Zambian President, Michael Sata dies in London

Zambian President, Michael Sata dies in London

Hivi hii ilitabiriwa na Temitope Joshua...??
(1) Mola wako ndiye mjuzi wa mambo ya siri (including yatakayojiri baadae kama vifo n.k) pekee.
(Na ziko kwake (Allaah) funguo za siri; hakuna azijuaye ila Yeye tu.) [Suratul-An'Am, 59]

(2) wale (mfano wa TB Joshua) wanaojifanya kujua yatakayojiri ambayo uhakika yanafahamika kwamba watu hawana uwezo nayo kuyafahamu (mambo ya ghaibu) kama vifo, ajali n.k wasifikiri wataachwa bure tu kwa hayo matabiri yao bali wataadhibiwa adhabu kali na mola wao.
((Kwani yeye amepata khabari za ghaibu, au amechukua ahadi kwa Arrahmani Mwingi wa Rehema?))
((Hasha! Tutaandika anayoyasema, Tutamkunjulia muda wa adhabu)) [Maryam: 78-79].
 
RIP Michael Satta,Mungu aifariji familia yake na wazambia wote katika kipindi hiki kigumu.
 
Hahaha...

Kama ni rahisi hivyo hebu fanya kutupa utabiri wa Bwana Mamvi maana nasikia naye afya yake si imara sana...
Baada ya wapelelezi wa Temitope Barogan kuja kuchunguza hali ya kisiasa nchini, walimrudishia majibu nabii kwamba mamvi is politically powerfully, hivyo akatabiri kuwa ndiye ajaye!!
 
Kha ha ha haaaaaaa! Mkuu Kuna huu usemi wa Waswahili "KUUGUA SIYO KUFA MGANGA NI MUNGU" umeisahau???

Satta apumzike kwa Amani yake Bwana wetu!
Inategemea unaugua nini mkuu, kuna maradhi mengine ukiugua inakuwa ni suala la muda, hata muda wenyewe unaweza kukadirika!!
Sasa kuna wajanjawajanja wanashika watu kirahisi tu kwa kujifanya eti wanatabiri, wakati kuna mambo yako wazi kabisa, halafu ni wajanja sana, wanatabiri katika namuna ambayo i kiakili sana, yasipotokea wanayotabiri wanakwambia sikumaanisha hivyo..

Ujanja ujanja tu, mtu ni bilionea, ameshasahau hata lile fundisho la yesu kuwa itakuwa rahisi kwa ngamia kulipenya tundu la sindano, kuliko"bilionea"kuingia mbinguni!
 
Back
Top Bottom