Four years!! Mkuu watu wame-date toka shule ya msingi hadi chuo kikuu na hawaoni ndani. Mchezo wanakuja kupewa siku ya ndoa (of coz hizi ni zile extreme cases lakini zilikuwepo za kutosha tu)
acha kudanganya wasiokuwepo wewe...uliona raha kula unga wa njano kisa tunakwenda kumpiga Iddi Amini!?
Watoto wa siku hizi ndio wanafaidi siku hizi picha uweki kwenye Albamu ni mwendo wa Selfie na kutupia Instagram kwa kuwa salamu ni WhatsApp hatutumiagi tena kalamu yale mambo ya kutuma barua leo inafika baada ya mwezi ww unadhani watu walikuwa wanafurahi kusubiri kutafutia mke wa kuoa na baba yako nani alikuwa anapenda eti ugongi mpama uoe kudadeki siku hizi ukipewa namba ya simu tu ushakubaliwa
#Zitto
Kwenda sekondari ilikuwa ni heshima kwa jamii inayokuzunguka. Wakati wa kwenda shule husindikizwa na kundi la watu huku umesaidiwa sanduku. Tulipanda treni.
Tiketi tulitunza kwani nauli tulirejeshewa baada ya safari. Makonda wa treni (tt) walikuwa ni wahindi.
Mwl.alipohamishwa shule ilipikwa pilau, pia mashairi yaliimbwa.
Picha tulipiga studio tena baada ya kusevu kwa muda mrefu.... Tofauti na siku hizi ''selfie''.
Tulisikiliza RTD, kwa miziki idhaa ya biashara.
Range rover haikuruhusiwa ku paki benki. Peugeot 504 iliaminika ni gari ya wahuni/majambazi.
Namba za serikali ilikuwa stb, stc, std, stg. Za wahisani ilikuwa tx - plate number nyekundu.
Sikukuu ya saba saba ilifana sana kitaifa ilifanyika. Na mikoa mingine ilishiriki pia.
Vitabu madaftari shule za msingi ilikuwa bure. Daftari likijaa unapeleka kwa mwl.wa darasa anakupa jipya
ole wako karatasi zikutwe pungufu, viboko vilitawala mashuleni na nidhamu ilikuwepo pia.
Wanafunzi shule ya msingi baadhi walikuwa wananyoa ndevu.
Itaendelea.
Nondo mla watu, kibanga ampiga mkoloni, brown ashika tama
Mkikutana na mwalimu,..mwalimu anakusalimia ''za saizi baba nusura!
hizi hadithi zilikuwa zina mafunzo makubwa
nimewakumbuka Mr & Mrs Daudi, Baraka na Neema na Neema atakuwa ameolewa sasa
Tulicheza mpira wa makaratasi na shule nzima ilitushangilia kwa nguvu ikiwa pamoja na waalimu wetu.
Halafu asubuhi kabla ya masomo tulikimbia mchakamchaka huku tukiimba nyimbo nyingi kama vile:
Idd Amini akifa,
mimi siwezi kulia,
Nitamtupa Kagera,
awe chakula cha mamba.
HIZO ZOTE NI HEKIMA NA BUSARA ZA BABA WA TAIFA,ati leo tuna madini,gesi na utalii..tunalipia Matibabu na elimu na maisha yamekua Kero kama sio nyoka mwenye makengeza basi utaomba ardhi ipasuke uingie!ndio maana nikasema tunatakiwa kama nchi si kusherehekea bali KUSIKITIKIA MIAKA 50 YA UHURU,tumuenzi Baba Nyerere!!
Udini haukuwepo, Watanzania walipendana na kusaidiana kwa hali na mali bila kujali huyu muislam au mkristo. Hakukuwepo na mafisadi kama ilivyo sasa. Viongozi walikuwa wanaheshimika kwa sababu badala ya kukwapua kwa ajili ya matumbo yao wengi wao walikuwa wanawatumikia Watanzania kwa faida yao na Tanzania. Wauza unga walikuwa hawapo tulikuwa tunasikia tu kwenye taarifa ya habari kuhusu wauza unga wa nchi za nje ambazo zote zilikuwa ni nje ya Afrika. Ikulu iliheshimika na Watanzania sio kama ilivyo sasa imegeuzwa kuwa danguro la mafisadi wanagawana pesa za umma walizokwapua ndani ya Ikulu.
Hii ya juzi hapo 90 huyu mleta mada kwa namna alivyoandika yeye ni miaka ya mwisho ya 80 kurudi nyuma kwa Mwl Nyerere. Kipindi hicho hata private schools sidhani kama zilikuwepo na mara nyingi ilikuwa ukifeli ndio basi tena labda ukarudie darasa sehemu nyingine.