Hawa Malawi siyo bure kuna msukumo wa mataifa ya nje,hata kupigana nao tutakuwa tunapigana na mataifa mengine ya nje,hizi ni mbinu wanazotumia mabwanyenye kudhoofisha mataifa tajiri masikini ili yaweze kuchukua mali kirahisi,Tanzania tuna gesi ya kutosha,dhahabu ya kumwaga,bado uranium,shaba makaa ya mawe na mafuta na tuko salama hauoni ajabu?fikiria kilichotokea Somalia na mafuta yao,Sudani,Nigeria,Angola,jirani zetu DRC na uifikirie TZ ni mungu tu anaweka mkono wake ila hili la Malawi ni lazima tuliangalie kwa jicho pevu vinginevyo tumekwisha,na serikali yetu hii isiyoeleweka tunaweza kujitumbukiza katika shida kubwa ambayo inaweza kuchukua zaidi ya miaka 50 bila majibu tukabaki ambaomba wa misaada ya kijeshi huku wakichukua rasilimali zetu kwa kubadilisha na silaha.