ina mashaka. Kwa hiyo wanatumia bei elekezi kwa bidhaa za aina hiyo kutegemea ilikotengenezwa. Tatizo waagizaji wengi wanadanganya kwenye ankara na siku hizi ni rahisi kupata bei halisi kutoka kwa watengenezaji wa bidhaa. Kupitishia bidhaa bandari kama Mombasa au Beira haisadii kwani mipaka yote ukokotoaji wa kodi hauna tofauti na bandari ya Dar. Kama mwaka jana alilipa kodi kidogo, awamu hii kodi halisi inakusanywa.
 
Unafahamu ni kiasi gani mzigo inayongia bandarini na kuuzwa ndani ya nchi na ile inayotoka nje?
Haijalishi mzigo umeingilia wapi, kodi itakuwa ni ile ile. Tozo za bandari ni habari nyingine. Kama mfanyabiashara ataona hasara kuleta mzigo Tanzania, ataacha kufanya hivyo lakini ufumbuzi sio kupitisha bandari nyingine.
Kwa transit goods ni sawa kupitisha bandari mbadala kama tozo za Dar ni kubwa.
 
Muhimu zaidi rudisha morali ya watumishi wa umma, wanaishi kwa woga mkubwa.... Hawa wanaweza kukukwamisha safari yako.... Bila hawa safari yako ni yakurudi nyuma sio kwenda mbele...
Point....
 
Back
Top Bottom