Zamani ilikuwa raha

Zamani ilikuwa raha

Zamani ilikuwa raha sana! Nakumbuka tulikuwa tunatoka uswazi na kwenda kuangalia sinema bubu pale drive in.....
 
-Matibabu ilikuwa bure. Hospitali za binafsi hazikuwepo labda za misheni.
-Ukivaa chupi ilikuwa ni dili kubwa!
-Hakukuwa na skini taiti
-Viatu ilikuwa tunanunua Bora
-Nyumba 10 alikuwa anaheshimika kama hakimu. Ukigombana na mkeo anakwenda kushitaki na kulala kwa mjumbe
-Ukimwi ulikuwa hakuna zaidi ya kisonono na kaswende
-Wasichana wa kazi walikuwa bwerere siku hizi ni shida!
-Hakukuwa na magril kwenye milango na madirisha
-Nyerere alikuwa kama Mungu
-Kawawa alikuwa alionekana kama kichekesho kwa stori za "Kawawa funika kikombe"
-Tulifanywe tuamini kuwa Kambona ni adui wa nchi yetu na nyimbo tuliimba
-Wakati ule wanafunzi kwenda kufanya kazi za mwalimu nyumbani kwake ilikuwa ni heshima kubwa, sasa hivi ni kesi
-Mashairi ya "Karudi baba mmoja" na "Sizitaki mbichi hizi" yalikuwa kichwani kwa kila mwanafunzi
-Jioni zilikuwa ni nyakati za kupiga hadithi na vitendawili au michezo ya kujificha. Siku hizi ni kuangalia TV
Nitaendelea......
yote tisa umesahau kuoa ilikuwa ni kuchagua bega yaani unamvizia binti ukimbeba tu kwako akilala kesho yake wazazi wa mvulana wanakwenda kujitambulisha ndoa tayari.
- ukilala na mvulana tayari ameshakua mmeo hata kama humtaki
-siku za gulio ndo siku za kutoka yaani ukienda gulioni wewe ni mkali ile mbaya
-zawadi kubwa mama akitoka sokoni ni mandazi
-baba alimiliki uchumi wote wa familia hata kama mama ndo kalima
-jamani kufagia samadi kila sbh kbla ya shule, na kulima bustani za mboga ni kawaida sanaaa
-siku mwl anakuja kutembelea mkoa wamnafunzi mnajipanga barabarani na kuimba nyimbo za kumpongeza
-mwenge wa uhuru ukija wilayani ni balaa mtaimba mashairi na kwaya ile mbaya
-shulen kulikuwa na siku ya mashundano ya kuimba kwaya katika wilaya na mshindi huenda mkoa hadi taifa
-umishumta ilikuwa balaa skati fupiii za netball lol!
ngoja nipike narudi..................
 
Kule kijijini tulikuwa tunajua uki fail darasa la saba ndo mwisho wako wa kusoma sikuwahi kusikia kuhusu shule binafsi.
Matokeo ya darasa la 7 tulifaulu wanafunzi wa 3 kati ya 85 kwenda form 1.tulikuwa kama miungu watu kijijini tulinyoshewa kidole kila sehemu tuliopita.
 
Mkuu shairi la karudi baba mmoja nililiimba nikiwa darasa la 4 mwaka 2000 ila shairi la sizitaki hizi mbichi sikubahatika emu weka mistari yake!
Shairi la "SIZITAKI MBICHI HIZI" lilikuwa hivi Mkuu!

Hadithi inayokuja, ni ya sungura sikia,
Hadithi uliyongoja, leo ninakuletea,
Alitoka siku moja, njaa aliposikia,
Njaa aliposikia, Sungura nakuambia

Siku ile akaenda, Porini kutembelea,
Akayaona matunda, mtini yameenea,
Sungura akayapenda, mtini akasogea,
Mtini akasogea, Sungura nakuambia.

Sungura karukaruka, lakini hakufikia,
Matunda hakuyashika, mikononi hakutia,
Hakika alisumbuka, nguvuze zikapungua,
Nguvuze zikapungua, Sungura nakuambia.

Mtazame hapo juu, Sungura amelegea,
Mtazame na miguu, matunda anarukia,
Atafanya sikukuu, matunda akifikia,
Matunda akifikia, Sungura nakuambia.

Karuka tena karuka, matunda akarukia,
Mwisho Wake akachoka, kachoka hata mkia,
Penye mti akatoka, pembeni akasogea,
Pembeni akasogea, Sungura nakuambia.

“Sizitaki mbichi hizi”, Sungura akagumia,
“Naona nafanya kazi, bila faida kujua”,
Yakamtoka machozi, matunda akalilia,
Matunda akalilia, Sungura nakuambia.

Sio kama hakutaka, sasa nakupasulia,
Matunda aliyataka, ndiyo kisa akalia,
Tunajua hakufika, alichoka kurukia,
Alichoka kurukia, Sungura nakuambia.

Hadithi nimemaliza, nimekwisha simulia,
Jambo moja sikiliza, rafiki yangu sikia,
Usikose kujikaza, mazuri kukazania,
Utamshinda Sungura, utapata mbivu hizi.
 
Wanaposema raha yaani level of happyness among the people ilikuwa juu yaani pamoja na yote hayo watu walikuwa na furaha na wanaheshimiana na wanaishi kama ndugu

na baada ya miaka 20 sidhani kama dunia itakua salama tena kuishi........zaman watu walikua happy san
 
yote tisa umesahau kuoa ilikuwa ni kuchagua bega yaani unamvizia binti ukimbeba tu kwako akilala kesho yake wazazi wa mvulana wanakwenda kujitambulisha ndoa tayari.
- ukilala na mvulana tayari ameshakua mmeo hata kama humtaki
-siku za gulio ndo siku za kutoka yaani ukienda gulioni wewe ni mkali ile mbaya
-zawadi kubwa mama akitoka sokoni ni mandazi
-baba alimiliki uchumi wote wa familia hata kama mama ndo kalima
-jamani kufagia samadi kila sbh kbla ya shule, na kulima bustani za mboga ni kawaida sanaaa
-siku mwl anakuja kutembelea mkoa wamnafunzi mnajipanga barabarani na kuimba nyimbo za kumpongeza
-mwenge wa uhuru ukija wilayani ni balaa mtaimba mashairi na kwaya ile mbaya
-shulen kulikuwa na siku ya mashundano ya kuimba kwaya katika wilaya na mshindi huenda mkoa hadi taifa
-umishumta ilikuwa balaa skati fupiii za netball lol!
ngoja nipike narudi..................

dada gfsonwin habari za masiku umehadimika?
 
chakachaka alipokuja dar mwaka 90 kiingilio laki moja pale makondeko nje ya jiji siku hizi diamond akiweka kiingilio elfu 50 mlimani city inakuwa matangazo kila kona

ha ha haa daah....huyu diamond huyu!!
 
Mkuu unataka zaman yangu iwe miaka gan?labda we ni wa 60 lakn kwa wale waliozaliwa miaka ya 75 adi 80s wengi wao wana miaka 30 adi 45 na wengi wao ukiwauliza kipndi gan kilikuwa kizuri atakwambia 90s,kipindi cha salamander na magoti,ukitaka bolingo unaenda Tazara

Nimekuelewa Mkuu! Ni kweli eti hata katoto ka mwaka 2000 ukikauliza zamani ya kenyewe katasema mwaka 2000 ha ha ha ha haaaa!! Frank bwana eti zamani yake 90s! Ila tuwe waungwana tukisema zamani mtuachie Wa 70s angalau tuongee, nyie Wa 90s msubiri ikifika 2030 ndo mtaulizana zamani yenu!!
 
RTD ndo ilikuwa mambo yote, Sauti ya Tanzania zanzibar,external service AM, hakukuwa na FM, DW,BBC tulipata Short waves!
 
Zamani tulisoma masomo LA Sayansi Kimu na Siasa, vijana wa leo ukiwaambia Sayansi Kimu watakuuliza hiyo ndio nini?

Vv
 
Jangwani sec partners wao Azania sec, Zanaki Sec vs Tambaza, ngoja itokee mechi ya basketball pale viwanja vya Zanaki kati ya Azania vs Tambaza ndio utaona raha yake.....kule boarding mitaa ya kaskazini Weruweru vs Ilboru, Umbwe or Old moshi, Kiraeni vs Killimanjaro boys/old moshi, Kibosho Girls vs Ilboru. Sekondari za Lyamungo, kibohehe na Kolila ilikuwa shida kupata parters kwa sababu ya fujo zao! Mlikuwa mkialikwa na Moshi Technical mnajua mnaenda kukutana na wakulima, hata kucheza walikuwa wanacheza ngoma za kienyeji badala ya muziki......wananuka vikwapa hasa.....Nakumbuka kuna siku tulialikwa Old moshi sec disco liishe saa sita usiku nasi tupande basi turudi kwetu, lakini mijamaa ikamnunulia bia dereva ikamnywesha akalewa halafu wakaiba funguo ya gari.....hatukuondoka mpaka asubuhi saa kumi na mbili ndio tunafika kwetu....usiulize yaliyotukuta!!!!!!
 
acha kudanganya wasiokuwepo wewe...uliona raha kula unga wa njano kisa tunakwenda kumpiga Iddi Amini!?
Watoto wa siku hizi ndio wanafaidi siku hizi picha uweki kwenye Albamu ni mwendo wa Selfie na kutupia Instagram kwa kuwa salamu ni WhatsApp hatutumiagi tena kalamu yale mambo ya kutuma barua leo inafika baada ya mwezi ww unadhani watu walikuwa wanafurahi kusubiri kutafutia mke wa kuoa na baba yako nani alikuwa anapenda eti ugongi mpama uoe kudadeki siku hizi ukipewa namba ya simu tu ushakubaliwa

#Zitto
 
Nimekuelewa Mkuu! Ni kweli eti hata katoto ka mwaka 2000 ukikauliza zamani ya kenyewe katasema mwaka 2000 ha ha ha ha haaaa!! Frank bwana eti zamani yake 90s! Ila tuwe waungwana tukisema zamani mtuachie Wa 70s angalau tuongee, nyie Wa 90s msubiri ikifika 2030 ndo mtaulizana zamani yenu!!

Mkuu mi sio wa 90s,nilikuwepo dunian longtym sema 90s kwangu ndio kilikuwa kpndi kizuri kwangu na hasa kwa watu waliozaliwa kuanzia 75s,kwa mtu aliyezaliwa kipndi hcho ujana wake lazma atakuwa amekula kipnd cha miaka ya tisini,mi nafikiri zaman ya mtu inategemea na yeye kazaliwa lini,kwangu zaman yangu ni 90s kipndi ambacho tulikuwa na wanamziki kama Michael Jackson,Whitney,Jodeci,New Edition,Monica na mashindano ya kudensi kila wikend
 
Back
Top Bottom