Sijali
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 2,700
- 1,857
Kweli maadili yako mferejini. Zamani mtu hamzungumzii vibaya mtu aliyefariki, katu. Jee, ni kweli kwamba watu hawana tena imani na yanayotokea baada ya kifo? Au hawajali tuu?
Binafsi nadhani huku kuenea sana kwa utamaduni wa vitu (materialism) kumewafanya watu hawafikirii tena yaliyo baada ya vitu (metaphysics). Hii ni hatari. Siku moja utajikuta ghafla kaburini.....na jee kama yaliyokuwa yanasemwa ni kweli, utafanyaje? Mtu mwenye akili timamu atakiwa asiweke mayai yake yote katika kapu moja! Siku zote atafakari: jee kama....?