Msimamo huo wa SMZ ulitolewa kwa nyakati tofauti na Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa pili wa Rais Zanzibar , Mohamed Aboud Mohamed , na waziri wa fedha wa Zanzibar Omary Yusuph Mzee , walipozungumza na Nipashe kuhusu msimamo wa EU , Marekani na washirika wao kusikitishwa na kurudia uchaguzi kabla ya kupatikana muafaka wa uchaguzi halali wa octoba 25 mwaka jana .
" Zanzibar ni nchi huru na itaendelea kuwa huru , tuko tayari kupokea misaada inayozingatia utu na heshima kwa Zanzibar na wananchi wake , kinyume chake tuko tayari kufa njaa " alisisitiza Aboud .
My Take - ukiona panya anaringa mbele ya paka basi ujue karibu yake kuna shimo , je shimo la Zanzibar ni Tanganyika ? na je katika hili Tanganyika itapona ?
Yetu macho .