Zanzibar: Ardhi maeneo 148 yaliwa na Bahari

Zanzibar: Ardhi maeneo 148 yaliwa na Bahari

MAGEUZI KWELI

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2011
Posts
1,947
Reaction score
254
fatma.jpg
Visiwa vya Zanzibar vinashuhudia maeneo yake kuingiliwa na maji ya bahari na kuathiri sehemu za kilimo.
Tayari maeneo 148 yameingiliwa na maji chumvi na hayafai tena kwa kilimo.
Nini hatma yake kwa miaka mingi ijayo?

Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imekiri kuathirika na tabianchi ambayo kwa kiwango fulani visiwa hivyo vibakabiliwa na tishio la mmomonyomko wa radhi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Fatma Abdulhabib Fereji alisema hayo wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Mtambwe (CUF), Salim Abdallah Hamad aliyetaka kujua athari ya mazingira ambayo imeonekana maeneo ya visiwa vya Zanzibar.

Pia, Salim alitaka kujua jinsi wizara ilivyojipanga kupambana na uharibifu huo, ili wananchi waweze kutumia ardhi yao ipasavyo.

Waziri Fereji alisema ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi ikiwamo kuingia maji ya chumvi kwenye mashamba ya wakulima, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, imekuwa ikiwahamasisha na kuwaelimisha wadau maeneo yalioathiriwa kupanda miti kwa wingi.

Alisema wakati mwingine ikibidi kujenga matuta ili kupunguza athari hizo, kuendelea kuyatumia maeneo hayo kwa shughuli za kilimo.

Waziri alisema maeneo ambayo tayari yamejengwa matuta kuzuia maji ya chumvi, ni Koowe, Ukele, Tumbe na Kwa Jibwa iliyopo Kengeja.

Pia, ofisi hiyo imekusanya taarifa za maeneo yote yanayoingia maji ya chumvi Zanzibar, imebaini yapo maeneo 148.

Alisema ofisi hiyo hivi sasa imeanza mchakato wa kutayarisha mapendekezo ya mradi kwa baadhi ya maeneo hayo, ili hatua zinazostahili zichukuliwe.

Fereji alisema kisiwa hicho kinakabiliwa na tatizo la maji ya bahari kuvamia maeneo ya makazi ya wananchi, kutokana na wananchi kukata miti aina ya mikoko kwa matumizi ya ujenzi.

Alisema miti ya mikoko ni maarufu kwa kuzuia kasi ya maji ya bahari kuvamia maeneo ya makazi.

Alisema Serikali imechukua hatua za awali, ikiwamo kutoa ushauri wa kupandwa kwa miti aina ya mikoko pembezoni mwa bahari.

Waziri Fereji alisema SMZ tayari imetafuta mshauri mwelekezi kufanya tathmini ya kina ya athari za mazingira, zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi.

Alisema kazi ya mshauri mwelekezi ni kuangalia maeneo ya athari za mazingira, ikiwamo visiwa vidogovidogo ambako wanaishi wananchi.

Waziri huyo alisema Serikali inatarajiwa kupata Sh546 milioni kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Mazingira.

Source
: Mwananchi
 
View attachment 89702
Visiwa vya Zanzibar vinashuhudia maeneo yake kuingiliwa na maji ya bahari na kuathiri sehemu za kilimo.
Tayari maeneo 148 yameingiliwa na maji chumvi na hayafai tena kwa kilimo.
Nini hatma yake kwa miaka mingi ijayo?
SMZ yakiri kuathiriwa mabadiliko tabianchi - Kitaifa - mwananchi.co.tz

MUNGU NI MKUU, Haya maji Bahari yataimarisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, wachache sana watabeza maneno yangu. Kiburi cha hao Wazanzibar kuwafukuza wenzao kutoka huku Bara kitakwisha.
 
Kuna mzanzibar mmoja aliniambia yeye kaamua kununua shamba kisarawe baada ya kutambua kuwa quran imetabiri visiwa vya zanzibar ni miongoni mwa visiwa vitakavyomezwa na bahari. Nikabaki najiuliza, hao UAMUSHO hawazijui hizo aya?
 
Ikiwezekana wamezwe na bahari kabsa kisiwa kipotee tuone watakumbilia wapi
 
MUNGU NI MKUU, Haya maji Bahari yataimarisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, wachache sana watabeza maneno yangu. Kiburi cha hao Wazanzibar kuwafukuza wenzao kutoka huku Bara kitakwisha.

Thubutu.
Hivi unawajua ama unawasikia?
 
Kwa kila la heshima,
Nikufahamishe kidogo siyo Kisiwa chetu tu kumezwa na mafuriko ya bahari, bali viswa vingi Km; maldive,mauritus,syecheells na maelfu ya huko mashariki ya mbali.....! hiyo kutokana na glob-warming!!
 
Oh Sister, siyo kiburi its just Haki ya anayomiliki!!

Sasa nasi waBara tutapokea jangaa letu kwani yote ni mifululizo ya mabadiliko ya tabianchi, nk.
Good luck tukiwa hai .....!!
 
Wazanzibar turudini kwa mungu na pia aminini kuwa binadam wote ni sawa, mungu hajabagua kutuleta duniani. So usimuone mwenzio kama mnyama kwa ajili ya imani yako.

Kumbukeni ya kuzama kwa meli na hili sasa pia fananisheni na ukatili munaowafanyia wenzenu. Sina uhakika sana kama kuna uhusiano ila ni bora muamini hivyo itawasaidia.
 
nawajibu wanaobweteka!!
with respect..Re: Zanzibar: Ardhi maeneo 148 yaliwa na Bahari
Oh Sister, siyo kiburi its just Haki ya anayomiliki!!
Kwa kila la heshima,
Nikufahamishe kidogo siyo Kisiwa chetu tu kumezwa na mafuriko ya bahari, bali viswa vingi Km; maldive,mauritus,syecheells na maelfu ya huko mashariki ya mbali.....! hiyo kutokana na glob-warming!!
Sasa nasi waBara tutapokea jangaa letu kwani yote ni mifululizo ya mabadiliko ya tabianchi, nk.
Good luck tukiwa hai .....!!​
 
Hii habari si ingewekwa "international forum"? Zanzibar si wanajiita ni nchi? Waache wadeal na matatizo ya nchi yao wenyewe.
 
Oh Sister, siyo kiburi its just Haki ya anayomiliki!!
Kwa kila la heshima,
Nikufahamishe kidogo siyo Kisiwa chetu tu kumezwa na mafuriko ya bahari, bali viswa vingi Km; maldive,mauritus,syecheells na maelfu ya huko mashariki ya mbali.....! hiyo kutokana na glob-warming!!
Sasa nasi waBara tutapokea jangaa letu kwani yote ni mifululizo ya mabadiliko ya tabianchi, nk.
Good luck tukiwa hai .....!!

HAWAII ISLAND Shall never Emerge Again
 
Wazanzibar turudini kwa mungu na pia aminini kuwa binadam wote ni sawa, mungu hajabagua kutuleta duniani. So usimuone mwenzio kama mnyama kwa ajili ya imani yako.

Kumbukeni ya kuzama kwa meli na hili sasa pia fananisheni na ukatili munaowafanyia wenzenu. Sina uhakika sana kama kuna uhusiano ila ni bora muamini hivyo itawasaidia.

Nyerere JK alisema "Kwa hili la Ubaguzi Haki ya Mungu Naomba Mungu Asiwasamehe"
 
udongo watautoa wapi...

Hujawaelewa. Wanasema maji ya bahari yanaingia nchi kavu na kufanya ardhi kutofaa kwa kilimo kutokana na chumvi nyingi. Soln ni kuzuia maji yasije nchi kavu kwa umbali fulani
 
Kiukweli watanganyika akili zenu weng zimefanana na unyerere si mnakumbuka nyerere alisema angekuwa na uwezo angevisukuma visiwa hivi bahari ya mbali?lakini vimemshinda sasa kaenda yeye yupo ardhi ya mbali,msizani mungu alikosea kuumba tanganyika kwake na visiwa kwake,hatuutaki muungano hata kama tutazama sote waz'br.
 
Back
Top Bottom