Zawadi ya Jumamosi kwa Mh. Rais

Zawadi ya Jumamosi kwa Mh. Rais

Sasa wakipitishia beira alafu wanakuja kuuza wap...!?
Wakiwa wanaingiza toka beira hawatalipa kodi...!?
 
Yerico amesema kile ninacho kujua kitambo!

Licha ya Bandari(Staff)kufanya kazi kwa kutukomoa baada ya wao kuondoa bei elekezi kwa maslahi yao, hata watu wa Shipping waliopo pale sio Taaluma yao (ukitaka kuamini kawaombe vyeti)

Hilo la sheria za kikoloni yupo sahihi kwa 100% kwani hata JWT na wajumbe wa Serikali (Kamati ndogo ya kiufundi) baada ya kwenda Nchi majirani kutafuta Taarifa za kutusaidia tumudu soko la ushindani walileta Ripoti kama alivyosema Yerico (Ukitaka kesho njoo nikupe uisome)wenzetu walishatoka huko ila sie tumeng'ang'ania na sijui kwa maslahi ya Nani.
Hivyo wanao pitisha Beira au Mombasa hawana kosa.

Kulinganisha mapato ya mwaka Jana Na mwaka huu, huo ni idhaifu wa kulazimisha ushindi kwa mifano mfu na baya zaidi kujumlisha na madeni.
Madeni ni pato la zamani huwezi kuyaweka kwenye FAIDA ya leo.

Hilo la maafisa wa forodha nilisha lisema kuwa tatizo la Mkuu anawaamini sana wataalamu wake hata kama wanampotosha.
Hajawahi kufikiria kutengeneza benchi la kukutana na Wafanyabiashara wa kati japo Mara moja kwa miezi sita ili kuwasikiliza wanasemaje kuhusu muundo wa kodi Nchini na hata kujua wanakutana na changamoto zipi.
Hawa ni Daraja Kuu kuliko yote kwa pato la Serikali.

Familia ikiwa na njaa huwa hakuna maelewano, kila mtu anawaza njia itakayo mfanya ashibe.
Sasa hivi kila mtu analia, kila kona ni machozi tu, hata walikuwa upande wake wameanza kuhama na tayari wanamshutumu.
Fanya yote lakini Mwananchi ashibe vinginevyo utavunja ngome inayokuunga mkono.

Watumishi wa umma ndio balaa, kila mtu anatamani kuacha kazi.
Hawana Amani mioyoni hata kidogo ndio maana inafikia mahali wanaona Bora wamfurahishe hata kama matokeo hayatalipa.
Ni kweli anatakiwa arudishe Morali wa kazi kwa watumishi wa Umma badala kuwatolea maneno ya vitisho.
Vinginevyo wenye Taaluma zao wataacha ili wajiajiri kwa kutafuta Amani za moyo.

Hilo la zawadi ya kitabu nalikubali sana.
Yeyote apendaey kujifunza hufanikiwa.
Hivyo kumsoma Marcus Cicero kwenye "HOW TO RUN A COUNTRY" ni Jambo la kukuza uelewa kiutawala/Kiongozi na sio kashfa Bali ni UPENDO wa kweli.

Nimejaribu kufafanua kwa ufahamu wangu mdogo

Marcus Cicero "HOW TO RUN A COUNTRY" kwanini tufuate ya Cicero wakati mwalimu ni hali halisi tuliyonayo? tutafute majibu sisi wenyewe kwa akili zetu
 
Sasa wakipitishia beira alafu wanakuja kuuza wap...!?
Wakiwa wanaingiza toka beira hawatalipa kodi...!?
Vipofu na nyumbu hawawezi kuona hayo. Hapa kinachozungumzwa ni kodi si tozo za bandari. Ikipitia Beira, hiyo container itaingiaje Tanzania? Kama sio transit goods lazima iletwe Tz na kodi iko pale pale
 
Rais wa Nchi hii ni mmoja tu. Mungu ndie aliemchagua kwa sababu zake maalum na kwa mwendo maalum atakao tutembeza. Kama Mungu asingependa tusingemjua yeye wala ubini wake katika Taifa ili.. Tumuunge mkono kwa sababu amepewa kazi maalum ya kuongoza Taifa ili.. Fikiria tu kwanini hasingekuwa babu yako au baba yako? Ila kawa Mheshimiwa.? Mungu akutangulie mh Rais utekeleze yale unayoona yanafaa katika Fikra zako.. Hakuna anaejua mbinu za mechi zaidi ya Kocha.
 
Yericko kama Lema vile! Cku hizi mmekuwa wapole, kumbe mmnaakili mlikuwa mnajitoa ufahamu tu kipindi cha JK

Huu ndio mchango wako kwenye mada muhimu kama hii?
 
Nilini wewe ulisema jambo zuri lililo tendwa na serikali?
Kwa asiye kufahamu atapoteza mudawake .
Mnafiki sikuzote niwakuogopwa sana
Jadili content ya post mkuu and not the person...
 
Tatizo kubwa la TRA mpaka leo hakuna bei elekezi ya kodi.. Nchi zote Afrika Mashariki zina bei elekezi ya kodi kwa kila bidhaa au shughuli inayotakiwa kupiwa kodi. Nchi za wenzetu Afrika Mashariki hazitumii sheria ile iliyoridhiwa na mataifa hayo enzi za umoja.. Na mtandao wa kihalifu nchini unatumia mwanya huu unaoruhusu afisa forodha akukadilie bei ya kulipia, sasa kama sehemu ya mkakati wa kumhujumu Rais, wao wanaweka bei mara mia ya ile iliyozoeleka miaka yote ilimradi ushindwe kulipa na uondoke kutumia Bandari hii ya Dar.

Ni bei au kiwango elekezi naomba wataalam wa kiswahili wanisaidie navyo jua bei huwa kwenye bidhaa zinazouzwa madukani au kwenye soko utasikia 'unauza bei gani', kodi bei gani?Naweza nje ya mada.
Hao ndo Chadema, mapovu yote hayo ni kwa sababu Bosi wao NHC wamemtupia virago sasa wanatapatapa. Mbowe alipe tu kodi hakuna namna
 
Rais wa Nchi hii ni mmoja tu. Mungu ndie aliemchagua kwa sababu zake maalum na kwa mwendo maalum atakao tutembeza. Kama Mungu asingependa tusingemjua yeye wala ubini wake katika Taifa ili.. Tumuunge mkono kwa sababu amepewa kazi maalum ya kuongoza Taifa ili.. Fikiria tu kwanini hasingekuwa babu yako au baba yako? Ila kawa Mheshimiwa.? Mungu akutangulie mh Rais utekeleze yale unayoona yanafaa katika Fikra zako.. Hakuna anaejua mbinu za mechi zaidi ya Kocha.
Sana tu, wengine hao ni Mapepo na yafaa tuyakemee kwa nguvu zote ili kumkinda rais wetu
 
Sijaona hoja yako sana sana ulitaka tu kulalamika kuwa rais ananyanyasa vyama vya siasa. Bora tu kwanza hivi vyama vimekuwa vichaka vya watu kujificha. Leo Mbowe anadaiwa bil.1 kwa miaka 20 kwa sababu tu alikuwa anaogopwa kuwa ni Mwenyekiti wa Chama. Tumuache rais afanye kazi, tutamhukumu mbele kwa mbele.
 
Eti TRA nao wanasema wanatukomoa sisi wafanyabiashara na wajasiliamali kumbe wanamkomoa boss wao..hao anaowaamini sijui maprofesa na madokta hakuna cha maana wanachomshauri kuukomboa uchumi wa TZ na kama unasema unaogopa kumshauri boss wako eti kisa atakutengua ujue wewe ni coward na huitaki mema nchi yako na ndugu zako maana unaona taifa linakoelekea siko na umechamaza ukiulizwa unajibu "mi naona mkuu anachosema yupo sahihi"
Mtalia sana safari hii Msukuma ndo ameamua kubana.
 
Kwakuwa sijui liujazalo moyo wa Rais wangu Magufuli, huenda anadhamiri ya kweli kulipeleka taifa kwenye dunia ya uchumi tenge, ama huende anapalilia utawala uleule wa miaka 55 nyuma.

Niliposikia mzigo bandarini imepungua na huku nikisikia matangazo ya kuongezeka kwa mapato kwamjibu wa TRA, nilijipa jukumu la kufuatilia binafsi. Nilichobaini ni harufu ya hujuma kwa taifa inayofanywa na TRA,

TRA mpaka leo inatumia sheria za kikoloni za kodi, hasa sheria ya forodha ya Afrika Mashariki, Sheria hiyo inamtaka afisa wa TRA kwa matakwa yake tu kumkadiria kodi mlipa kodi kulingana na aina ya biashara au mzigo alionao...

Baada ya kuingia Utawala huu wa Rais Magufuli na kuanzisha oparesheni ya nguvu ndani ya mamlaka hiyo ambayo ilitajwa kuwa ndipo wizi mkubwa upo, Maafisa hawa nao wakaja na msimamo wao, Leo mfano kontena la futi 40 la marumaru (tiles) ambalo kabla ya oparesheni ya Magufuli pale Bandarini ulikuwa ukilipia milioni 20, leo unatakiwa kulipia milioni 80, Yani hii ni matakwa ya Ofisa TRA tu na unaambiwa kodi kwanza mengne baadae....isome namba.. Kinachotokea ni mfanyabiashara kutopitishia tena mzigo wake katika bandari ya Dar, anakwenda Beira au Mombasa.. Sio kwamba anakwepa kodi, bali anakwepa wizi unaofanywa na TRA kwaajili ya kuufurahisha utawala.. Na mwisho Bandari imebaki nyeupe...

Sasa ukija kwenye mapato ya kila mwezi tunatangaziwa kuwa yameongezeka... Lakini ukihoji yameongezeka ukilinganisha na nini? Watakujibu ukilinganisha na mapato ya mwaka jana mwezi kama huu... Hili ni jibu dhaifu la kiuchumi. Kuna taarifa ama tetesi zisizorasmi kwamba TRA inatoa hesabu dhahania tu. Madeni hewa yanawekwa katika hesabu za mwezi ili kukidhi haja ya makadirio.. Jambo hili laweza kuangusha nchi kiuchumi..

Tatizo kubwa la TRA mpaka leo hakuna bei elekezi ya kodi.. Nchi zote Afrika Mashariki zina bei elekezi ya kodi kwa kila bidhaa au shughuli inayotakiwa kupiwa kodi. Nchi za wenzetu Afrika Mashariki hazitumii sheria ile iliyoridhiwa na mataifa hayo enzi za umoja.. Na mtandao wa kihalifu nchini unatumia mwanya huu unaoruhusu afisa forodha akukadilie bei ya kulipia, sasa kama sehemu ya mkakati wa kumhujumu Rais, wao wanaweka bei mara mia ya ile iliyozoeleka miaka yote ilimradi ushindwe kulipa na uondoke kutumia Bandari hii ya Dar.

Rais wangu Magufuli, unapoteza muda mwingi kuhujumu vyama vya siasa, lakini unaowaamini wanakujumu katika uchumi. Huenda washauri wako wa Uchumi wanakushauri vizuri, lakini wanakosea kidogo kufahamu kuwa uchumi wowote huwa hauendelei kama pesa haipo kwenye mzunguko... Kinyume chake utaaminishwa kwamba Wafanyabiashara wameficha hela..... Hakuna mfanyabishara gani nchini afiche pesa ya Tanzania hii shilingi ya madafu. Kuchapisha noti mpya sio kukomoa ama kunusuru Uchumi wa nchi, bali kwa tangazo lako lile huenda likashusha thamani ya shungi na kupandisha dola ya kimarekani.

Njia sahihi ruhusu pesa iingie kwenye mzunguko, toa hela wape wananchi wako... Sio uwape mkoni bali kopesha makampuni makubwa na taasisi kubwa zenye uajiri mkubwa na zikopeshwe bila masharti (riba)... Pesa hiyo itaingia kwenye mzunguko na itakaa kwa mda mrefu kuliko ukiwapa masikini kwa njia sijui milioni hamsini kila kijiji...hizo ukiwapa leo hata wiki haitaisha zitarudi benki hivyo utakuwa hujanusuru uchumi.

Muhimu zaidi rudisha morali ya watumishi wa umma, wanaishi kwa woga mkubwa.... Hawa wanaweza kukukwamisha safari yako.... Bila hawa safari yako ni yakurudi nyuma sio kwenda mbele...

Zawadi yangu muhimu kwako Rais Magufuli, naomba umsome Marcus Tullius Cicero katika kitabu chake "HOW TO RUN A COUNTRY" anaweka misimamo ya kiutawala/kiuongozi katika uga mpana zaidi....

Kitabu hiki ni zawadi yangu kwako Mh mtukufu sana rais wangu Mh John Pombe Magufuli, kitakuwa na mafaa kwako na taifa litachekelea..

View attachment 392741
nakuunga mkoni kaka Yericko.... sema utaeleweka kweli kwa haya watu?
 
Magufuli yuko kwenye 'self destruction mode'
sijui kama unaweza kumshauri akasikia

dunia nzima serikali ikibana sana matumizi uchumi unayumba.....

Mfano mashirika ya umma now hayaruhusiwi kufanya mikutano kwenye mahoteli
sekta ya hoteli yoote imeyumba sababu hii

sasa mshauri abadili hili uone kama atakuelewa
 
Back
Top Bottom