Hilo ni sharti la kwanza kikatiba, chama chochote kinachoingia madarakani ni lazima kiheshimu ya kulinda Mapinduzi ya 1964. kwa CUF hilo ni kaa la moto wanashindwa kulimeza kwa sababu kuna wahafidhina hawataki kukubaliana na hilo.Hivi siasa za zanzibar zipo kwa ajili ya human development ? Au zipo kwa ajili ya kulinda mapinduzi ya 1964 .?
Msimamo huo wa SMZ ulitolewa kwa nyakati tofauti na Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa pili wa Rais Zanzibar , Mohamed Aboud Mohamed , na waziri wa fedha wa Zanzibar Omary Yusuph Mzee , walipozungumza na Nipashe kuhusu msimamo wa EU , Marekani na washirika wao kusikitishwa na kurudia uchaguzi kabla ya kupatikana muafaka wa uchaguzi halali wa octoba 25 mwaka jana .
" Zanzibar ni nchi huru na itaendelea kuwa huru , tuko tayari kupokea misaada inayozingatia utu na heshima kwa Zanzibar na wananchi wake , kinyume chake tuko tayari kufa njaa " alisisitiza Aboud .
My Take - ukiona panya anaringa mbele ya paka basi ujue karibu yake kuna shimo , je shimo la Zanzibar ni Tanganyika ? na je katika hili Tanganyika itapona ?
Yetu macho .
Usisubiri sana nyepesi nyepesi 8nateta kuwa kuna kamradi ka barabara kwa ufadhili wa USA umesimama ghafla baada ya wahisani hao kunyuti kiaina na mbaya zaidi mbarabara wameshaanza kuukwangua!Tusubiri tuone
Well said Mkuu tutegemee misiba ya masikini hao viongozi wanauwezo wa kwenda kuishi popoteTatizo ni kwamba hadi hiyo njaa imfikie Abood na hao waropokaji wenzake, Zanzibar itakuwa imejaa mizoga isiyokuwa na wazikaji!
halafu huyu anayesema hivi naye ni chotara kama machotara wanaobaguliwa .Kiongozi yoyote duniani wenye sifa ya uongozi angelisema "Hii hali nahofia raia wangu watapata shida" lakini ukianza kumsikia kiongozi anaonge maneno kama "bora tufe njaa " kwa tatizo ambalo linaweza kutatuliwa ujue huyo sio kiongozi.
Watakao kufa njaa ni wazanzibari wanyonge pangu pakavu nitilie mchuzi,hakuna hata kiongozi mmoja wa juu atakae kufa njaa,hii nikusema huyo aliesema mamneno hayo ni mchumia tumbo,anajijali mwenyewe kuliko anaowaongoza...
2001 si 2016 , halafu siasa za kishamba za kutishana hazina nafasi tena , kumbuka kwamba hakuna UMMA uliowahi kushindwa , ni suala la muda tu .Kwani itakuwa mara ya kwanza, 2001 machafuko ya uchaguzi, walitishia Nyau na misaada yao Zanzibar ili survive na hiyo iliendelea wenyewe wakaachia.
....Zanzibar iankuwa na KIBURI cha "kuwaringia" nchi za Ulaya na Amrika wakati Kyuba wanaIMARISHA mahusiano yao na Amrika!..... Ni kama kwenda ambako wenzako wanatoka!Mohamed aboud ni kati ya wazanzibar wawili wenye kiburi cha kishamba sana ! mwingine anaitwa seif idd , wanasahau kwamba ukitaka kuheshimiwa basi ni lazima nawewe uwe na heshima , heshimuni katiba na ni lazima mheshimu vyama vingine .
si ule mrija maarufu unaoitwa Tanganyika upo !....Zanzibar iankuwa na KIBURI cha "kuwaringia" nchi za Ulaya na Amrika wakati Kyuba wanaIMARISHA mahusiano yao na Amrika!..... Ni kama kwenda ambako wenzako wanatoka!
Mwenyezi Mungu akupe maisha marefu mkuu .Erythrocyte,
Hiyo heshima aisemayo kuwa ipo Zanzibar hadhi hiyo haipo.
Huwezi kuwa na uongozi wa sampuli iliyoko sasa madarakani
tena kwa kutumia mabavu nchi ikabaki na heshima yake.
Huwezi kuwa na wahuni wanatembea na silaha za jadi na za
kisasa mabarabarani wakipiga watu na kuvunja stesheni za
radio nchi pamoja na viongozi wake wakabaki na heshima.
Hebu tazama hii picha hapo chini chanzo chake ni gazeti la Mwananchi la
tarehe 22 Machi 2016.
![]()
Hii ni picha ya Mazombie.
Ikiwa msomaji anataka kuwajua zaidi hawa Mazombie na mfano wake
aingie Google atafute ''Ton Ton Macoute.''
Serikali yenye heshima haiwi na kikosi cha wahuni kupiga raia wake:
![]()
Heshima ya wananchi anayozungumza Mohamed Aboud iko
wapi?
Au ndiyo hiyo hapo juu?
Uhuru anaozungumza Mohamed Aboud uko wapi au ndiyo huu
hapo chini?
![]()
Zanzibar ilikuwa na heshima yake lakini hiyo heshima imepotea miaka mingi
sana.
Zanzibar ilishafikwa na shida ya njaa na wala sababu zake hazikuwa hizo
Mohamed Aboud anazozisema.
Hapo sasa! Tuendako huu "mrija" waweza katwa pia....si ule mrija maarufu unaoitwa Tanganyika upo !
Piinda alishasema zanzibar si nchi nyinyi mnaleta hadithi ni nchiMsimamo huo wa SMZ ulitolewa kwa nyakati tofauti na Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa pili wa Rais Zanzibar , Mohamed Aboud Mohamed , na waziri wa fedha wa Zanzibar Omary Yusuph Mzee , walipozungumza na Nipashe kuhusu msimamo wa EU , Marekani na washirika wao kusikitishwa na kurudia uchaguzi kabla ya kupatikana muafaka wa uchaguzi halali wa octoba 25 mwaka jana .
" Zanzibar ni nchi huru na itaendelea kuwa huru , tuko tayari kupokea misaada inayozingatia utu na heshima kwa Zanzibar na wananchi wake , kinyume chake tuko tayari kufa njaa " alisisitiza Aboud .
My Take - ukiona panya anaringa mbele ya paka basi ujue karibu yake kuna shimo , je shimo la Zanzibar ni Tanganyika ? na je katika hili Tanganyika itapona ?
Yetu macho .
Hivi pinda yupo jamani ?Piinda alishasema zanzibar si nchi nyinyi mnaleta hadithi ni nchi
Erythrocyte,Mwenyezi Mungu akupe maisha marefu mkuu .