Zanzibar ni Non secular state?

Zanzibar ni Non secular state?

Hivi kuna mwezi mtukufu na usio? Siku tukufu na isiyo?ila wakoloni walituweza aisee
Anayehukumu kwa kula mchana,ni mzinzi hatari,anayehukumu walevi ni mwizi halaa,anayehubiri haki amani na upendo ni msengenyaji wa kutupwa. Nini kujivika viatu vya Mungu?Mbona neno liko wazi tu 'usihukumu usije ukahukumiwa'
Mkuu umesahau kipengele kimoja.
Mwizi wa kura wakati wa uchaguzi ndio anaingia bungeni kutunga sheria za kudhibiti wizi. Ndio maana wezi wote wa kura ambao pia ni wezi wa Mali za taifa hawataki kuiona report ya CAG.
Mnamkumbuka Ndugai alivyomcharaza mtu bakora kipindi cha uchaguzi? Ndugai ndio alipita na hatimae kushinda. Na huko Zanzibar.......
 
Sasa haupo Zanzibar ila unatoa ushauri kwa kitu ambacho unaelezwa na watu waliopo au waliwahi kuwepo Zanznibar
Nimeongelea kuheshimu sheria za nchi ya watu au niseme mji wa watu, wakati mimi au wewe tukiwa wageni. Hauwezi kumpeleka mtoto wako shule ya private bila ya kulipia ada, lakini za serikali ni bure. Hii ndio kuheshibu taratibu mkuu

Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Si kweli ndugu.hakuna anaelazimishwa kufunga,wengi hawafungi sababu jambo la kufunga linatokana na imani.
Kinachopiganiwa zanzibar ni kuipata swaumu iliyo sahihi na ili ipatikane funga iliyo sawa ni lazima kukabiliana na yenye kufunguza.nafsi ya mwanadam imeumbwa na matamanio hivyo kula hadharani kutaathiri funga za waliofunga,kutazama Dada zetu wasiojistiri vema maungo yao itaathiri funga.
Kwa mazingira ya Tanganyika hasa dar na miji mingine mikubwa kufunga kwa usahihi ni jambo gumu sana sababu ya mazingira yenye kufunguza kuwepo bila kukemewa kutokana na uwiano wa dini hizi mbili kuwa sawa.

Kufunga si kujizulia kula na kunywa.
Nyie watu ni wagonjwa wa akili! Ujue sijakuelewa... hebu fafanua!
 
Ulilazimishwa ukae Zanzibar, Ule ovyo tu halafu uwachiliwe, huo utakuwa ugonjwa subiri uwepo Sinza, Ubungo.... utakula hadharani, sio Zanzibar.
Kwahiyo watu waende wakale chakula uvunguni kwa kuwa nyie wapumbavu wachache mmefunga?
 
Duh yani kukueleza kote bado unarudia palepale tu!!!

Nimeshaeleza hadi kwamba hata kama serikali isingetangaza bado kuna biashara nyingi tu wenyewe wangefunga bila hata serikali kusema na nikasema hata huku bara kuna biashara nyingi tu za chakula wenyewe wanaacha kuuza mchana wa mwezi wa ramadhani bila kulazimishwa na yeyote,ila wewe umekazania kulazimisha na haoni kuwa hadi serikali imeweza kufanya hivyo(japo sio nchi ya kiislamu) kutokana na jamii yenyewe ilivyo. Kitu ambacho huku bara hakiwezekani kanisa ila huko zanzibar kuna hadi vijana hufikia kupiga watu bakora wanaokula mchana wa mwezi wa ramadhani.

Na chengine serikali haijalazimisha mtu kufunga bali inazuia watu kula hadharani mchana wa mwezi wa ramadhani. Sasa hapa tu hujanielewa na ndiyo maana unataka et nikutajie nchi yenye wakristo wengi yenye kulazimisha waislamu.
Utetezi wako hauna mantiki, unasema kama wasingekataza watu kufunga watu wangefunga wenyewe, sasa ni kwa nini imekataza isiwaache wakajifungia wenyewe?

Na kwa nini umlazimishe mtu kutokula hadharani? Hii ni njia ya kuwalazimisha watu wafunge kwa nguvu, ni njia ya kumfanya mtu afuate Ramadhani hata kama haamini

Ila haishangazi, nchi za Kiislam hazina uhuru wa kidini, nchi nyingi za Kiislam wamepitisha adhabu ya kifo kama mtu atabadili Dini kutoka Uislam kwenda imani nyingine
 
Sema tu.KAZI NGUMU MPE MNYAMWEZI
Wabara ndo waliuzwa kwani walionekana wao ndo wanaweza kufanya kazi nzito na ngumu sna

Hadi kuna kamsemo kapo hadi leo ila nikikitamka hapa nitaambiwa mbaguzi bora niache maana mwenyewe naishi bara ingawa ni mzanzibar fyoko kabisa
 
Utetezi wako hauna mantiki, unasema kama wasingekataza watu kufunga watu wangefunga wenyewe, sasa ni kwa nini imekataza isiwaache wakajifungia wenyewe?
Na kwa nini umlazimishe mtu kutokula hadharani? Hii ni njia ya kuwalazimisha watu wafunge kwa nguvu, ni njia ya kumfanya mtu afuate Ramadhani hata kama haamini
Ila haishangazi, nchi za Kiislam hazina uhuru wa kidini, nchi nyingi za Kiislam wamepitisha adhabu ya kifo kama mtu atabadili Dini kutoka Uislam kwenda imani nyingine
Hilo ndio lilikuwa lengo lako na ndiyo maana hutaki kabisa kunielewa,hoja ni zanzibar ambayo si nchi ya kiislamu ila wewe unaleta habari za nchi za kiislamu ndiyo hatuelewani kabisa. Halafu vitu vyengine ni vya ajabu kama ushasema nchi za kiislamu kwa maana miongozo yake inafuata uislamu na kwa akili ya kawaida tu ya kawaida utategemea kuzungumzia uhuru wa dini zengine hapo? hivi hata kungekuwa na nchi yeynye kuongozwa kwa misingi ya kikristo ndio ungetegemea kuwepo kwa uhuru wa dini zengine? kama hao wanaobadili dini huko huuliwa basi hilo huko ni kosa na ndio sheria ya nchi na inatoa adhabu hiyo kwa hilo kosa na si kwamba wananyima uhuru.
 
Nchi yenue Waislam wengi, ndio muktadha wangu hapa

Nchi zenye waislam wengi kama Zanzibar japo sio nchi ya Kiislam rasm, hakuna uhuru wa kuabudu, ila tunashuhudia Waislam wakienda kwingineko ndio wanaoongoza kwa kupiga makelele kuwa wanabanwa, China ni mfano tosha, Japo Dini zote zimekatazwa, Waislam ndio wanaopiga kelele kuwa wananyimwa uhuru wa kuabudk, utafikiri hata wanaheshimu huo uhuru
 
Kwahiyo watu waende wakale chakula uvunguni kwa kuwa nyie wapumbavu wachache mmefunga?
Wapumbavu sisi au mpumbavu ni wewe. Laana za Mungu zikufikie. Hii nchii sio genge la wahuni Unaweza kufunga, utafunga la huwezi basi hakikisha unataka kubakia Zanzibar usijilie ovyo mbele ya Hadhara za watu, kaa hata Chooni ule,ukiachia uvunguni.
 
Ilibidi vitu vyote. Sheria ,katiba n.k za tanganyika zitumike hadi zanzibar.mtu ukitoka bara kwenda znz unaishi kwa shida utafikiri znz sio tanzania,au vinginevyo watuambie znz ni nchi kamili haipo tanzania.
Kama ni hivyo utakavyo wewe basi na hata ushuru pale bandarini ungetumika wa bara, kwa maana kusingekuwa na ushuru, ukitoka na bidhaa Zanzibar bandarini unapita zako tu, lakini mbona anaetoka na bidhaa Zanzibar analipia ushuru pale, ila hilo hamlioni mnaliona la wao kuzuia watu kula hadharani mwezi wa Ramadhani. Kha! Bara wana sheria zao na Zanzibar pia. Kama msemavyo wenyewe ndani ya Muungano Zanzibar sio nchi, ila nje ya Muungano Zanzibar ni nchi.
 
Nchi yenue Waislam wengi, ndio muktadha wangu hapa
Nchi zenye waislam wengi kama Zanzibar japo sio nchi ya Kiislam rasm, hakuna uhuru wa kuabudu, ila tunashuhudia Waislam wakienda kwingineko ndio wanaoongoza kwa kupiga makelele kuwa wanabanwa, China ni mfano tosha, Japo Dini zote zimekatazwa, Waislam ndio wanaopiga kelele kuwa wananyimwa uhuru wa kuabudk, utafikiri hata wanaheshimu huo uhuru.
Kwahiyo nchi ambazo hazina mapumziko au hazitambua sikukuu za kiislamu kama sikukuu ya Eid ila sikukuu ya Christmax zipo,je nchi hiyo nayo ina uhuru wa kuabudu au haina?
 
Kwahiyo nchi ambazo hazina mapumziko au hazitambua sikukuu za kiislamu kama sikukuu ya Eid ila sikukuu ya Christmax zipo,je nchi hiyo nayo ina uhuru wa kuabudu au haina?
Sikukuu ni kitu cha siku moja au mbili, ikiwa watu wanaosherekea hiyo sikukuu ni wachache wanapewa mapumziko ya kusherekea peke yao ila inakuwa sio sikukuu ya kitaifa zipo nchi zinafanya hivyo, mfano nchi nyingi za Ulaya zinawafanyia hivyo

Hapo ina make sense na ni fair kabisa, hii ni tofauti na kuzuia biashara ya mtu kwa mwezi mzima.!
 
Wapumbavu sisi au mpumbavu ni wewe. Laana za Mungu zikufikie. Hii nchii sio genge la wahuni Unaweza kufunga, utafunga la huwezi basi hakikisha unataka kubakia Zanzibar usijilie ovyo mbele ya Hadhara za watu, kaa hata Chooni ule,ukiachia uvunguni.
Kweli wewe ni Kubwalijalo!
 
Sikukuu ni kitu cha siku moja au mbili, ikiwa watu wanaosherekea hiyo sikukuu ni wachache wanapewa mapumziko ya kusherekea peke yao ila inakuwa sio sikukuu ya kitaifa zipo nchi zinafanya hivyo, mfano nchi nyingi za Ulaya zinawafanyia hivyo
Hapo ina make sense na ni fair kabisa, hii ni tofauti na kuzuia biashara ya mtu kwa mwezi mzima.!
Ila hujajibu nilichokuuliza,hoja si muda wala baadhi ya nchi zinafanyaje bali nimetaka kujua kwa nchi ambayo haina mapumbuziko kwa sikukuu ya eid kwamba hiyo nchi ina uhuru au haina uhuru wa dini?
 
Huyo jamaa kaongea kwa chuki na kutuchonganisha tu

Halafu eti ooh wazanzibar tuna ubaguzi na chuki wakat wao ndo wanaanza kuleta pumba kama hizi
Ndio Wajing.a kutoka upande wa pili walivyo. wenzao wamezaliwi huku na wameishi miaka yote huku ata hawalalamiki. hawa wakuja wana tabu sana.
 
Kwamaelezo yako una maanisha kuwa na sisi huku bara kwakuwa wakristo niwengi nji iongozwe kikristo siyo
Nchi ikishakua na Waislam kwa zaidi ya 70% hiyo lazima itaendeshwa kwa sheria za Kiislam tu, japokuwa zinaweza kuwa hazijaingizwa kwenye katiba rasmi, ila nchi itaendeshwa kiislam

Waislam wakishakuwa wengi zaidi mahali lazima wafanye sheria zao ndio sheria za nchi

Wakienda sehemu ambazo wao ndio wapo wachache, wataanza kudai kutengewa naeneo ya kuswalia,
 
Back
Top Bottom