Zambi ataka serikali ilazimishe wasomi wa KiTZ warudi

Leo mapema nikiwa ndani ya ukumbi wa Bunge , ndugu Zambi alisimama kuchangia na akataka kujua kwa nini Serikali isitumie nguvu kuwarudisha nyumbani ma expert wote watanzania wanaofanya kazi nje ya Nchi na kupata kipato kikubwa .Haya yalizuka baada ya Bunge kuelezwa kwamba watu wakisha soma Ulaya hubakia na kupata mishahara minono huko .
Kombani kasimama na kusema serikali inaweza kusema nasi kwa utaratibu wa kutuomba na si kuomba kwa nguvu tunyimwa ajira .Huyu Zambi nimeshangaa uwezo wake wa kuelewa mambo .Mwaka 2008 yeye anafikiria miaka ya 60 ? Wewe unasemaje ?

Alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi (CCM). Katika swali lake la nyongeza, Zambi alihoji juu ya watumishi wa serikali wanaopelekwa masomoni nje ya nchi kutorejea baada ya kumaliza na kwa nini serikali isiziandikie barua nchi husika kutowaajiri.


No Comments
Source
 
Hii ni roho mbaya ya Zambi .Huyu kweli hana watoto walioko ughaibuni kwa pesa za walipa kodi wa TZ ?
 
Kwa kweli hakuna kitu ambacho wabongo wanakipenda kama kuishi Bongo. mtu yeyote mwenye kazi ya Maana bongo, hawezi kufikiria kubaki nje ya nchi yake. Tatizo linakuja ni pale wanasiasa wanapojifanya wao ni kila kitu, Yaani Madaktari, mainjinia, wahasibu, n.k. Ukifanya kazi nje ya nchi utakuta wanasiasa wao ni policy makers tu na hawaingilii utendaji, hivyo kuwapa wataalam nafasi ya kutumia elimu yao vizuri.

Bongo kama wewe ni mtaalam na humjui mwanasiasa mwenye ushawishi, ujue vyeti vyako vitaliwa na mchwa kabatini, hakuna wa kukujua. Bongo hapendwi mtu, haipendwi nchi bali ni maslahi binafsi ya wanasiasa. Kwa nini watu wasijenge nchi za watu na wao kujijengea maisha bora?.

Wanasiasa waache longolongo kwanza na ubinafsi kabla ya kuwalaumu wanaoamua kujitafutia riziki zao nje ya nchi. Leo hii siasa bongo inalipa zaidi ya utaalam, hebu angalia bungeni leo kuna wasomi wangapi wenye PhD na Masters wanachapa usingizi bungeni wakifukuzia posho za vikao badala ya kufikiria na kutumia taaluma zao kwa maendeleo ya nchi?

Bongo watu wanasoma ili kuwa wanasiasa, kama hutaki kuwa mwanasiasa ujue umeliwa ni bora ubakie kwa watu ujiendeleze.
 
Ogah,

Hivi waki-opt kupoteza ajira kuna sheria gani kuwashurtisha warudi?

Ikiwa tunashindwa kurudisha fedha za uhujumu na uzembe wa viongozi wa Serikali leo tunasema tuunde sheria na kulazimisha waliochoka ajira za Jamhuri warudishwe kitemi?

.......sio kurudishwa kitemi lah hasha....ila kuwepo na system/utaratibu/sheria ambayo kwa namna moja au nyingine.......itatu-cover/linda na loss ina/itakayotokea.........NOTE hii i-apply kwa wale waliotumwa na kusomeshwa na serikali...........

.......binafsi sifagilii kabisa kuhalalisha kosa kwa kutumia kosa jingine......na kuidanganya system/serikali ili kujinufaisha binafsi......ndio vita tunayopigana nayo kila siku hapa JF.............

...Ninacholaumu kutoka kwa Waziri Kombani ni kuwa jibu lake ni very WEAK..........kwani kama policy makers wanatakiwa kujifunza kutokana na makosa yaliyopita........hili jambo la kusomesha wafanyakazi wa serikali na wafanyakazi hao kutokomea huko huko si geni.........na i doubt sana na hizo Data zake kuwa ni sahihi.........nafikiri idadi ni kubwa zaidi.........

.....i mean watu wasikatazwe kufanya kazi huko nje endapo watapata......kwani nayo ni experience ya aina yake ambayo ikiletwa nyumbani........itakuwa na faida kwa Taifa

.....yes ni kweli inatakiwa iwepo sheria ya kuwabana wafanyakazi wa serikali wanaopelekwa kusoma kwa pesa za kodi zetu.........ili warudi kutumikia kile ambacho alitumwa kukisomea ili i-advance ufanisi makazini.........kumbuka pia kuwa wengi wao hulipwa mishahara kama kawaida...............

.......sasa kama mtu binafsi ameamua kuivunja sheria hiyo....hilo ni suala jengine.....lakini sheria ni MUHIMU ikawepo ya kulishughulikia hili tatizo.......

..........tusipojiwekea hizi sheria hata mafisadi tutawabana vipi kama tutaruhusu mianya kama hiyo kuwepo.............

......tuendelee kujifunza kuwa na discipline.......ili tupambane vema na mafisadi/ufisadi.........otherwise tutakuwa tunapigana vita ya maji maji (ofcourse not to offend no anybody)
 
Kasema hayo maneno au wewe umeongezea tu na kuja na title zako tu?Mwanakijiji nadhani anafaa kuwa Mwandishi wa Lowassa kwa sasa.
Ni kweli alisema nimeona katika tv na ni kweli Kombani alisema serikali haiwezi kuwarudisha kwa nguvu maana wao wanajitafutia maslahi manono manono kama vile wabunge walivyoacha kazi zao na kwenda katika siasa ili kujitafutia maslahi mazuri kidogo.
Ilinishangaza kwamba kumbe wabunge uenda kule bungeni kwa ajili ya maslahi tu wala si kuwatumikia wananchi na nadhani huu ndio ukweli mweupe aliouanika Selina Kombani.
Nakushauri Gembe ubaki huko huko S/A hakuna atakayekulazimisha kurudi kama maslahi yakipendeza.
Na mimi sasa nafuta nchi nikatafute maslahi. Naweza kuwa mlinzi yaani huku wanaitwa watchman. Maana sisi kabila letu huku kaskazini ya Tz ndio mabingwa wa kazi hiyo
 
Sioni ubaya ni kwa nini wasirudi, cha msingi hapa ni kuwashawishi warudi na kupatiwa ujira mzuri, sasa wewe uko nje ya tanzania kwa ajili ya masomo, ukisha maliza masomo basi rudi nyumbani kasaidie kujenga inchi kwa utaalamu elimu na exposure uliyopata, daima inchi hujengwa na wenye inchi....narudi tena serikali itengeneze mazingira mazuri ya kuwashawishi na kuwalipa ujira mzuri, ikifanya hivyo hakika watarudi, nani anayefurahia baridi, vyakula vya kopo, maisha ya speed ya ajabu, kazi zisizopungua watu wanafanya hivyo kwa ajili ya maisha....wanandugu na jamaa ambao wanawategemea nyumbani Tanzania...watu wanatamani kurudi nyumbani, kunjwa kilimanjaro baridi, nyama choma na vyakula fresh na vitamu vya nyumbani....wanatamani kurudi na kufanya kazi masaa nane...kinachoshindikana ni ujira mdogo....ni hayo tuu
Shida wakirudi hapa kwetu hawa wanasiasa ambao hatukwenda shule tunawadharau sana maana mishahara yao itakuwa kidogo wakati sisi tunapeta na mishahara minono na pensheni ya sh. 20,000,000 kila miaka 5. wakati huo huo wao wakistaafu mbali na kupunjwa hata hiyo pensheni haitoshi nauli ya kuifuata mjini ambako ndiko banks ziko.
Sasa si afadhali wakae huko huko wanakowajali na hapa tuwaachie wana si hasa, waendeshe nchi yao? Ya nini waje kwenye shida na mahali hakuna mtu anawajali? Mwisho na wao watafundishwa ufisadi na tuanze kuwamela
.
 
Kwa kweli hakuna kitu ambacho wabongo wanakipenda kama kuishi Bongo. mtu yeyote mwenye kazi ya Maana bongo, hawezi kufikiria kubaki nje ya nchi yake. Tatizo linakuja ni pale wanasiasa wanapojifanya wao ni kila kitu, Yaani Madaktari, mainjinia, wahasibu, n.k. Ukifanya kazi nje ya nchi utakuta wanasiasa wao ni policy makers tu na hawaingilii utendaji, hivyo kuwapa wataalam nafasi ya kutumia elimu yao vizuri.

Bongo kama wewe ni mtaalam na humjui mwanasiasa mwenye ushawishi, ujue vyeti vyako vitaliwa na mchwa kabatini, hakuna wa kukujua. Bongo hapendwi mtu, haipendwi nchi bali ni maslahi binafsi ya wanasiasa. Kwa nini watu wasijenge nchi za watu na wao kujijengea maisha bora?.

Wanasiasa waache longolongo kwanza na ubinafsi kabla ya kuwalaumu wanaoamua kujitafutia riziki zao nje ya nchi. Leo hii siasa bongo inalipa zaidi ya utaalam, hebu angalia bungeni leo kuna wasomi wangapi wenye PhD na Masters wanachapa usingizi bungeni wakifukuzia posho za vikao badala ya kufikiria na kutumia taaluma zao kwa maendeleo ya nchi?

Bongo watu wanasoma ili kuwa wanasiasa, kama hutaki kuwa mwanasiasa ujue umeliwa ni bora ubakie kwa watu ujiendeleze.Maneno haya ni mazito sana .
 
Ma-expert wengi sana wa kiTz waliosoma nchi za nje katika miaka ya tisini na hii ya elfu mbili hawakulipiwa na serikali. Waliolipiwa na serikali ni wale waliokuwa connected ndani ya serikali. Kama kuna MTz aliyezamia meli kwenda ughaibuni, halafu kufika huko akabeba maboksi huku akijisomesha kidogo kidogo hadi akawa expert anayelipwa hela nyingi, je serikali ya Tz ina hisa gani kwake kutaka kumrudisha kwa nguvu?

Hata wale waliolipiwa na serikali, bado siyo busara kuwarudisha kwa nguvu kwani tunaweza kuwaharibia maisha yao na ya wale ndugu zao wanaopata cheki ya westernunion kila mwezi bila sisi wenyewe kufaidika lolote kama taifa. Ni afadhali tuendelee kupokea hizo remittances za Westernunion na Moneygram kuliko kuwalazimisha jamaa hawa kurudi Tanzania ambako huenda hawatafanya kazi yoyote ya kulisaidia Taifa. Wahenga walisema kuwa unaweza kumpeleka ngombe kwenye maji lakini huwezi kumlazimisha kuyanywa.
 
Serikali inatakiwa kuweka mikataba na balozi zote kama mtu umesomeshwa na serikali na hutaki kurudi kwa sababu binafsi basi serikali itakupa miaka mitano au kumi kulipa deni lako la shule. Kama umejishomesha mwenyewe ni uamuzi binafsi kurudi Tanzania au kubaki nchi za nje. Mimi kwa mfano nimejisomesha peke yangu hivyo uamuzi wa kurudi ni wangu na sijatumia pesa ya uma.Kama mtu hatataka kurudi na kasomeshwa na serikali basi serikali ya nchi anayoishi itaweka mpango wa kumkata pesa polepole kwenye Income yake kurudisha gharama.
 
Say what,

Mkuu Mchukia Ufisadi am I reading you right kwamba Waziri Selina Kombani kaanika wazi sababu ya watu kugombea ubunge kuwa ni maslahi binafsi?
 
Serikali inatakiwa kuweka mikataba na balozi zote kama mtu umesomeshwa na serikali na hutaki kurudi kwa sababu binafsi basi serikali itakupa miaka mitano au kumi kulipa deni lako la shule. Kama umejishomesha mwenyewe ni uamuzi binafsi kurudi Tanzania au kubaki nchi za nje. Mimi kwa mfano nimejisomesha peke yangu hivyo uamuzi wa kurudi ni wangu na sijatumia pesa ya uma.Kama mtu hatataka kurudi na kasomeshwa na serikali basi serikali ya nchi anayoishi itaweka mpango wa kumkata pesa polepole kwenye Income yake kurudisha gharama.

Kamundu,

Umejisomesha mwenyewe kuanzia shule za msingi mpaka chuo kikuu?

Unajua hapa tunaweza kuanza kunyosheana vidole, kumbe vidole vingine vinatusuta na sisi pia.

labda kwa watu ambao wameishi nje toka utoto wao, vinginevyo kila mtu amesomeshwa na taifa kwa njia moja ama nyingine.
 
Kamundu,

Umejisomesha mwenyewe kuanzia shule za msingi mpaka chuo kikuu?

Unajua hapa tunaweza kuanza kunyosheana vidole, kumbe vidole vingine vinatusuta na sisi pia.

labda kwa watu ambao wameishi nje toka utoto wao, vinginevyo kila mtu amesomeshwa na taifa kwa njia moja ama nyingine.


Mimi ni kati ya wachache wanao weza kusema asilimia 99% yua shule yangu ni Baba yangu na watu walio nisaidia kufikia hapa.Yet naitumikia Serikali kwa kipato kidogo sana .Zambi nadhani he need to think again .
 
Huyu Zambi afikirie tena.....kwanza kuna baadhi ya fani watu walizosomea hazipo tanzania......nani anataka kuwa frastreted na maovu ya serikali ya Kikwete.Tanzania kuna mambo yanaudhi sana......hili la Dr Masau mbona dogo......kaeni huko huko ili mradi hamfanyi illegal business...
 
Say what,

Mkuu Mchukia Ufisadi am I reading you right kwamba Waziri Selina Kombani kaanika wazi sababu ya watu kugombea ubunge kuwa ni maslahi binafsi?

Yesssssssssssssss kama kuna waliomsikia na wabishe kama hakusema!!!!!
 
Kwa watu kama sisi MAN ALONE ambao hatujapata msaada wowote kutoka huko bongo...Kwa kweli inakuwa hatutendewi haki kama serikali itaongea na sisi kwa lugha za kibabe.

Kwanza mtu kama mimi ndio hata sijui...Kwasababu serikali imeninyanyasa maisha yangu yote na ndio maana hata neno ccm kwangu ni kichefu chefu...Yani hata kama kusingekuwa na vyama vya upinzani ama hata siasa za mageuzi...Still ccm kwangu siipendi kabisa...Ni chama chenye wenyewe...Na wafuasi masikini wasiojaliwa...Ni chama kilichotekwa...Na kubadilika kuwa chama cha mapinduzi ya kifisadi kwenye historia ya Taifa letu.

ccm wamepoteza vipaji vingi sana kwenye kizazi cha Taifa letu toka UHURU na bado wanaendelea na system ile ile...Ila sasa hivi nia na madhumuni vimebadilika kwasababu sasa na UTAJIRI wa Taifa letu unaporwa wazi wazi tofauti na zamani amabpo walikuwa wakipora na kuendelea kutupatisha shida sisi watoto wa Tanzania na huku wakutuimbia sisi ni masikini na wao ni wazi nai MATAJIRI.. na huku stori za mtaani ama hali halisi ya wanasiasa walio karibu na viongozi wakuu wa serikali na wengine wenye ushawishi mkubwa ikizidi kuneemekea na huku wakitumia dola kama vile jeshi la wananchi na polisi nk.

Kwangu mimi nikisikia serikali nakumbuka manyanyaso na wala sina kumbu kumbu yoyote nzuri kwani sikuwa hata na qualification ya kusomeshwa na serikali bali kunyanyaswa kuonekana sifai kama ilivyo kwa vipaji vingine na pia vingine hata vimeshazikwa kabisa.

Hakuna siku nimeshawahi kujivunia kuwa kuna opportunity na HASWA nchini kwetu.

Watu ni wale wale na kazi ni kwa undugu na kujuwana nk.

Pamoja na hayo...Jamii inateketea kwani hata hao wanaofanya kazi hizo za kusimamia mali na shughuli za serikali na Taifa kwa ujumla...Hawana accountability na wao hufanya chochote wanachotaka na UTU UMEPOTEA.

Kwetu sisi tunaopambana wenyewe...Ambao serikali ilitutupa...Hatuna haja ya kubabaikia.
 
Kwangu mimi nikisikia serikali nakumbuka manyanyaso na wala sina kumbu kumbu yoyote nzuri kwani sikuwa hata na qualification ya kusomeshwa na serikali bali kunyanyaswa kuonekana sifai kama ilivyo kwa vipaji vingine na pia vingine hata vimeshazikwa kabisa./QUOTE]
Unailaumu serikali kivipi
 
Zambi nadhani ana Dhambi , matatizo ya Nchi hii ni mengi na yameletwa na CCM na kubweteka kwamba Tanzania imejaa amani na Utulivu huku kura zaibwa nk .
 
Kisheria unaweza ku force mtu arudi nchini?

Kama utamzushia kwamba ni muuza unga na gaidi unaweza kwa njia moja ama nyingine kumlazimisha akimbie huko lakini bila ya haya hakuna lolote kama hana criminal records na awe wanted na wewe unayemtaka uthibitishe madai yako.It is a process not a quick thing though
 
Back
Top Bottom