Zanzibar: Tuliialika Yanga SC baada ya kupata kura nyingi

Labani og

JF-Expert Member
Sep 15, 2020
15,773
24,208
Wizara ya habari utamaduni vijana Sanaa na michezo ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar SMZ imesema katika kusheherekea mwaka mmoja wa uongozi wa Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dkt HUSSEIN ALLI MWINYI walikuwa na mapendekezo ya timu Tatu katika kufanikisha sherehe hizo ambazo ni kutoka bara yaani YANGA, SIMBA NA AZAM na Yanga ilipata kura nyingi zaidi.

Katibu mkuu wizara hiyo Bi FATMA HAMAD RAJAB amesema Leo visiwani humo katika kuwashukuru wadau waliofanikisha sherehe hizo ambazo zilifana.

Tulipeleka timu Tatu 3 kwa wadau ili zipigiwe kura ni timu ipi tuialike kuja kusheherehesha ambazo kutoka bara tulipendekeza YANGA, SIMBA NA AZAM FC baada ya mchakato wa kama wiki hivi timu pekee iliyopata kura nyingi ni YANGA hivyo tulipeleka mwaliko na tukawaambia kabisa viongozi wa YANGA wadau wenu visiwani wanahitaji mje kutoa burudani--Bi FATMA.

Katika kura zaidi ya 5500 zilizopigwa na wadau wa soka hapa visiwani YANGA ilipata kura 4915, Simba ilipata kura 422 na Azam ilipata kura 163 pekee--bi FATMA HAMAD RAJAB.

Hatukuwa na namna zaidi ya kuwasiliana na uongozi wa YANGA ambao nao walitupa ushirikiano mkubwa na kuahidi kuleta kikosi Chao kamili Ili kutoa burudani kwa wapenda soka hapa visiwani na kama mlivyoona wenyewe Yanga waliuwasha hasa hivyo tunawashukuru hawakutuangusha--bi FATMA.

Imani ya wazanzibar kwa timu za bara hasa YANGA ni kubwa mno hivyo kwa kutambua Hilo viongozi wa YANGA nao waliitikia mualiko wetu vizuri na hawakutaka kuleta kikosi B kwani walituambia wachezaji pekee watakaokosekana ni wale tu walioitwa kwenye timu zao za taifa lakini wengine wote watakuja nao na walifanya hivyo sisi kama wizara na ambao tulipewa jukumu la kuratibu Hilo tunatoa shukrani zetu za dhati kwa uongozi wa YANGA na mashabiki kwa ujumla--alimalizia bi FATMA HAMAD RAJAB.

Studio sauti inatosha huko au iongezwe?
 
Mwanasoka yeyote anayejua mpira atajua club kualikwa kwa lengo la kusherehesha ni out of football ethics

Yanga ilikua inakila sababu ya kupita, na hata ingetokea imezidiwa kura ningeamini tu imehujumiwa

Kwasababu watu wameona wachezaji wa yanga wanaumuhimu kwenye hiyo sherehe kwakua waliwaona wakiimba kwenye siku ya mwananchi pale kwa mkapa

Simba haina record hiyo ya kuwa na wachezaji wa namna hiyo, ila yanga CV inawabeba na ndio maana hata ukiangalia wakongo wako vizuri kwenye kukata viuno

Kwa hiyo ifahamike kwamba yanga inaenda kuhusika kama bendi ya burudani kwenye shughuli huku iki represent jina la club ya mpira
 
Aliyetoa hizo taarifa amefanya makosa makubwa sana ya kiufundi.

Hata kama kulikua na upigaji kura na matokeo yakawa hivyo, hakukuwa na umuhimu wowote wa kuja hadharani kuyasema hayo.

Kwa kujua au kutokujua anaharibu mahusiano kati ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (waliokua na hiyo shughuli) na vilabu vingine visivyokua "Yanga".

Sijui kulikua na ulazima gani wa kuyasema hayo, lakini nadhani hajafikiria vizuri sana kuhusu kesho.
 
Yanga imeongoza kwa kura 4900 kati ya kura 5500, ni Nchi gani hiyo yenye wananchi 5500?

Halafu nchi gani hiyo ambayo wananchi wa club hiyo kwenye mitandao ya kijamii followers kwenye page ya timu yao hawazidi 1M?
Punguza povu nyoko wewe, hata research ikifanyika haihusishi raia wote inachukuliwa sample tu ya watu kadhaa wakiwemo wajinga kama wewe na werevu kuwakilisha kundi fulani.
 
Mwanasoka yeyote anayejua mpira atajua club kualikwa kwa lengo la kusherehesha ni out of football ethics

Yanga ilikua inakila sababu ya kupita, na hata ingetokea imezidiwa kura ningeamini tu imehujumiwa

Kwasababu watu wameona wachezaji wa yanga wanaumuhimu kwenye hiyo sherehe kwakua waliwaona wakiimba kwenye siku ya mwananchi pale kwa mkapa

Simba haina record hiyo ya kuwa na wachezaji wa namna hiyo, ila yanga CV inawabeba na ndio maana hata ukiangalia wakongo wako vizuri kwenye kukata viuno

Kwa hiyo ifahamike kwamba yanga inaenda kuhusika kama bendi ya burudani kwenye shughuli huku iki represent jina la club ya mpira
Wakati wa mkwere tuliwaalika Brazil wakaja Bongo na tukapiga nao mechi taifa, unadhani walikuja kwa kuangalia kigezo gani then linganisha na hili la WANANCHI.

Umia kidogo kidogo kama paka mwizi.
 
Punguza povu nyoko wewe, hata research ikifanyika haihusishi raia wote inachukuliwa sample tu ya watu kadhaa wakiwemo wajinga kama wewe na werevu kuwakilisha kundi fulani.
Ona ulivyo mjinga, sasa kama hizo research zinafanyika kimatabaka unakujaje ku generalize kwa kuwahusisha watu wote?

Kwa hiyo mimi nikisema watu wa yanga hamna akili kwasababu research ya manara ilisema mwenye akili ni baba yake na kikwete, nitakua sahihi?
 
Wakati wa mkwere tuliwaalika Brazil wakaja Bongo na tukapiga nao mechi taifa, unadhani walikuja kwa kuangalia kigezo gani then linganisha na hili la WANANCHI.

Umia kidogo kidogo kama paka mwizi.
Mliwaalika brazil kusheheresha shuhuli gani?

Yanga imealikwa kama kikundi cha ngoma kwa ajili ya kusherehesha, hilo la mpira ni kama la ziada tu
 
Back
Top Bottom