Mfanyabiashara kwa kawaida matarajio yake ni faida na siyo faida tu bali faida kubwa, Tulikotoka wamejinufaisha sana kwa kulipa kodi kidogo na huku wakitengeneza faiida kubwa, hivyo katika hali ya sasa ambayo pengine washikaji pale TRA wameondolewa na kodi stahiki ni lazima zilipwe itakuwa vigumu kulipokea kirahisi, katika hali ya kawaida lazima malalamiko yawepo, Maamuzi ya kuhama bandari binafsi siyaafiki japo ni hiali ya mfanyabiashara mwenyewe, lakini kungefanyika mazungumzo baina ya wafanyabiashara na serikali kujua tatizo liko wapi kuliko kusukumwa na nguvu ya kuhama bandari na tatizo likibaki palepale, inawezekana madai yana ukweli juu ya ukadiriaji wa kodi lakini yatafahamika iwapo waagizaji (Wafanyabiashara) watakaa meza moja na serikali yao kuangalia suala hilo naamini muafaka utapatikana tu. Kwa asili Bwana Kodi (mtozaji) hapendwi ila anaweza kuwa tatizo pia kulingana na kazi yake kuifanya kibabe kuliko ueledi'
Kwa mwananchi wa kawaida ambae amepata vijisenti na kutaka kujikwamua kwa kununua Gari (Usafiri) Makadirio yale ya TRA CALCULATOR yatazamwe kulingana na Bei ya Soko ya magari, Bei ya kununua Gari (used) ni ndogo kulinganisha na Kodi inayotozwa, Dawati la malalamiko lifanyie kazi malalamiko na sio kuyatupa kapuni, Serikali inapoteza fedha nyingi hapa, Ukiagiza Gari kodi itaendelea kupatikana kwenye Mafuta,Matairi, vipuri, vilainishi hata barabara kutokana na hilo Gari moja, Ubunifu wa mapato lazima uongezeke na mapato yaongezeke Serikali ipatie Wananchi huduma na yenyewe ikijiendesha.
Tanesco ilipata washauri wataalamu sasa imepunguza gharama zake za kuunganisha kwa wateja matokeo yake japo hayataonekana sasa lakini tunakoelekea litakuwa shirika imara na lenye Mafanikio makubwa kwa kuwa na wateja wengi nchini wenye kutumia Nishati hiyo na Shirika kujiingizia Mapato ya kutosha.
Ushauri mwingine TRA tokeni ofisini mkafanye kazi kwenye mitaa yenye Maduka makubwa kwa namna mnayojua, Bado kuna ukwepaji mkubwa wa kodi, pale Arusha Jirani na Stendi ya Mabasi kuna Maduka ya vipuri vya Magari, nilishuhudia Mteja akinunua DRIVE BELT TATU za Landcruiser VX kama ifutavyo: Altonetor Belt Tsh 118,000/= AC Belt Tsh 56,000/=Jumla Tsh 174,000/=+VAT 31320/= 205,320/= akaomba kupunguziwa bei, akaambiwa Bei bila vat itapungua kwa sharti hakuna risiti na kifungashio cha vipuri hivyo uache hapa, kwa kuona unafuu akalipa Tsh 170,000/= akaondoka zake..! Sasa wako wangapi wa namna hiyo?