Yericko Nyerere
Platinum Member
- Dec 22, 2010
- 17,027
- 20,519
Kwakuwa sijui liujazalo moyo wa Rais wangu Magufuli, huenda anadhamiri ya kweli kulipeleka taifa kwenye dunia ya uchumi tenge, ama huende anapalilia utawala uleule wa miaka 55 nyuma.
Niliposikia mzigo bandarini imepungua na huku nikisikia matangazo ya kuongezeka kwa mapato kwamjibu wa TRA, nilijipa jukumu la kufuatilia binafsi. Nilichobaini ni harufu ya hujuma kwa taifa inayofanywa na TRA,
TRA mpaka leo inatumia sheria za kikoloni za kodi, hasa sheria ya forodha ya Afrika Mashariki, Sheria hiyo inamtaka afisa wa TRA kwa matakwa yake tu kumkadiria kodi mlipa kodi kulingana na aina ya biashara au mzigo alionao...
Baada ya kuingia Utawala huu wa Rais Magufuli na kuanzisha oparesheni ya nguvu ndani ya mamlaka hiyo ambayo ilitajwa kuwa ndipo wizi mkubwa upo, Maafisa hawa nao wakaja na msimamo wao, Leo mfano kontena la futi 40 la marumaru (tiles) ambalo kabla ya oparesheni ya Magufuli pale Bandarini ulikuwa ukilipia milioni 20, leo unatakiwa kulipia milioni 80, Yani hii ni matakwa ya Ofisa TRA tu na unaambiwa kodi kwanza mengne baadae....isome namba.. Kinachotokea ni mfanyabiashara kutopitishia tena mzigo wake katika bandari ya Dar, anakwenda Beira au Mombasa.. Sio kwamba anakwepa kodi, bali anakwepa wizi unaofanywa na TRA kwaajili ya kuufurahisha utawala.. Na mwisho Bandari imebaki nyeupe...
Sasa ukija kwenye mapato ya kila mwezi tunatangaziwa kuwa yameongezeka... Lakini ukihoji yameongezeka ukilinganisha na nini? Watakujibu ukilinganisha na mapato ya mwaka jana mwezi kama huu... Hili ni jibu dhaifu la kiuchumi. Kuna taarifa ama tetesi zisizorasmi kwamba TRA inatoa hesabu dhahania tu. Madeni hewa yanawekwa katika hesabu za mwezi ili kukidhi haja ya makadirio.. Jambo hili laweza kuangusha nchi kiuchumi..
Tatizo kubwa la TRA mpaka leo hakuna bei elekezi ya kodi.. Nchi zote Afrika Mashariki zina bei elekezi ya kodi kwa kila bidhaa au shughuli inayotakiwa kupiwa kodi. Nchi za wenzetu Afrika Mashariki hazitumii sheria ile iliyoridhiwa na mataifa hayo enzi za umoja.. Na mtandao wa kihalifu nchini unatumia mwanya huu unaoruhusu afisa forodha akukadilie bei ya kulipia, sasa kama sehemu ya mkakati wa kumhujumu Rais, wao wanaweka bei mara mia ya ile iliyozoeleka miaka yote ilimradi ushindwe kulipa na uondoke kutumia Bandari hii ya Dar.
Rais wangu Magufuli, unapoteza muda mwingi kuhujumu vyama vya siasa, lakini unaowaamini wanakujumu katika uchumi. Huenda washauri wako wa Uchumi wanakushauri vizuri, lakini wanakosea kidogo kufahamu kuwa uchumi wowote huwa hauendelei kama pesa haipo kwenye mzunguko... Kinyume chake utaaminishwa kwamba Wafanyabiashara wameficha hela..... Hakuna mfanyabishara gani nchini afiche pesa ya Tanzania hii shilingi ya madafu. Kuchapisha noti mpya sio kukomoa ama kunusuru Uchumi wa nchi, bali kwa tangazo lako lile huenda likashusha thamani ya shungi na kupandisha dola ya kimarekani.
Njia sahihi ruhusu pesa iingie kwenye mzunguko, toa hela wape wananchi wako... Sio uwape mkoni bali kopesha makampuni makubwa na taasisi kubwa zenye uajiri mkubwa na zikopeshwe bila masharti (riba)... Pesa hiyo itaingia kwenye mzunguko na itakaa kwa mda mrefu kuliko ukiwapa masikini kwa njia sijui milioni hamsini kila kijiji...hizo ukiwapa leo hata wiki haitaisha zitarudi benki hivyo utakuwa hujanusuru uchumi.
Muhimu zaidi rudisha morali ya watumishi wa umma, wanaishi kwa woga mkubwa.... Hawa wanaweza kukukwamisha safari yako.... Bila hawa safari yako ni yakurudi nyuma sio kwenda mbele...
Zawadi yangu muhimu kwako Rais Magufuli, naomba umsome Marcus Tullius Cicero katika kitabu chake "HOW TO RUN A COUNTRY" anaweka misimamo ya kiutawala/kiuongozi katika uga mpana zaidi....
Kitabu hiki ni zawadi yangu kwako Mh mtukufu sana rais wangu Mh John Pombe Magufuli, kitakuwa na mafaa kwako na taifa litachekelea..