Zambi ataka serikali ilazimishe wasomi wa KiTZ warudi

Je Tanzania ikimtaka mtaalamu wa kitanzania aliyebobea kwenye aerospace engineering arudi Tanzania, je mtaweza kumpatia lab ya kufanya mavitu yake? Ni lini Tanzania inategemea kutuma astronauts mwezini?

Hata nchi kubwa kama USA ikitoa tamko la kidizaini hii, nchi hiyo haitaweza kuwa-contain wasomi wote na kuwapatia ajira, maana kuna wengine wamesomea vitu ambavyo ni vigumu kupata kazi ya kuajiriwa na serikali.

Wanasiasa wetu ni bora wakaachana na propaganda zisizo na msingi. Globalization is the way of life!!! Badala ya kupoteza mda kujadili masuala yasiyo na majibu ni bora wakatilia mkazo masuala yaliyo solvable, like KIWIRA, listi ya wafanyabiashara wa madawa ya kulevya, BOT, barabara mbovu, mahospitali yasiyo na vyandarua wala madawa etc
 
UKiangalia kwa umakini kuna mambo mengine yanatisha na yanaletwa na serikali kutowalipa vizuri watu wake.......mfano Msumbiji 75% ya Physician wake wanafanya kazi nje wengi wao wakiwa Ureno......
.....nchi kama Ghana inakadiriwa 56% wanafanya kazi nje na kameruni wako 46% sasa data hizi ni hatari kubwa.....

Afrika ndio inahitaji kwa wingi watalaam hawa na wao wanakwenda nje kwa kuangalia maslahi...kweli nawaunga mkono sidhani kama kuna kasota Muhimbili miaka zaidi ya 5 na Supp na Disco juu afu aje akubali kulipwa 150,000/= huku anaona sehemu nyingine anaweza kupata $80000 kwa mwaka.

Hebu angalia kwa upande wa tanzania.....utafiti wa mwaka 2000
Idadi ya madaktari Tanzania 1,264

Idadi ya madaktari ambao wapo nje 1356

Idadi ya manesi Tanzania 26,023

Idadi ya manesi ambao wapo nje 953


Hali hii inatisha....nani wa kulaumiwa?
 
UKiangalia kwa umakini kuna mambo mengine yanatisha na yanaletwa na serikali kutowalipa vizuri watu wake.......mfano Msumbiji 75% ya Physician wake wanafanya kazi nje wengi wao wakiwa Ureno......
.....nchi kama Ghana inakadiriwa 56% wanafanya kazi nje na kameruni wako 46% sasa data hizi ni hatari kubwa.....

Afrika ndio inahitaji kwa wingi watalaam hawa na wao wanakwenda nje kwa kuangalia maslahi...kweli nawaunga mkono sidhani kama kuna kasota Muhimbili miaka zaidi ya 5 na Supp na Disco juu afu aje akubali kulipwa 150,000/= huku anaona sehemu nyingine anaweza kupata $80000 kwa mwaka.

Hebu angalia kwa upande wa tanzania.....utafiti wa mwaka 200
Idadi ya madaktari Tanzania 1,264

Idadi ya madaktari ambao wapo nje 1356

Idadi ya manesi Tanzania 26,023

Idadi ya manesi ambao wapo nje 953


Hali hii inatisha....nani wa kulaumiwa?

Mwaka 200? duh! zamani sana hiyo mzee!, natania najua ulimaanisha mwaka 2000
 
Zambi inabidi aanze mjadala wake kwa kutoa hoja binafsi bungeni kuwazuia wabunge wote wenye taaluma nyeti kurudi kwenye taaluma zao, kabla hajaanza kuitaka serikali kuwaambia kina Mwanakijiji warudi.
 
Ni kuwa tumekuwa wabishi wa kuelewa alichosema Zambi au tunapinga kwa sababu ni mbunge wa CCM kasema?

Sidhani kama alimaanisha wasomi wote wa kitanzania walioko nje ya nchi bali wale watumishi wa serikali waliopelekwa na serikali na kulipiwa masomo baada ya kumaliza shule wanaingia mitini.
 
Nimelipenda jibu la Kombani, Zambi anawanyoshea vidole wenzake, kumbe na yeye kuna vidole vinne vinamsuta na kumwambia na wewe je?


Kuna njia nyingi za kuijenga nchi na wacha kila mtu aamue kuijenga nchi kwa njia zake.
 
Kamundu,

Umejisomesha mwenyewe kuanzia shule za msingi mpaka chuo kikuu?

Unajua hapa tunaweza kuanza kunyosheana vidole, kumbe vidole vingine vinatusuta na sisi pia.

labda kwa watu ambao wameishi nje toka utoto wao, vinginevyo kila mtu amesomeshwa na taifa kwa njia moja ama nyingine.

Mtanzania,

Kusomeshwa Bure shule ya msingi na sekondari hata chuo kikuu si kigezo cha kusema kuwa lazima mtu afanye kazi serikalini.

Huo ni wajibu wa Serikali kutoa elimu bila masharti. Kosa lililopo ambalo linaendelea na ndilo linasababisha elimu ya Tanzania iwe ni mbofu mbofu na kufanya wale wanaopata mwanya kulipiwa elimu ya juu na serikali kutokomea ni ile dhana ya kuendelea kusema kuwa elimu ya vyuo ni bure.

Kama elimu ya vyuoni ingetolewa na wanafunzi kujilipia, bila kuleta vijisababu vingi kama ulalahoi, basi wengi tungekwenda vyuoni na kuwajibika kulipa gharama iwe ni mikopo au utumishi wa miaka kadhaa, basi tusingekuwa na mazungumzo tunayofanya sasa hivi.

Watanzania ni watu ambao tumechanganyikiwa na hatujui kuchambua mifumo ya maisha na kiuchumi tuliyonayo.

Kwa nchi tajiri kama Marekani, elimu ya bure ni shule ya msingi na sekondari, hata hivyo ukitaka kujilipia kuna shule za msingi na sekondari za kujilipia.

Ukija kwenye vyuo, hakuna cha bure, hata hizo community college kila mwanafunzi analipa ada, iwe kutoka mfukoni mwake au kutokana na mikopo ya bodi za elimu (Perkins etc). Hivyo hakuna haja au ulazima wa kulazimisha mtu atumikie serikali au kufanya kazi eti arudishe fadhila.

Ni wale wanaokwenda Jeshini na kusomeshwa ambao huwa na mikataba ya kuwataka wakae Jeshini si chini ya miaka 6 kabla ya kuachana na jeshi na kuingia uraiani.

Sasa sisi Tanzania kama tunashindwa kuunda mfumo bora kama wa wenzetu, kwa nini tuendelee kulalama na kutaka kushurtisha ajira na utumishi Serikalini?
 
Serikali ina wajibu wa kutoa basic education (elimu ya msingi na sekondari) kwa raia wake bure kwa sababu inawalipisha kodi wananchi. Pesa zinazopatikana kutokana na kodi wanazolipa wananchi kila siku zinapaswa kutumika kuboresha miundombinu ya elimu katika nchi ili kuwawezesha raia kupata hiyo basic education.

Hakuna excuse kwa Serikali kuanza kuwabana watu eti mrudi kulitumikia taifa kwa kutumia kigezo kwamba wamesomeshwa bure. Kwani hao watu na wanafamilia wao wengine hawakulipa kodi? Hizi ni propaganda zisizo na misingi yoyote.
 
Ni kuwa tumekuwa wabishi wa kuelewa alichosema Zambi au tunapinga kwa sababu ni mbunge wa CCM kasema?

Sidhani kama alimaanisha wasomi wote wa kitanzania walioko nje ya nchi bali wale watumishi wa serikali waliopelekwa na serikali na kulipiwa masomo baada ya kumaliza shule wanaingia mitini.

........Icadon.......yaani im very much surprised.........this chama oriented thinking ni kitu mbaya sana.............

Halafu kilichonishangaza ni majibu ya Kombani.........yaani hii tunaita pure "mipasho"...........kwa jinsi hii ......kwa kweli tuna safari ndefuu sana
 
Ni kuwa tumekuwa wabishi wa kuelewa alichosema Zambi au tunapinga kwa sababu ni mbunge wa CCM kasema?

Sidhani kama alimaanisha wasomi wote wa kitanzania walioko nje ya nchi bali wale watumishi wa serikali waliopelekwa na serikali na kulipiwa masomo baada ya kumaliza shule wanaingia mitini.

Icadon unajua s'times inakuwa taabu hata kuchangia hoja sababu kuna watu wanajitahidi kutoelewa kilicho ongelewa. na ikiwa kimeongewa na ccm, hata ukitazama Lunyungu alivyo present no tofautu na Mwanakijiji alivyo quote kutoka gazeti. wengine cha muhimu ni ligi tu.
 
Watu wa aina ya Zambi hatuwahitaji kamwe bungeni. Hivi zambi anaelewa concept ya 'freedom of movement of labour?' Hivi Zambi hajui kwamba pesa zinazotumwa na wafanyakazi walio nje ya nchi (remittances), have become the second largest capital flow behind foreign direct investments (FDI) and ahead of Overseas Development Assistance (ODA)? in 2001 remittances represented 42% of FDI and a whopping 260% of ODA!! Remittances flows have surpassed ODA since 1996! Upo hapo mzee zambi?

remittances have significantly contributed to the improvement of the welfare of the receiving household ( utajua tu kaya ambayo mtoto wao anafanya kazi nje!). By the way the same applies to urban-rural remittances....ukiwa kijijini utajua tu kaya ambayo mtoto wao anafanya kazi daisalamu!

according to zambi basi wote tungebaki kijijini kushika jembe la mkono? na atangulie yeye!!
 
jamani hao wasomi mnaotaka warudi wapo? watanzania wengi wanaoenda nje kusoma huishia kurudia na kupata marks za chini sana, wapo wanaofanya fresh ila ukweli wengi hawafanyi vizuri, hio ndio sababu pia hawataki kurudi nyumbani, wengi wameishia kuacha shule...
swala hili la watanzania kutorudi nyumbani ni swala zitosana, na sababu ni nyingi zinazochangia wasirudi
 
Lunyungu, good to see you back.

Namuunga Zambi mkono in principal kwamba wale wote waliosomeshwa na serikali huku nje warudi kuitumikia Taifa japo kwa muda fulani kama kurudisha fadhila and offcourse kujenga nchi. Sioni kama ni matumizi makini ya kodi za wananchi iwapo hela zinatumika kusomesha wananchi nje halafu hawarudi kuwatumikia wananchi waliowasomesha.

Sasa tunaweza kujadili iwapo kubaki nje ya nchi kunaweza kuongeza uzalishaji Tanzania kwa namna moja au nyingine.

Katika kuonyesha kujisafisha na lawama za kuiba wasomi waliosomeshwa na Serikali zao; waingereza wakaja na utaratibu kuwa iwapo umesomeshwa na Serikali au British Council ni lazima wakupe barua ya kukuruhusu kufanya kazi UK kabla hawajakubalia kukupa Work Permit. Sasa kwa kiasi fulani naona iwapo hii itafuatiliwa na makini kuliko ilivyo sasa inaweza kurudisha kodi za wananchi japo kidogo.

Ukiwa mwingereza ukaenda kufanya kazi nje, sehemu ya mshahara wako inaingia kwenye serikali yako. Kwa maana ya kwamba haijalishi upo wapi, ili mradi unazalisha kipato pale ulipo basi serikali/ wananchi wako inafaidika moja kwa moja.


Naungana na Kaiyura kwamba, remittances zinazorudishwa nyumbani na walio nje ya nchi ni kubwa sana, kiasi cha kushindana na mauzo ya bidhaa zetu nje ya kila mwaka. Sasa basi sirikali haiwezi kuwarudishwa watu hawa wakati wao ni chanzo cha kipato kwa taifa na klwa wananchi pia.
Grow up man!
 
Icadon unajua s'times inakuwa taabu hata kuchangia hoja sababu kuna watu wanajitahidi kutoelewa kilicho ongelewa. na ikiwa kimeongewa na ccm, hata ukitazama Lunyungu alivyo present no tofautu na Mwanakijiji alivyo quote kutoka gazeti. wengine cha muhimu ni ligi tu.


Steetwiser mkuu ukitaka kuchangia wewe sema tu .Mimi nime sema haya baada ya kumuona na kumsikia Zambi LIVE .Maswali ya Zambi yamekaa ki dhambi sana .Sasa tafadhali sana changia mkuu badala ya kumtafuta nyoka miguu nakulinganisha watu .Au ulitaka niseme kama ulicho andika mkubwa .Karibu JF tafadhali naona ulikuwa hujafika .
 
Back
Top Bottom