Zamani ilikuwa raha

Zamani ilikuwa raha

Suruali za jeans hazikuwepo kulikuwa na suruali za codrai na surual za mabuga luuu, ndo zilikuwa fashion.

Mkuu kulikuwa na products za Levi's,Lee & Wrangler
Bugaluu sawa ila kwa nyongeza kulikuwa na Bell bottom Tina -buu na Chupa! viatu mkuki moyoni,Raise on,platform na Raba mtoni.
 
kulikuwa na vijarida vya katuni maarufu "Comic" kulikuwa na Beano,Beezer,Toppers bila kusahau Tintin vyote vilikuwa vinachapishwa Ulaya.
 
kama hujasoma Novels za James Hadley Chase tulikuwa hatukuelewi.
 
Vijana mpooo....tupoooo ...tupo kabisa

jeuri ya chama...chini ya umoja wa vijana

yebaaa .....waaaa

………………………………


mwenge huooo..mwenge...mbio...mbio

mwenge tunaukimbiza mbio..mbio

mpaka makao makuu mbio...mbio

ZAMANI KULIKUWA NA KAUZALENDO TOFAUTI NA SASA,

TULIKUWA TUNAJIPANGA BARABARANI KUMSUBIRI RAIS AKIPITA.

ILA SIKU HIZI WATU HAWANA UJINGA HUO.

Ongezea na hii:
..sisi vijana tuko imara, tunaahidi mbele ya chama, tutakuwa mashahidi wa chama na serikaliii...

kiitikio: ..tuko imara kulitumikia taifa, daima mbele haturudi nyuma sisi vijanaaa.....

................................................................

Kwenye somo la siasa mnalazimishwa kukariri kanuni za TANU, vitabu vya kufundishia siasa ni Mwongozo wa TANU na katiba ya ccm.

Uhamisho wa shule lazima upitishwe na kiongozi wa shina au tawi la ccm.
 
Na ukiwa mwajiriwa serkalini ni marufuku kufanya biashara leo maduka makubwa ya dawa ni yamadoctor TAFAKARI
 
Mnaikumbuka pool side kilimanjaro hotel
Kilimanjaro Hotel umenikumbusha zamani sana wakati bado nipo kinda tulikuwa tunapelekwa kuangalia mashindano ya magari Kilimanjaro Hotel ndio wanapomalizia mashindano yao kuna dereva mmoja anaitwa DUDU(Singasinga)
alikuwa anatisha sana akiingia yeye watu DUDU huyo. Kwanza lazima achimbe sana mashine lazima uisikie kisha gari imejaa(imetapakaa tope) tele.

Jamani kuna mtu yeyote mwenye data za DUDU
 
Ahante sana, miaka hiyoooo 80's.......
Kweli ilikuwa raha sana, hata vitabu tulivyokuwa tunasoma vya akina asha na rozi vilikuwa vizuri sana, yuo can't compare kwakweli...... "rafiki ni bora kuliko mwanasesere"

Somo la jiografia lilikuwa poa sana, by that time darasa la nne tu unaijua mikoa yote ya Tanzania, mkoa gani unalima mazao gani n.k sasa hivi sidhani kama watoto wanafundishwa hivi vitu.

Manjagata unakikukmbuka kitabu cha jiandae kumaliza elimu ya msingi, zile atlasi, ndani unakutana na Tanzania- sura ya nchi, yaakisha mambo ya tanzania, inafuata afrika mashariki, then afrika na mwisho dunia, mwanafunzi unaelewa kwa undani tanzania kuna nini, afrika mashariki kuna nini, afrika kuna vitu gani hadi dunia

Kwenye atlas umenikumbusha kitambo kweli kuna mchezo wa kutafuta miji tulikuwa tunacheza 'mtu anataja mji/sehemu wengine mnatafuta.'
 
Last edited by a moderator:
Kumbe mi mdogo sana haya yote hata siyaelewi.
Miaka ya 90 ndo tumeingia hapa Nyerere tumemjua alipokufa
 
Tulivaa skafu za bendera ya taifa na shati la kijani na suruali nyeusi na kofia nyeusi na mfano wa silaha na raba nyeusi siku hiyo nyerere anakuja kuazimisha kitu sabasaba au afla yoyote au kaja Adoud Jumbe!leo ni vijana CCM agh!
 
Nakumbuka KAMATA walikuwa na hotel zao katika kila mkoa yaani gari likiwaharibikia tu unaenda zako kulala huko, na huduma ilikuwa ni heavy kweli kweli...
 
Ukisafiri mwanafunzi unapewa mikate na juisi,mkikuta train limepita mnaenda kupata mlo bure bwalo la jeshi,ukitaka kupanda ndege kama wazazi wako wana chembe ya ushua ,tiketi ilikuwa nusu nauli,ndege nauli TZS 50000,mwanafunzi TZS 25000,au pia unaweza vizia kupanda ''Buffalo''(ndege za mizigo za jeshi),game likikubaliunapanda ile ya maafisa ya watu 45 Fokker,wengine kwa mara ya kwanza kupaa angani ilikuwa ni ndege za kijeshi,mwisho shuleni kulikuwa hakuna mambo ya mapenzi wala kuwa na simu,ukiwa na shida unasubiri siku ya jumapili kwenda kupiga reverse call posta.Godoro,Kitanda,muscan,kamata(bakuli kubwa nzito ,kama zile za wafungwa magereza ,ilikuwa ni bakuli,sahani,sufuria kazi zote ilikuwa inafanya nayo unapata buure ).
 
Kwenye atlas umenikumbusha kitambo kweli kuna mchezo wa kutafuta miji tulikuwa tunacheza 'mtu anataja mji/sehemu wengine mnatafuta.'

Yaani miaka hiyo kwa kweli ilikuwa raha! Walimu walikuwa na mbinu za ufundishaji na sisi wanafunzi nao tulikuwa na mbinu zetu za kuelewa mambo! Darasa la sita unakuwa unajua nchi nyingi na miji mikuu kwa kila nchi! Pia unakuwa unawafahamu marais wote Wa Africa! Hiyo ya kutafuta miji ilikuwa kiboko, naona enzi hizo tuliifanya Tanzania nzima!
 
Ahante sana, miaka hiyoooo 80's.......
Kweli ilikuwa raha sana, hata vitabu tulivyokuwa tunasoma vya akina asha na rozi vilikuwa vizuri sana, yuo can't compare kwakweli...... "rafiki ni bora kuliko mwanasesere"

Somo la jiografia lilikuwa poa sana, by that time darasa la nne tu unaijua mikoa yote ya Tanzania, mkoa gani unalima mazao gani n.k sasa hivi sidhani kama watoto wanafundishwa hivi vitu.

Manjagata unakikukmbuka kitabu cha jiandae kumaliza elimu ya msingi, zile atlasi, ndani unakutana na Tanzania- sura ya nchi, yaakisha mambo ya tanzania, inafuata afrika mashariki, then afrika na mwisho dunia, mwanafunzi unaelewa kwa undani tanzania kuna nini, afrika mashariki kuna nini, afrika kuna vitu gani hadi dunia
ram usinikumbushe kabisa hizo enzi ilikuwa raha jamani! Vita tu ndo ilituharibia mambo kiasi kwamba maisha yakayumba, kabla ya hapo ilikuwa mteremko sana! Jiandae kumaliza ELIMU ya Msingi ilikuwa na maswali ya masomo yote! Ila wakuu darasa la kwanza miaka hiyo nilikuwa kilaza kweli, basi siku moja mwalimu akawa ameandika ubaoni "HILI NI CHANUO" na chanuo limechorwa hapo sasa ikawa ukitajwa unasoma hiyo sentensi. Ikafika zamu yangu bwana sasa kwa vile Mimi nilikuwa sijui kusoma, nikawa nimekariri, lakini katika kukariri kwangu nikawa nimejichanganya nikaongeza neno la kwangu nikasoma "CHANUO HILI HAPA" badala ya "HILI NI CHANUO" Weeeee nilioga viboko kama kibaka! Tangu siku hiyo haki ya nani nilikuwa moto chini ile mbaya!!
 
Last edited by a moderator:
-Matibabu ilikuwa bure. Hospitali za binafsi hazikuwepo labda za misheni.
-Ukivaa chupi ilikuwa ni dili kubwa!
-Hakukuwa na skini taiti
-Viatu ilikuwa tunanunua Bora
-Nyumba 10 alikuwa anaheshimika kama hakimu. Ukigombana na mkeo anakwenda kushitaki na kulala kwa mjumbe
-Ukimwi ulikuwa hakuna zaidi ya kisonono na kaswende
-Wasichana wa kazi walikuwa bwerere siku hizi ni shida!
-Hakukuwa na magril kwenye milango na madirisha
-Nyerere alikuwa kama Mungu
-Kawawa alikuwa alionekana kama kichekesho kwa stori za "Kawawa funika kikombe"
-Tulifanywe tuamini kuwa Kambona ni adui wa nchi yetu na nyimbo tuliimba
-Wakati ule wanafunzi kwenda kufanya kazi za mwalimu nyumbani kwake ilikuwa ni heshima kubwa, sasa hivi ni kesi
-Mashairi ya "Karudi baba mmoja" na "Sizitaki mbichi hizi" yalikuwa kichwani kwa kila mwanafunzi
-Jioni zilikuwa ni nyakati za kupiga hadithi na vitendawili au michezo ya kujificha. Siku hizi ni kuangalia TV
Nitaendelea......
Wajanja wa mjini ilikuwa lazima ukariri zile aya za kitemi za Umsolopagaazi
 
Nikitazama milima ya kwetu enhe machozi yanitoka kwa uchungu na mawazo'tulitoka wawili ninarudi peke yangu baba na mm wa
 
Zaman wale wa born town kucheki movie Avaron,Empress,New Chox au Drive Inn,wale wapenzi wa movie za kihindi Cameo ndio ilikuwa mpango mzima,kabla ya movie mangoma ya wanyamwezi yalikuwa yanapolomoshwa,wanyamwez kama wakina Billy Ocean,Cool n the Gang wengineo ndio ilikuwa stata kabla ya movie kuanza,da!miaka ile ilikuwa bomba kuwai kutokea katika maisha yangu na nina uhakika kwa wale vijana wa 90s na waliopitia viwanja vile,watakuwa wanamiss kipndi kile,da!kwa bahati mbaya vyote vimekufa.
Sunday boogie pale Princess kila jpili lilkitumbuizwa na Safari Trippers wakiwa na Marijani Rajabu.Gateways palikuwa na The Sunburst.
 
Back
Top Bottom