Zamani ilikuwa raha

Zamani ilikuwa raha

hapo kwenye red panahitaji ufafanuzi ile wanetu waelewe vyema by the way nitaongeza hapa;

  • kuhamishiwa mtwara au sumbawanga kwa mfanyakzi ilikua laana tosha
  • tulitishwa kupelekwa mafya (kisiwani)
  • ukivaa chumpi mpya hasa za zabron au 007 lazima kale ka chuma kaonekane ili washikaji wajue umenunuliwa mpya
  • matozi waliitwa magwangwe na maranyingi walikua hawatawazi
  • wakuu wa wilaya waliweza kukutandika bakora mbele ya mkeo
  • ubakaji ilikua tendo la kawaida tuuu lilitwa mande au mtungo
  • tulisafiri kwa juma kwenda mtwara
  • wakazi wa kigoma walijivunia biasha ya homela homela wenyewe wakiita pia bize
  • form 4 alikua msomi na angeweza oa mtoto wa mwenyekiti wa kijiji
  • ma bwana mifugo walitutibu gono pia kwa sindano za ng'ombe na tulipoa
  • tulipanda foleni ili tupate kipande cha sabuni ya ilula
  • chai walikunywa waungwana wa town sis zetu uji kwa asali
pia kulikuwa na biashara ya yomboo
 
kulikua na maneno maarufu kama
kristobe
damdam
mzeemeko
doletupu
komredi
makaburu
 
Watu wa zamani mlipata shida sana. Sijui hata mlikuwa mnatongozaje wakati kulikuwa hakuna simu... Inawezekana pia mlikuwa mnachapiana sana.. Na ndio pengine mkafikia hatua ya kutunga ule msemo kuwa "kuchapiwa ni siri ya ndani"

Wakati ule mkifunga shule unaambiwa likizo kwa bibi, mjomba babu, au baba mkubwa na ilisaidia sana kuweka familia pamoja....hakukuwa na hizi mobile phones hivyo kama ni nyumba au kijiji jirani mtoto unatumwa au kama ni jambo zito inabidi mfunge safari. Watu/familia zilikuwa karibu sana kwani zilikuwa zinaonana uso kwa uso, tofauti na sasa tunapigiana simu na mtu anakuambia yupo salama kumbe ana hali mbaya.....mobile phones zimerahisisha sana mawasiliano na mambo mengine ila imetupunguzia sana kukutana hasa kwa ndugu na majirani. tunakutana kwenye misiba na harusi tu.....vinginevyo ni mwendo wa mobile phones.....nafikiri kutembeleana kulidumisha upendo na mshikamano zaidi...ila sasa hivi tuna excuse za kutosha...tuko busy, foleni za magari, kwenda kwa mtu lazima uweke appointment, budget ya kutembeana haitoshi,n.k!
 
Kipindi Edward Moringe(R I P amen) akiwa Waziri mkuu alipofanya opereshen kwa wahujumu uchumi watu walitupa pesa zao sio leo EPA mnawabembeleza warudishe na Escrow kubeba kwa sandarusi!
Waliohujumu kwa kufungia sukari stoo ili wapandishe bei waliimwaga sukari mtoni.
 
Kipindi Edward Moringe(R I P amen) akiwa Waziri mkuu alipofanya opereshen kwa wahujumu uchumi watu walitupa pesa zao sio leo EPA mnawabembeleza warudishe na Escrow kubeba kwa sandarusi!Waliohujumu kwa kufungia sukari stoo ili wapandishe bei waliimwaga sukari mtoni.
Thats true !! nilikuwa nimedunduliza na kuchanga pesa mwaka mzima zikafika $ 57 !! duuh wakati wa Opereshen hujumu uchumi eti wanyumbani wakanilazimisha nizichome moto !!iliniuma sana !! maana nilijinyima mda mrefu hatimae nikageuza pesa masizi na majivu !!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Zamani tulikuwa tuna hudhuria ma beach party kila wiki ilikuwa buruudaniii sana
 
siku za sikukuu kulikuwa na tamaduni za kupeana chakula hasa pilau, kama mimi ni mkristo na ni krismass lazima pilau ipikwe na niwagawie jirani zangu hasa ambao sio wakristo, na wao vileviile ikifika sikukuu yao wanafanya hivyo hivyo....

Hii hadi kristmass ya mwaka jana nimefanya, na pasaka hii ntafanya. Huwa nanunua kuku nampa anachinja, analeta anapikwa twala, na yeye sikukuu zake hivyo hivyo, so atleast mimi nipo zamani kwa hili..!
 
Weee Mtoto utakuwa umesoma kitabu cha maktaba! Maana hilo shairi tumeliimba miaka ya 80s! Kwa vitabu vyenu vya Ben & Co Ltd hamwezi kuyakuta hayo mashairi!!

Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali
kavimba yote mapaja na kutetemeka mwili
watoto wake wakaja, ili kumtaka hali
wakataka na kauli, iwafae maishani

Kwani hili shairi wamelitoa kwenye mtaala wa sasa?! Maana mimi nilikuwa nalichukulia kama kipimo cha mtu aliyepatia elimu ya msingi Tz.
 
Kwenye sikukuu ya saba saba umesema kweli mkuu, ilikuwa ni sherehe kubwa mkienda huko uwanjani mnakula miwa balaa. Kwenye magari nilikuta STC ndio zinaishilia, ilikuwa tukiona gari yenye TX basi tunajua ni gari ya mzungu
 
Shairi la "SIZITAKI MBICHI HIZI" lilikuwa hivi Mkuu!

Hadithi inayokuja, ni ya sungura sikia,
Hadithi uliyongoja, leo ninakuletea,
Alitoka siku moja, njaa aliposikia,
Njaa aliposikia, Sungura nakuambia

Siku ile akaenda, Porini kutembelea,
Akayaona matunda, mtini yameenea,
Sungura akayapenda, mtini akasogea,
Mtini akasogea, Sungura nakuambia.

Sungura karukaruka, lakini hakufikia,
Matunda hakuyashika, mikononi hakutia,
Hakika alisumbuka, nguvuze zikapungua,
Nguvuze zikapungua, Sungura nakuambia.

Mtazame hapo juu, Sungura amelegea,
Mtazame na miguu, matunda anarukia,
Atafanya sikukuu, matunda akifikia,
Matunda akifikia, Sungura nakuambia.

Karuka tena karuka, matunda akarukia,
Mwisho Wake akachoka, kachoka hata mkia,
Penye mti akatoka, pembeni akasogea,
Pembeni akasogea, Sungura nakuambia.

“Sizitaki mbichi hizi”, Sungura akagumia,
“Naona nafanya kazi, bila faida kujua”,
Yakamtoka machozi, matunda akalilia,
Matunda akalilia, Sungura nakuambia.

Sio kama hakutaka, sasa nakupasulia,
Matunda aliyataka, ndiyo kisa akalia,
Tunajua hakufika, alichoka kurukia,
Alichoka kurukia, Sungura nakuambia.

Hadithi nimemaliza, nimekwisha simulia,
Jambo moja sikiliza, rafiki yangu sikia,
Usikose kujikaza, mazuri kukazania,
Utamshinda Sungura, utapata mbivu hizi.

Asante sana mkuu nimeipenda kwelikwel!
 
-Kuangalia sinema kwenye projector kuuubwa kijijini mida ya jioni hasa zile sinema ya Chack Norris na Rambo na kiingilio ilikuwa shilingi tano hadi kumi

-Wakati Pepe Kalle anatumbuiza pale Diamond Jubilee, kulikuwa hakuna utamaduni wa kukaa kwenye siti kama sasa hivi maana afya zetu hizo zilikuwa safi siyo sasa miili imejaa chips mayai
 
Tulikua tunaudhulia mashindano ya disco lan'gata social hall na harbour's club walikuepo mabingwa wa kucheza style mbalimbali. Mabingwa wetu kama akina savy pops akiwa kijana mdogo kabisa kuchukua ubingwa akitokea mitaa ya keko. Akina Black Moses kinondo, Ngedere Morogoro. Du!! Ilikua hatari natamani siku zingerudi nyuma.

Kokolikoo, Maxi priest, Athumani Digadiga, (na huyu wa juzi Super Faby na Queen Vero)
 
Ahante sana, miaka hiyoooo 80's.......
Kweli ilikuwa raha sana, hata vitabu tulivyokuwa tunasoma vya akina asha na rozi vilikuwa vizuri sana, yuo can't compare kwakweli...... "rafiki ni bora kuliko mwanasesere"

Somo la jiografia lilikuwa poa sana, by that time darasa la nne tu unaijua mikoa yote ya Tanzania, mkoa gani unalima mazao gani n.k sasa hivi sidhani kama watoto wanafundishwa hivi vitu.

Manjagata unakikukmbuka kitabu cha jiandae kumaliza elimu ya msingi, zile atlasi, ndani unakutana na Tanzania- sura ya nchi, yaakisha mambo ya tanzania, inafuata afrika mashariki, then afrika na mwisho dunia, mwanafunzi unaelewa kwa undani tanzania kuna nini, afrika mashariki kuna nini, afrika kuna vitu gani hadi dunia


Shairi la "SIZITAKI MBICHI HIZI" lilikuwa hivi Mkuu!

Hadithi inayokuja, ni ya sungura sikia,
Hadithi uliyongoja, leo ninakuletea,
Alitoka siku moja, njaa aliposikia,
Njaa aliposikia, Sungura nakuambia

Siku ile akaenda, Porini kutembelea,
Akayaona matunda, mtini yameenea,
Sungura akayapenda, mtini akasogea,
Mtini akasogea, Sungura nakuambia.

Sungura karukaruka, lakini hakufikia,
Matunda hakuyashika, mikononi hakutia,
Hakika alisumbuka, nguvuze zikapungua,
Nguvuze zikapungua, Sungura nakuambia.

Mtazame hapo juu, Sungura amelegea,
Mtazame na miguu, matunda anarukia,
Atafanya sikukuu, matunda akifikia,
Matunda akifikia, Sungura nakuambia.

Karuka tena karuka, matunda akarukia,
Mwisho Wake akachoka, kachoka hata mkia,
Penye mti akatoka, pembeni akasogea,
Pembeni akasogea, Sungura nakuambia.

“Sizitaki mbichi hizi”, Sungura akagumia,
“Naona nafanya kazi, bila faida kujua”,
Yakamtoka machozi, matunda akalilia,
Matunda akalilia, Sungura nakuambia.

Sio kama hakutaka, sasa nakupasulia,
Matunda aliyataka, ndiyo kisa akalia,
Tunajua hakufika, alichoka kurukia,
Alichoka kurukia, Sungura nakuambia.

Hadithi nimemaliza, nimekwisha simulia,
Jambo moja sikiliza, rafiki yangu sikia,
Usikose kujikaza, mazuri kukazania,
Utamshinda Sungura, utapata mbivu hizi.
 
Last edited by a moderator:
Zamani sema kulikuwa hakuna ngoma tuu ndio uzuri wake,,ukiugua zako kaswende unapiga mitishamba kesho unadunda kitaa na raizoni.
 
Umeona eeh....

siku hizi sijui watu wanafuturia wapi, nakumbuka tulikuwa tumepanga nyumba ya waislam, tulikuwa tunafuturu mwanzo mwisho utadhani na sisi tumefunga, siku za sikukuu iddi au christmas ilikuwa hakuna ubaguzi mnashirikiana kupika na kula pamoja kama ndugu jamani, haya mamba hayapo tena nowdays, kweli zamani ilikuwa raha


Zamani kweli raha,

Kipindi ikifika Ramadhani watu wanafutari nje na kila mpita njia anaweza kukaa na akala na majirani wote munakua pamoja
 
Back
Top Bottom