Zawadi ya Jumamosi kwa Mh. Rais

Zawadi ya Jumamosi kwa Mh. Rais

Hii serikali ni serikali ya mabulicheka utasikia waziri yupo wizarani kama Kingwangwala anasema eti nasikia kuna tatizo la ukosefu wa chanjo nataka waniambie mara moja waganga wakuu kwa nini chanjo zinapotea ha haaaaaaaaaaaaaaaa mwaka wa vioja wewe ndio upo na katibu mkuu hivi hamjuwi stock yenu ya dawa nchini maskiniii wewe sasa Magufuli anasingizia analaani analalamika utafikiri sio mwenye nchi maajabu hana jibu amepotea kabisa
 
Hili la tra lina ukweli fulani.
Binafsi nilikua nataka ufafanuzi wa kodi fulani na rates zake...hawa jamaa wamegoma kutoa kiwango
Wanasema utatozwa ukiwa tayari.
Nikawambia nataka kujua ili kupanga bajeti vizuru...Tra wamegoma kabisa.
Hivyo kuna ubabaishaji mkubwa sana kwenye tozo na rates zitumikazo. Hawako wazi ni wizi mtupu na kukomoana.
Sababu ya hivo sijui ni kuajiri vilazaa au ndo amri.
Tuna kazi lkn kama trend itakua hivi ...tutegemee economic crush muda sio mrefu....
 
Na mizigo ya Tanzania inapita Mombasa, je kama inapita Namanga kuja Tanzania, au Tunduma je kodi hailipiwi hizo kontena

Kuna kitu ambacho hukijui! Ukipitisha mzingo bandarini na kuvusha mzingo ulioshushwa labla bandari ya Mombasa bei ya kuvushia mpakani ni tofauti na unayo tozwa pale bandarini!

Tena wakifanya hivyo serikali itapoteza hela nyingi sana!

Rais akae meza meja na mzee Prf Lipumba awe mshauri wake kwenye maswala ya kiuchumi siasa aweke pembeni!
 
Mkuu umegusa maeneo muhimu. Kwa nchi ilipo sasa, hata mbinu alizotumia Franklin Delano Roosevelt kukomboa uchumi wa America kupitia New Deal zingetufaa pia. Serikali ikopeshe makampuni madogo na kati kupitia bank, lakini kwenye suala la riba serikali ichukue riba ndogo kwa muda mrefu.
 
Kwakuwa sijui liujazalo moyo wa Rais wangu Magufuli, huenda anadhamiri ya kweli kulipeleka taifa kwenye dunia ya uchumi tenge, ama huende anapalilia utawala uleule wa miaka 55 nyuma.

Niliposikia mzigo bandarini imepungua na huku nikisikia matangazo ya kuongezeka kwa mapato kwamjibu wa TRA, nilijipa jukumu la kufuatilia binafsi. Nilichobaini ni harufu ya hujuma kwa taifa inayofanywa na TRA,

TRA mpaka leo inatumia sheria za kikoloni za kodi, hasa sheria ya forodha ya Afrika Mashariki, Sheria hiyo inamtaka afisa wa TRA kwa matakwa yake tu kumkadiria kodi mlipa kodi kulingana na aina ya biashara au mzigo alionao...

Baada ya kuingia Utawala huu wa Rais Magufuli na kuanzisha oparesheni ya nguvu ndani ya mamlaka hiyo ambayo ilitajwa kuwa ndipo wizi mkubwa upo, Maafisa hawa nao wakaja na msimamo wao, Leo mfano kontena la futi 40 la marumaru (tiles) ambalo kabla ya oparesheni ya Magufuli pale Bandarini ulikuwa ukilipia milioni 20, leo unatakiwa kulipia milioni 80, Yani hii ni matakwa ya Ofisa TRA tu na unaambiwa kodi kwanza mengne baadae....isome namba.. Kinachotokea ni mfanyabiashara kutopitishia tena mzigo wake katika bandari ya Dar, anakwenda Beira au Mombasa.. Sio kwamba anakwepa kodi, bali anakwepa wizi unaofanywa na TRA kwaajili ya kuufurahisha utawala.. Na mwisho Bandari imebaki nyeupe...

Sasa ukija kwenye mapato ya kila mwezi tunatangaziwa kuwa yameongezeka... Lakini ukihoji yameongezeka ukilinganisha na nini? Watakujibu ukilinganisha na mapato ya mwaka jana mwezi kama huu... Hili ni jibu dhaifu la kiuchumi. Kuna taarifa ama tetesi zisizorasmi kwamba TRA inatoa hesabu dhahania tu. Madeni hewa yanawekwa katika hesabu za mwezi ili kukidhi haja ya makadirio.. Jambo hili laweza kuangusha nchi kiuchumi..

Tatizo kubwa la TRA mpaka leo hakuna bei elekezi ya kodi.. Nchi zote Afrika Mashariki zina bei elekezi ya kodi kwa kila bidhaa au shughuli inayotakiwa kupiwa kodi. Nchi za wenzetu Afrika Mashariki hazitumii sheria ile iliyoridhiwa na mataifa hayo enzi za umoja.. Na mtandao wa kihalifu nchini unatumia mwanya huu unaoruhusu afisa forodha akukadilie bei ya kulipia, sasa kama sehemu ya mkakati wa kumhujumu Rais, wao wanaweka bei mara mia ya ile iliyozoeleka miaka yote ilimradi ushindwe kulipa na uondoke kutumia Bandari hii ya Dar.

Rais wangu Magufuli, unapoteza muda mwingi kuhujumu vyama vya siasa, lakini unaowaamini wanakujumu katika uchumi. Huenda washauri wako wa Uchumi wanakushauri vizuri, lakini wanakosea kidogo kufahamu kuwa uchumi wowote huwa hauendelei kama pesa haipo kwenye mzunguko... Kinyume chake utaaminishwa kwamba Wafanyabiashara wameficha hela..... Hakuna mfanyabishara gani nchini afiche pesa ya Tanzania hii shilingi ya madafu. Kuchapisha noti mpya sio kukomoa ama kunusuru Uchumi wa nchi, bali kwa tangazo lako lile huenda likashusha thamani ya shungi na kupandisha dola ya kimarekani.

Njia sahihi ruhusu pesa iingie kwenye mzunguko, toa hela wape wananchi wako... Sio uwape mkoni bali kopesha makampuni makubwa na taasisi kubwa zenye uajiri mkubwa na zikopeshwe bila masharti (riba)... Pesa hiyo itaingia kwenye mzunguko na itakaa kwa mda mrefu kuliko ukiwapa masikini kwa njia sijui milioni hamsini kila kijiji...hizo ukiwapa leo hata wiki haitaisha zitarudi benki hivyo utakuwa hujanusuru uchumi.

Muhimu zaidi rudisha morali ya watumishi wa umma, wanaishi kwa woga mkubwa.... Hawa wanaweza kukukwamisha safari yako.... Bila hawa safari yako ni yakurudi nyuma sio kwenda mbele...

Zawadi yangu muhimu kwako Rais Magufuli, naomba umsome Marcus Tullius Cicero katika kitabu chake "HOW TO RUN A COUNTRY" anaweka misimamo ya kiutawala/kiuongozi katika uga mpana zaidi....

Kitabu hiki ni zawadi yangu kwako Mh mtukufu sana rais wangu Mh John Pombe Magufuli, kitakuwa na mafaa kwako na taifa litachekelea..

View attachment 392741
kama kimendikwa kidhungu sijui kama atakisoma, yeye amekariri anadhani uraisi ni kupambana na wapinzani, kumbe uraisi kazi kubwa ni kuinua uchumi
 
Nilini wewe ulisema jambo zuri lililo tendwa na serikali?
Kwa asiye kufahamu atapoteza mudawake .
Mnafiki sikuzote niwakuogopwa sana
Nchi hii haina wanafiki kama ccm. wapinzani walipopiga kelele safari za nje ccm wakasema zina manufaa sana kwa nchi. JPM alipozifuta wakasema ni kweli zimekuwa zikigharimu sana nchi. Wapizani waliposema nchi hii inaliwa sana na serikali ya ccm wakasema uongo kama hujui kusoma hata picha huoni? JPM alipoingia madarakani akadai hii nchi imeliwa sana na serikali iliyokuwapo madarakani wakashangilia tumbuatumbua yake, wanafiki hujisahulisha
 
Mwandishi wa hiko kitabu alikuwa Rais wa nchi gani?
 
Hoja za kujenga na kuimarisha uchumi ni nyingi sana , lakini je wanapokea ushauri ?

Ni vizuri uzi ukanakiliwa kwa Dr Mpango pia .
 
Nchi hii haina wanafiki kama ccm. wapinzani walipopiga kelele safari za nje ccm wakasema zina manufaa sana kwa nchi. JPM alipozifuta wakasema ni kweli zimekuwa zikigharimu sana nchi. Wapizani waliposema nchi hii inaliwa sana na serikali ya ccm wakasema uongo kama hujui kusoma hata picha huoni? JPM alipoingia madarakani akadai hii nchi imeliwa sana na serikali iliyokuwapo madarakani wakashangilia tumbuatumbua yake, wanafiki hujisahulisha
Ilifikia wakati JK alivunja rekodi ya dunia kwa kusafiri , akaitwa Vasco Da Gama
 
Kwakuwa sijui liujazalo moyo wa Rais wangu Magufuli, huenda anadhamiri ya kweli kulipeleka taifa kwenye dunia ya uchumi tenge, ama huende anapalilia utawala uleule wa miaka 55 nyuma.

Niliposikia mzigo bandarini imepungua na huku nikisikia matangazo ya kuongezeka kwa mapato kwamjibu wa TRA, nilijipa jukumu la kufuatilia binafsi. Nilichobaini ni harufu ya hujuma kwa taifa inayofanywa na TRA,

TRA mpaka leo inatumia sheria za kikoloni za kodi, hasa sheria ya forodha ya Afrika Mashariki, Sheria hiyo inamtaka afisa wa TRA kwa matakwa yake tu kumkadiria kodi mlipa kodi kulingana na aina ya biashara au mzigo alionao...

Baada ya kuingia Utawala huu wa Rais Magufuli na kuanzisha oparesheni ya nguvu ndani ya mamlaka hiyo ambayo ilitajwa kuwa ndipo wizi mkubwa upo, Maafisa hawa nao wakaja na msimamo wao, Leo mfano kontena la futi 40 la marumaru (tiles) ambalo kabla ya oparesheni ya Magufuli pale Bandarini ulikuwa ukilipia milioni 20, leo unatakiwa kulipia milioni 80, Yani hii ni matakwa ya Ofisa TRA tu na unaambiwa kodi kwanza mengne baadae....isome namba.. Kinachotokea ni mfanyabiashara kutopitishia tena mzigo wake katika bandari ya Dar, anakwenda Beira au Mombasa.. Sio kwamba anakwepa kodi, bali anakwepa wizi unaofanywa na TRA kwaajili ya kuufurahisha utawala.. Na mwisho Bandari imebaki nyeupe...

Sasa ukija kwenye mapato ya kila mwezi tunatangaziwa kuwa yameongezeka... Lakini ukihoji yameongezeka ukilinganisha na nini? Watakujibu ukilinganisha na mapato ya mwaka jana mwezi kama huu... Hili ni jibu dhaifu la kiuchumi. Kuna taarifa ama tetesi zisizorasmi kwamba TRA inatoa hesabu dhahania tu. Madeni hewa yanawekwa katika hesabu za mwezi ili kukidhi haja ya makadirio.. Jambo hili laweza kuangusha nchi kiuchumi..

Tatizo kubwa la TRA mpaka leo hakuna bei elekezi ya kodi.. Nchi zote Afrika Mashariki zina bei elekezi ya kodi kwa kila bidhaa au shughuli inayotakiwa kupiwa kodi. Nchi za wenzetu Afrika Mashariki hazitumii sheria ile iliyoridhiwa na mataifa hayo enzi za umoja.. Na mtandao wa kihalifu nchini unatumia mwanya huu unaoruhusu afisa forodha akukadilie bei ya kulipia, sasa kama sehemu ya mkakati wa kumhujumu Rais, wao wanaweka bei mara mia ya ile iliyozoeleka miaka yote ilimradi ushindwe kulipa na uondoke kutumia Bandari hii ya Dar.

Rais wangu Magufuli, unapoteza muda mwingi kuhujumu vyama vya siasa, lakini unaowaamini wanakujumu katika uchumi. Huenda washauri wako wa Uchumi wanakushauri vizuri, lakini wanakosea kidogo kufahamu kuwa uchumi wowote huwa hauendelei kama pesa haipo kwenye mzunguko... Kinyume chake utaaminishwa kwamba Wafanyabiashara wameficha hela..... Hakuna mfanyabishara gani nchini afiche pesa ya Tanzania hii shilingi ya madafu. Kuchapisha noti mpya sio kukomoa ama kunusuru Uchumi wa nchi, bali kwa tangazo lako lile huenda likashusha thamani ya shungi na kupandisha dola ya kimarekani.

Njia sahihi ruhusu pesa iingie kwenye mzunguko, toa hela wape wananchi wako... Sio uwape mkoni bali kopesha makampuni makubwa na taasisi kubwa zenye uajiri mkubwa na zikopeshwe bila masharti (riba)... Pesa hiyo itaingia kwenye mzunguko na itakaa kwa mda mrefu kuliko ukiwapa masikini kwa njia sijui milioni hamsini kila kijiji...hizo ukiwapa leo hata wiki haitaisha zitarudi benki hivyo utakuwa hujanusuru uchumi.

Muhimu zaidi rudisha morali ya watumishi wa umma, wanaishi kwa woga mkubwa.... Hawa wanaweza kukukwamisha safari yako.... Bila hawa safari yako ni yakurudi nyuma sio kwenda mbele...

Zawadi yangu muhimu kwako Rais Magufuli, naomba umsome Marcus Tullius Cicero katika kitabu chake "HOW TO RUN A COUNTRY" anaweka misimamo ya kiutawala/kiuongozi katika uga mpana zaidi....

Kitabu hiki ni zawadi yangu kwako Mh mtukufu sana rais wangu Mh John Pombe Magufuli, kitakuwa na mafaa kwako na taifa litachekelea..

View attachment 392741



!
!
Customs tariff nomecluture au harmonised system.
 
Back
Top Bottom