Zanzibar: Midoli ya kutangazia nguo zisizo na stara yapigwa marufuku kuwekwa nje ya maduka

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,116
Screenshot_20230215-165854_Instagram.jpg

Mkuu wa Wilaya ya Mjini Magharibi Unguja, Rashid Simai Msaraka amepiga marufuku, Wafanyabiashara wa Wilaya hiyo kuweka midoli yenye nguo zisizo za staha nje ya maduka yao.

DC Msaraka ametoa kauli hiyo baada ya kukutana na Mfanyabiashara maeneo ya Kwahani Zanzibar akiwa ameweka midoli hiyo nje ya duka ikiwa imevalishwa nguo ambazo zinadaiwa kupotosha maadili ya Zanzibar hususan kwa Watoto pindi wanapoona midoli hiyo imevishwa nguo hizo

DC Msaraka ameiambia AyoTV kuwa maarufuku hiyo imetokana na Watoto na Vijana kuona vitu visivyo na staha na kupelekea kuvuraga akili za Vijana wa Zanzibar Hatuwakatazi kuwa na midoli hiyo wala hatuwakatazi kufanya biashara hizo ila biashara hizo zifanywe ndani na zisiwekwe nje, Mtu anayetaka kuvaa nguo hizo avae
mwenyewe anajua utaratibu gani wa kuzivaa na wapi azivae"

Chanzo: Millard Ayo


Pia soma mada zinazohusiana
Vitu vingine vilivyowahi kupigwa marufuku Zanzibar
 
Wangewapiga marufuku watalii wakizungu wanaomiminika huko visiwani na vinguo vyao vya kimagharibi kama kweli wanamaanisha sio kupambana na midoli wakati watu halisi wanaopiga pamba tata wakikatiza tu mitaa ya stone town au ndio baniani mbaya....
 
Back
Top Bottom