Zao la cocoa Wilaya ya Kyela

Zao la cocoa Wilaya ya Kyela

Matema kuna bonge la Beach umenikumbusha mbali mkuu
Ukienda kipindi hiki utafurahia beach moja ya huyo mwenye Land mark,kaweka sehemu nzuri sana,sehemu yenye kina kinachoanza taratibu kwa umbali mrefu. Mandhali yake utaifurahia,utapenda kuwepo hapo hakika. Muda wote utatamani uogelee. Hakika ni mahala muafaka kusafisha akili. Patulivu
 
Zao hili lina soko kubwa duniani maana wazungu wanakula chocolates sana
Itabidi kiwanda kiwepo cha kutengeneza chochote kabisa hapo
 
Zao hili lina soko kubwa duniani maana wazungu wanakula chocolates sana
Itabidi kiwanda kiwepo cha kutengeneza chochote kabisa hapo
Ni kweli kabisa linahitajika sana duniani,lakini ndio hivyo wakulima wake hawathaminiwi mkuu
 
Hujajua kilichopo nyuma yake rafikiangu,ikiwezekana tembelea hayo maeneo utajionea na kuwasikiliza wanavyolalamika wakulima wa kawaida mpaka wakubwa. Toka hiyo hali ianze mkulima mkubwa akipeleka cocoa kwenye hicho chama kwanza tu ataambiwa mifuko hamna,utasikia hatuna mahala pa kuhifadhi kwa sasa. Achilia mbali ile kukopwa. Na hapo ni mwanzo tu. Kinachofuatia baadae ni chama kujipangia bei,tena itakuwa bei chini ya 2000,ksbb mnunuzi ni mmoja tu,tofauti na ushindani uliokuwepo. Kama unavyojua mnunuzi akiwa mmoja,ni kila kitu kujipangia mwenyewe na ksbb mkulima hajui chochote ataanza kudanganywa soko la dunia limeshuka. pili mpaka sasa wakulima wadogo mpaka sasa kawaulize wanauzaje sasa na kabla ya hapo,kawaulize jinsi walivyokata tamaa

Sasa hivi kuna Stakabadhi ghalani, Hebu tuambie bei ikoje baada ya huu utaratibu?
 
Ni kweli kabisa linahitajika sana duniani,lakini ndio hivyo wakulima wake hawathaminiwi mkuu
Yaani haya mazao korosho, cocoa na tumbaku ni mazoa ambayo yana soko sana duniani na yanahitajika kila wakati.

Tuna utajiri kiasi ambacho hata ardhi yetu tukitaka kulima mazao ya ghali duniani kama vanilla tungeweza ila tatizo ni kubwa sana
Wakulima wanaonewa sana
Tuombe siku moja tupate wa kumsaidia Rais kwa kufanya kweli.
Tatizo wanaoteuliwa hawana maono yoyote au huwa wanahongwa sijui kwa kweli
 
Jibu hoja, bei ikoje tangu utaratibu wa kuuza kupitia stakabadhi ghalani?
Nimekupata mkuu,Wakulima wa cocoa sasa wanalimia meno hasa maeneo ya ntabs,ipinda,ipande na nsanga wanalilia mfumo wa zamani akina MOETL waliwaokoa sana wakulima wa cocoa!
 
Sipo huko mkuu. Ila nilipita huko nilienda kusafisha akili kidogo matema beach,nimekuwepo huko kwa wiki moja ndio nikapata kubadirishana mawazo na wakazi wa huko. Wakati wa kurudi nikawa nasimama karibia vijiji vya njiani,ngyekye,mababu,mabunga na vingine vyenye wakulima wa cocoa,nikawa nabadirishana nao mawazo na kuwasikiliza
Mkuu ile lami imemalizika hadi matema?
 
Wewe mtu ni fisadi wa kutupwa. Hayo makampuni binafsi yamekuwa yanawanyonya wananchi, kilo moja wananunua chini ya sh 2,000 lakini sasa kupitia vyama vyao wanauza kwa zaidi ya 4000. Watu hamna huruma bado mnataka kuwadhulumu kwa sababu mna uwezo wa kugonga keyboard. Kuweni na aibu, kama unataka COCOA kalime mwenyewe lakini sio kunyonya wananchi.
Najua una nia nzuri ila huna ushahidi. Next time pata taarifa kwa wakulima wenyewe ujue cha kutetea. Adios
 
Ile lami imemalizika. Iko vizuri sana mpaka ziwani kabisa. Unaenda tu hata ba gari ndogo

duh..those days..kulikua na 'fumbi'zito..wenyej wa pande zile wengi wao walikia watu wenye hali duni sana sana walikua wakituon tunPitA n school bus wanajaA kama wote..kulikua na vidaraja vibovu bovu kweli....hyo ni miaka ya early 80 mwanzoooni😎
 
Hujajua kilichopo nyuma yake rafikiangu,ikiwezekana tembelea hayo maeneo utajionea na kuwasikiliza wanavyolalamika wakulima wa kawaida mpaka wakubwa. Toka hiyo hali ianze mkulima mkubwa akipeleka cocoa kwenye hicho chama kwanza tu ataambiwa mifuko hamna,utasikia hatuna mahala pa kuhifadhi kwa sasa. Achilia mbali ile kukopwa. Na hapo ni mwanzo tu. Kinachofuatia baadae ni chama kujipangia bei,tena itakuwa bei chini ya 2000,ksbb mnunuzi ni mmoja tu,tofauti na ushindani uliokuwepo. Kama unavyojua mnunuzi akiwa mmoja,ni kila kitu kujipangia mwenyewe na ksbb mkulima hajui chochote ataanza kudanganywa soko la dunia limeshuka. pili mpaka sasa wakulima wadogo mpaka sasa kawaulize wanauzaje sasa na kabla ya hapo,kawaulize jinsi walivyokata tamaa
Nafikiri haujui dhana nzima ya ushirika... ushirika sio mnunuzi na sheria inasema hivyo Ushirika anakusanya mazao ya washirika/wakulima ili wauze pamoja wawe na sauti moja ya nguvu ya soko kuliko kuuza mmojammoja... Hao wanunuzi unaowataka wanaenda kununua kwenye chama cha ushirika baada ya kukusanywa. Hao wanunuzi watashindania bei hapo kituoni na mnada ni wa hadharani atayetoa bei nzuri anapewa mzigo uliomo kwa bei aliyoshinda. Ushirika hawapangi bei ya bidhaa yoyote. ingekuwa hivyo basi korosho wangepanga ushirika, tumbaku , pamba, kahawa... Ila wangekuwa na viwanda vya kuchakata wangechakata na kuuza wenyewe na hapo ndio wangeweza kununua kwa wakulima na sheria pia ipo. Kasome sheria ya ushirika namba 6 ya 2013. Msiwe mnapotosha watu
 
Sasa hivi kuna Stakabadhi ghalani, Hebu tuambie bei ikoje baada ya huu utaratibu?
Mfumo wa Stakabadhi mazao ghalani (warehouse receipt system) wrs.. Ni kwamba haupandishi bei ya zao ila unampa mkulima nafasi ya kuweza kukopesheka wakati wa mavuno ili asiuze kipindi Hicho bei ikiwa chini asubiri bei ikiwa nzuri (other factors remain constant). Mfano tunajua msimu wa mpunga mavuno Gunia shilingi 35,000 mpaka 45,000. Mkulima akiwa na stakabadhi ya mazao yake sema magunia 1,00 anaweza kwenda kwenye taasisi ya kifedha akakopa 1,00x45,000=4,500,000 ili asilanguliwe kwa bei mbovu. Kwa matarajio mauzo mazuri may be watauza gunia la mpunga 80,000x100 = 8,000,000. Hivyo itamsaidia kipindi cha high season akidhi mahitaji yake na pia asipoteze mali yake kwa kulanguliwa. hiyo ni moja kuuza kama ghafi, Lakini pia mkopo huo unampa nafasi mkulima Huyo kuchakata mpunga wake na kuuongezea thamani na kuuza kama mchele hivyo kuwa na bei nzuri zaidi. Huu Mfano pia unaweza kuupeleka ngazi ya kiushirika hapo nimekupa Mfano ngazi ya mkulima mmojammoja. Asante
 
Kwa ujumla wao watu wa kyela walikufanyia uishi maisha ya tabu uishiyo? au mmoja kati yao?. Japo sijui walichokufanyia,lakini pole sana mkuu,ila mojawapo ya watu wakalimu sana Tanzania
WTF? Watu wa kyela ndio wanaolichafua kabila la wanyakyusa kwa 95%.Umalaya,wasengenyaji,kiburi,jeuri,dharau,majivuno..mbali na hayo ni wanaume ni wavivu kutwa kusubiria wake zao wajishughulishe wao wale walale asubuhi waamke kucheza bao.Ukarimu wanao watu wa mwakaleli lkn sio kyela.
 
Duuh...! wewe ulikutana na wanyakyusa wa maeneo gani mkuu? Sifa za wanyakyusa wa kyela 1. KUJIAMINI ”sasa mtu mwingine mgeni kwa hali hiyo yake ya kujiamini unaweza kumwita ana dharau ksbb anaamini kile anachokijua-(nafikiri ulitaka kuwadanganya mahala wakakugomea,ukawaita wana dharau) 2. HAWATAKI KUONEWA-ndio maana wanaitwa wana kiburi,jeuri. 3. HAWATAKI SHIDA-wakipata huwa wanaridhika haraka na kile walichonacho-labda ndio maana unawaita wavivu. Lakini kiuhalisia umesema wanaume hawataki kufanya kazi hiyo nakukatalia kabisa-uzalishaji mali wote wa kaya unahusisha moja kwa moja wanaume. Nenda kipindi hiki mvua zikianza kunyesha hutamkuta mwanaume nyumbani,utawakuta wote wako shambani. Mfano mdogo ni hizi power tiler za kulimia,zile zinatumika nguvu,mwanamke tu hawezi,sasa utasemaje mwanamke ndie anaezalisha? Wanajituma sana kufanya kazi watu wa kyela isipokuwa wanaridhika haraka. 4. WANAPENDA KUSHIRIKIANA,KUKAA PAMOJA-labda ndio umeita wasengenyaji. Kwa sababu kila baada ya kazi ile jioni au wakishavuna,kazi za shamba zikipungua kijijini wana ngoma zao za asili wanakusanyika pamoja. 5. WANAWAKE NI WAZURI WANAJIPENDA,NA WANAUME NI WASAFI WANAJIPENDA-”ndio maana ukawaita malaya. Nikuambie kitu jamaa yangu. Dunia ya sasa ya digtal-mwanamke yoyote akiwa mzuri lazima atatongozwa sana. Kwa vyovyote vile akitongozwa na watu 100 hapo hakosi kuondoka na wa3 hapo katika kipindi fulani,kufuatana na uzaifu wa mwanamke yoyote hawezi kuruka viunzi,vishawishi vya wanaume wote hao 100. Uliza akina weme supet,humis mubet,lalua mikoel n.k,ndivyo ilivyo kwa mwanamke yoyote mzuri. Hata wewe ukioa mwanamke mzuri sana hesabu maumivu. Kwa hiyo ni kokote kule sio kyela tu
 
Hivo basi BIOLAND NA OLAM watafungasha virago make wamejenga mashule huko vyoo maji safi Ambulance duuh poleni wana kyela sema na nyie mumezid unafiki wallah watu wa kyela ni wanafiki kupitiliza
Mmmmh sawa achana na wanafiki angalia pande zingine,kwani wewe umeongeza nini kwa watu wa kyela?Inawezekana ulienda kibabaishaji na kujifanya mjuaji ukidhani wale watu warahisi kivile, unajua maana ya kyela?
 
Nafikiri haujui dhana nzima ya ushirika... ushirika sio mnunuzi na sheria inasema hivyo Ushirika anakusanya mazao ya washirika/wakulima ili wauze pamoja wawe na sauti moja ya nguvu ya soko kuliko kuuza mmojammoja... Hao wanunuzi unaowataka wanaenda kununua kwenye chama cha ushirika baada ya kukusanywa. Hao wanunuzi watashindania bei hapo kituoni na mnada ni wa hadharani atayetoa bei nzuri anapewa mzigo uliomo kwa bei aliyoshinda. Ushirika hawapangi bei ya bidhaa yoyote. ingekuwa hivyo basi korosho wangepanga ushirika, tumbaku , pamba, kahawa... Ila wangekuwa na viwanda vya kuchakata wangechakata na kuuza wenyewe na hapo ndio wangeweza kununua kwa wakulima na sheria pia ipo. Kasome sheria ya ushirika namba 6 ya 2013. Msiwe mnapotosha watu
Hakuna cha kupotosha,nenda zungukia vijijini waulize wakulima mmoja mmoja,hata wale wanunuzi wakubwa wasikilize. 95% hawataki huo mfumo wenu mpya. Sasa zaidi ya hapo utataka nini? Wape wengi wanachokihitaji. Mpaka hivi sasa wale wakulima wadogo wadogo wameshaanza kuumia,zao hilo kijijini tayari wanauza chini ya vile walivyozoea
 
Back
Top Bottom