Zamani ilikuwa raha

Zamani ilikuwa raha

mambo ya nyonya damu yalituogopesha

Rino lens, Mister T, The Pointman, Timetrax zilibamba

stori za jiwe fatuma zilitunyima raha sisi wenye tv mtaani

Michuano ya kombe la dunia ikifika Tv hutolewa nje ili kila mtu mtaani ajionee
 
Mkuu mi sio wa 90s,nilikuwepo dunian longtym sema 90s kwangu ndio kilikuwa kpndi kizuri kwangu na hasa kwa watu waliozaliwa kuanzia 75s,kwa mtu aliyezaliwa kipndi hcho ujana wake lazma atakuwa amekula kipnd cha miaka ya tisini,mi nafikiri zaman ya mtu inategemea na yeye kazaliwa lini,kwangu zaman yangu ni 90s kipndi ambacho tulikuwa na wanamziki kama Michael Jackson,Whitney,Jodeci,New Edition,Monica na mashindano ya kudensi kila wikend

Umenikumbusha club raha leo show,
Jodeci, akina keith sweat, bozi boziana, chico chicaya na we miss you manelo daaah!!! Nakumbuka wimbo wangu wa kwanza wa kingereza kuukariri ulikuwa all that she wants wa ace of base..
 
Suruali aina ya Tokyo na savico... Suruali za mchele mchele na Bahama shirt
 
Utoki darasani mapumziko hadi ununue embe ya mwalimu
 
Zamani inayosemwa hapa ni ile mwalim anaheshimika kijiji kizima na wanafunzi wanalima shambani kwa mwalim wengine wanachota maji. Mwalim ana kila kitu kazi yake kufundisha tu na wala hakuna twisheni.
Ilikuwa hakuna kupasi wala kufeli bali wenye bahati wenye maksi (marks) za juu ndio wanachaguliwa kwenda sekondari
Mwalimu wakati huo hakuwa na shida ya kuuza embe wala ubuyu
 
Baadhi ya Waalimu wa enzi Nyerere waliteliwa kuwa wakuu wa Wilaya na Mikoa.Au wakurugenzi wa maendeleo.
 
Nakumbuka tulikuwa tunaimba huu wimbo wakati wa kuingia madarasani CHAMA CHAMA KIMETUKOMBOA CHAMA,Umishumta ukifika muda wa kushindanisha kwaya ya kila shule unawaona waalimu wenye redio za tape za kurekodi wanazuchukua na kusimama mbele na kuanza kurekodi.Enzi hizo ikifika saa tisa na dk ishirini unaanza kuwaza kwenda kulima kwenye shamba la shule au kwa mwanakijiji shambani kwake tunakwenda kupalilia shamba lake ili yeye aje kutulimia shamba letu la shule.Hakuna siku ambayo siisahau ktk maisha yangu ya elimu ya msingi siku nilipopewa cheo cha kuwa TIME KEEPER.Nilifurahi sana kwa sababu nilikuwa nimepona na vichapo vya viranja.Pia nakumbuka kuna siku alikuja mtaalamu wa kilimo shuleni kwetu alikuja kutufundisha jinsi ya kutega fuko wale wanaofanana na panya wanaokula mihogo na viazi tuliolielewa vizuri somo hilo tukateuliwa kuwa tunawatega hao fuko kwenye mashamba ya shule na tulikuwa tukiwanasa tunawapeleka kwa mwl wa kilimo ili kuweka rekodi akija bwana shamba shuleni anaonyeshwa takwimu.Dah tulikuwa tunachafuka nguo zetu za shule shauli ya kulala chini wakati wa kutega tukipita unasikia wanafunzi wanasema watega fuko hao.Dah redioni kipindi nilichokuwa nakipenda kilikuwa kinaitwa Harakati saa kumi na nusu. nikiwa natumia karedio kadogo aina ya philips pesa ya kununua betri nilikuwa naipata kwa kutega fuko kwenye mashamba ya wanakijiji waliokuwa wananilipa baada ya kuwategea mashambani mwao.Mh! yaani sasa hivi huwa nikipata breakdown na kausafiri kangu nikichuchuma chini kukakagua uvunguni kumbukumbu zinanirejea za miaka hiyo ya kupiga magoti chini natega fuko.
 
Hhaahhhaa...Kibanga ampiga mkoloni
Mfalme ana masikio marefu kama ya punda
Tola anakula Gizani
Gulioni Katerero
Du...Rosa Mistika

Ha ha ha, Brown ashika tama, Jogoo aliyesema, Safari yenye mikosi...
 
Zamani inayosemwa hapa ni ile mwalim anaheshimika kijiji kizima na wanafunzi wanalima shambani kwa mwalim wengine wanachota maji. Mwalim ana kila kitu kazi yake kufundisha tu na wala hakuna twisheni.
Ilikuwa hakuna kupasi wala kufeli bali wenye bahati wenye maksi (marks) za juu ndio wanachaguliwa kwenda sekondari
Mwalimu wakati huo hakuwa na shida ya kuuza embe wala ubuyu

I miss those times...lol
 
Nakumbuka tulikuwa tunaimba huu wimbo wakati wa kuingia madarasani CHAMA CHAMA KIMETUKOMBOA CHAMA,Umishumta ukifika muda wa kushindanisha kwaya ya kila shule unawaona waalimu wenye redio za tape za kurekodi wanazuchukua na kusimama mbele na kuanza kurekodi.Enzi hizo ikifika saa tisa na dk ishirini unaanza kuwaza kwenda kulima kwenye shamba la shule au kwa mwanakijiji shambani kwake tunakwenda kupalilia shamba lake ili yeye aje kutulimia shamba letu la shule.Hakuna siku ambayo siisahau ktk maisha yangu ya elimu ya msingi siku nilipopewa cheo cha kuwa TIME KEEPER.Nilifurahi sana kwa sababu nilikuwa nimepona na vichapo vya viranja.Pia nakumbuka kuna siku alikuja mtaalamu wa kilimo shuleni kwetu alikuja kutufundisha jinsi ya kutega fuko wale wanaofanana na panya wanaokula mihogo na viazi tuliolielewa vizuri somo hilo tukateuliwa kuwa tunawatega hao fuko kwenye mashamba ya shule na tulikuwa tukiwanasa tunawapeleka kwa mwl wa kilimo ili kuweka rekodi akija bwana shamba shuleni anaonyeshwa takwimu.Dah tulikuwa tunachafuka nguo zetu za shule shauli ya kulala chini wakati wa kutega tukipita unasikia wanafunzi wanasema watega fuko hao.Dah redioni kipindi nilichokuwa nakipenda kilikuwa kinaitwa Harakati saa kumi na nusu. nikiwa natumia karedio kadogo aina ya philips pesa ya kununua betri nilikuwa naipata kwa kutega fuko kwenye mashamba ya wanakijiji waliokuwa wananilipa baada ya kuwategea mashambani mwao.Mh! yaani sasa hivi huwa nikipata breakdown na kausafiri kangu nikichuchuma chini kukakagua uvunguni kumbukumbu zinanirejea za miaka hiyo ya kupiga magoti chini natega fuko.

Mkuu dhule gan umesoma!....km hutaweza ksema ntajie hata mkoa tu
 
Back
Top Bottom