Zanzibar: Askari Polisi ajidhalilisha, apokea rushwa mbele ya Camera

Zanzibar: Askari Polisi ajidhalilisha, apokea rushwa mbele ya Camera

Mwacheni Mwenzenu, Mna Uhakika alichukua zaidi ya Tsh 5000, Si Mnakumbuka, Mh. Magufuli alishasema Tsh 5000 ya Kupakia Kiatu rangi sio Rushwa?Na hata Kama amechukua Tsh 60,000 Unaweza Ukakuta wako 12, wenzake akaenda Kuwakatia Tsh. 5000 si atakuwa amesevu? Amakwali Hii Ndiyo Tanzania Ninayoitaka, Kwa Spidi Ninayokwenda nayo hii heeee!

kazi ipo
 
Huyu akari kana anakajishamba kake kwa karafuu, ajiandae kuwa Bwaba Shamba daimu
 
You will never come to zanzibar again,thats your fuckin right.no one forced you to board a plane to Zanzibar, you gave that money on your own consent and filmed it. You thought because you are white and you will be treated like a white god.
 
Nimeshasema mara nyingi humu, tatizo letu ni mentality!! Watu inawauma kwa vile nao kila wakipata nafasi wanapiga madeal kama huyo askari. It's part of our lives!!

Haya anayofanya Rais ya kupangua na kupanga kila siku hatafanikiwa kama hatafanyia kazi people's mentality. Kama 80 % ya watanzania wako design hiyo basi ajue kila anapotoa watu na kuweka wapya, 80 % watakuwa kama wale aliowaondoa. Sana sana watashindwa kupiga deal kwa vile wamebanwa na si kwa kuwa ni waadilifu. Vile vile kwa kupanga na kupangua anaweza kuwa anaondoa competent na kuweka incompetent people hivyo kuharibu zaidi huko mbeleni.

Kitu cha kufanya sasa waanze pia kufanya campaign za kuhamasisha civil servants vile vile wajitahidi kuboresha mafao yao. Pia wajaribu kupunguza gap kati ya wafanyakazi wa serikali na mashirika ya umma. Kwa kweli haiingiii akilini dreva wa shirika la umma awe na mshahara kuliko Mkurungezi serikalini au Professor!!
Wataalamu wanaochanganua mchango wa nafsi kwenye udanganyifu (The Human Component of Fraud) wana Kanuni iitwayo The 20-60-20 Rule. Kwa mujibu wa kanuni hiyo, asilimia 20 ya watu kwenye mjumuiko wowote ule hawataiba (kuiba kwa maana pana ya fraud) hata iweje. Asilimia 60 nyengine ni ya walioketi chini ya uzio (fence sitters). Kimsingi ni watu waamnifu, lakini wakipata fursa ya kuiba na hatari ya kubainika ikiwa ndogo, wanaweza kuchupa uzio. Asilimia 20 iliyobakia kimsingi si waaminifu. Daima watakwapua pale fursa itapotokezea. Mara nyingi watajaribu kuiba kila fursa itapotokezea.
Kwa hivyo kimsingi jamii zote ziko hivyo. Ndio maana tumeshuhudia yaliyotokea FIFA na vigogo wake wa karibu Kanda zake zote, Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya China, tuhuma dhidi ya Donald Trump, akina Rais Uli Hoeness wa Bayern Munich aliyetumikia kifungo kwa kukwapua, akina Sofia Loren ambaye pia alishatumikia kifungo kwao Italy, n.k.
Kinachotofautisha sisi na nchi zinazoonekana kuwa hazina rushwa ni jinsi tunavyoshughulika na hii asilimia 60 ya waaminifu (fence sitters). Wenzetu wameweza kuondoa hizi fursa za rushwa na kuongeza hatari ya kubainika kwa kuweka maamuzi nyeti yasiwe ya mtu mmoja au watu wachache, taratibu zinazoruhusu mwajiri wa taasisi inayoshughulika na fedha nyingi kuchungulia akaunti za wafanyakazi inaowashuku, raia kujaza fomu za kulipa kodi (tax return forms), n.k. Baada ya miaka mingi, uaminifu huu wa kulazimisha unakuwa ni mazowea (behavioral), hivyo kubaki na ile asilimia 20 ya mwisho tu ambayo nayo pia itakuwa pungufu kutokana na kupunguka kwa fursa za kukwapua.
Kwa hivyo unaweza kuwa sahihi kwamba ili rushwa iondoke tunapaswa kubadili mitizamo yetu na kuziba tofauti za kimaslahi kwa wafanyakazi. Lakini si sahihi sana kudhani kwamba Watanzania 'tumezoea' rushwa; ni sahihi zaidi kudhani kwamba mazingira yetu yanalea rushwa. Kubadili mtizamo ni sahihi, lakini lazima iwe kwa namna ya kujenga mazingira yatayoondoa fursa za kuiba na kuongeza hatari ya kubainika.
 
Nimejaribu kuitizama hii clip kwa umakini Mkubwa....

Nimegundua Askari wetu hakuomba Rushwa isipikuwa hawa jamaa walidhamilia kumpa pesa na kutegesha mapema ili ionekane Askari anaomba Rushwa....Sijaona sehemu yoyote akisema wampe Hiyo pesa......Askari hana kosa
Hupo sahihi mkuu wamemtega kwa vile ni mzungu watu wanakulupuka tu kumponda Askari.
 
Kwani hii si imeruhusiwa kwajili ya kusafishia viatu
Kwa hisani ya "MNIOMBEE"
 
Nimejaribu kuitizama hii clip kwa umakini Mkubwa....

Nimegundua Askari wetu hakuomba Rushwa isipikuwa hawa jamaa walidhamilia kumpa pesa na kutegesha mapema ili ionekane Askari anaomba Rushwa....Sijaona sehemu yoyote akisema wampe Hiyo pesa......Askari hana kosa


Kama ni hivyo , huyo askari angalizichukua hizo pesa baadaye akawashitaki hao jamaa kwa kujaribu kumpa rushwa ili kukimbia makosa yao.

Lakini kumbe huo ndio mchezo wake wa kawaida , na alipomaliza anaagana nao kama vile hapakufanyika kitu na mwisho anampongeza mzungu kwa kiengereza chake cha maskani , You are educated man, tehtehtehhhhhh
 
ni rushwa.
ila huyu mzungu aache uongo, mara kamuomba dola 40 ( kama 88,000 tsh), akadanganya tena eti baada ya kuongea akampa 60,000 (kama dola 28), wakati inaonekana wazi kabisa kampa 10,000 tsh.
Hata ukimtuhumu mtu basi ongea kitu cha ukweli.
Mi sipendagi ujinga kama huu!
 
ni rushwa.
ila huyu mzungu aache uongo, mara kamuomba dola 40 ( kama 88,000 tsh), akadanganya tena eti baada ya kuongea akampa 60,000 (kama dola 28), wakati inaonekana wazi kabisa kampa 10,000 tsh.
Hata ukimtuhumu mtu basi ongea kitu cha ukweli.
Mi sipendagi ujinga kama huu!
Zile pesa ni zaidi ya elfu kumi aisee angalia vizuri
 
Back
Top Bottom