Zambia yafungua mpaka na Tanzania

Zambia yafungua mpaka na Tanzania

Kila mmoja wetu ombi lake ni kuhakikisha chanzo inapatikana mapema kuliko kawaida.

Lakini dunia ifanyeje wakati wataalamu wapo kusugua vichwa huko kutafuta tiba je, iendelee kujifungia ndani.

Tuchukue tahadhali tuheshimu ushauri wa wataalamu.

Hatuwezi kusimamisha kila kitu kisa ugonjwa unaoua mtu mmoja kati ya watu kumi wanaoumwa.
Hakuna anayeshabikia "kusimamisha kila kitu".

"Kusimamisha" kulikuwa na maana yake katika wakati wake..., kabla ya kujua tabia ya huyu coronavirus ipoje.
Mtu kujiamria tu, "mimi sisimamishi", na huku huna ufahamu wowote juu ya huyo adui.

China alisimamisha Wuhan, na alifanikiwa, mfano huo hatupendi kamwe kujikumbushia!

Wataalam wanasugua vichwa, lakini hawa wa kwetu hata ule ushauri tu tukawapuuza!

Ni nani aliyejua wakati huo kwamba COVID-19 inaua "mtu mmoja kati ya watu kumi wanaoumwa"?

Huku ni kutafuta kujisafisha kwa makosa yaliyofanyika.
 
Wapi hujaelewa mkuu.?

Ni kwamba Wilaya ya Nakonde ambayo ndio imepakana na Tunduma ndio ilipigwa lockdown wananchi wake walifungiwa toka tarehe 10/5.

Yaani mabasi ya kutoka sehemu zingine ndani ya Zambia hususani Lusaka,Kitwe, Ndola hayakurusiwa kuja Nakonde Wala ya Nakonde kwenda huko.

Ila huko kwingine shughuli zilikuwa zinaendelea kama kawaida.!
Wamefungua kwa business as usual au kuna conditions?
 
Rais wa Zambia Edger Lungu akihutubia Taifa Jioni hii tarehe 22/5 amefungua rasmi mpaka na Tanzania na kuruhusu wananchi kuendelea na shughuli zao kama kawaida.

Rais Lungu amesema wananchi waendelee na shughuli zao huku wakifuata maoni na ushauri wa wataalamu.

Ukumbukwe Zambia ilifunga mpaka wake na Tanzania toka tarehe 10/5, huku wilaya ya Nakonde ikipigwa lockdown.

Mabasi na magari yote ya abiria hayakuruhusia kuingia Nakonde Wala kutoka, ni malori ya trust tu ndio yaliyoruhusiwa nayo kwa utaratibu maalumu.

Kumbe Tanzania na Zambia tune zenu za Wimbo wa Taifa zinafanana nadhani pia na SA. Ningependa kujua nchi ipi ilitunga hii tune?
Kwenye issue ya Corona mimi ni pro lock down lakini naona kama vile tumepotezana njia kama US na UK wanafungua hata sijui tufuate au tumuige nani.
 
May 22, 2020
National Address By President Edgar Lungu On Covid-19

17: 36' country men and women, Nakonde business activities and in other provinces will be allowed to flow as normal while observing health guidelines. Covid -19 is no longer pandemic it is an epidemic so we should learn to live with it. Covid -19 has transform ourlives in term of maintaining and adherence to handwashing and social distancing measures
Source : Zambian Portal

Kenya ma zambia wamesalim amri...
 
Kumbe Tanzania na Zambia tune zenu za Wimbo wa Taifa zinafanana nadhani pia na SA. Ningependa kujua nchi ipi ilitunga hii tune?
Kwenye issue ya Corona mimi ni pro lock down lakini naona kama vile tumepotezana njia kama US na UK wanafungua hata sijui tufuate au tumuige nani.
Tatizo huu ugonjwa tunaowategemea watuongoze nao wapo gizani.
 
Endelea kuamini uongo wake. Eti Janja janja wakati Watanzania wanakufa!!! Kweli upumbavu nacho ni KIPAJI. Kama anajiamini kwanini ANAZUIA takwimu za wagonjwa na vifo nchini kwa wiki nne ili KUTHIBITISHA kauli yake ya ugonjwa kupungua?

Usiamini kila kitu mkuu, huu ugonjwa ni janjajanja nyingi sana, Ni Rais wetu tu ndo amegundua. Tujiulize Magufuli anajiamini niini?
 
Endelea kuamini uongo wake. Eti Janja janja wakati Watanzania wanakufa!!! Kweli upumbavu nacho ni KIPAJI. Kama anajiamini kwanini ANAZUIA takwimu za wagonjwa na vifo nchini kwa wiki nne ili KUTHIBITISHA kauli yake ya ugonjwa kupungua?
Wewe umekufa au kwenu kuna yeyote amekufa kwa Corona? Unadhani Rais ni mjinga kuruhusu Vyuo kufunguliwa? Wajinga ndio waliwao, hofu inaua mkuu, acha hadithi njoo kwenye field.
 
Acha ujinga wewe! Kama kwetu tunachukua TAHADHARI ZOTE kujilinda na covid itatupataje? Na kwa kuwa kwetu hakuna aliyekufa HAIMAANISHI hakuna ugonjwa ambao umeshaua Watanzania wengi tu.

Bila kuweka TAKWIMU husika ni UPUUZI kuruhusu vyuo vifunguliwe na hivyo kuendeleza maambukizi Nchini.

Hunijui wewe acha KUJIBARAGUZA eti njoo kwenye field.

Unajuaje kama na wengine wanachukua tahadhari kama kwenu mkuu? Mkuu nikupe assignment kidogo, tafadhali kajisomee uone ni jinsi gani kinga ya mwili inakuwa developed. Au search kwenye YouTube namna ugonjwa huu ulivyo na siasa nyingi kuliko ukweli. Janjajanja kibao, Magufuli kawashitukia. Kama swala LA Dawa ipo Madagascar ila sasa ona WHO wafnavyozunguka.
 
Watu wanakufa Sana . Serikali haipimi naona wameamua tutakaokufa tufena watakaobaki wabaki.
Inaonesha kadri watu wanavyozidi kufiwa na ndugu zao kwa wingi kutokana na corona ndivyo wanavyozidi kuacha kujikinga na corona, sasa hivi barakoa hazivaliwi sana kama mwanzo na sasa watu ndio hawana hofu kabisa kufanya mikusanyiko.
 
Wabunge wangapi wamekufa kwa kipindi kifupi? Mazishi ya usiku kwanini wafiwa WALAZIMISHWE kuzika usiku? Kwanini balozi za USA [emoji631] na UK [emoji636] ziondoe raia wao ili kuwaepusha na covid huku wakisema hospitali za Tanzania zimeelemewa na Serikali kupiga kimya!? TAFAKARI kwa kina Mkuu.
Mkuu ni vyema kutujuza hospital zipi tutimbe tukacheki pakoje. Uzuri wagonjwa au wenye dalili wanatengwa ivyo ni rahisi kuwajua.

Pili tuko na madaktar wanaotwambia kinachojiri na humu jf wapo ni bora wazibitishe watupe mwanga.

Kikubwa ni kufurahi na kumshukuru mungu kama wewe, na familia yako haijapata shida kwa corona. Mengine kumwachia Mungu.
.
.
.

*propaganda ya uchumi*

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatari sana inaonesha kadri watu wanavyozidi kufiwa na ndugu zao kwa wingi kutokana na corona ndivyo wanavyozidi kuacha kujikinga na corona, sasa hivi barakoa hazivaliwi sana kama mwanzo na sasa watu ndio hawana hofu kabisa kufanya mikusanyiko.
Umefiwa na ndugu zako wangapi?
 
Back
Top Bottom