Zamani ilikuwa raha

Zamani ilikuwa raha

karudi baba mmoja toka safari ya mbali
kavimba yote mapaja na kutetemeka mwili
watoto wake wakaja ili kumtaka hali
wakata na kauli iwafae maishani
.....................................................
Roho naona yashindwa kifo kibenikabili
.........................................................
Kama mataka mali mtayapata shambani

Mkuu shairi la karudi baba mmoja nililiimba nikiwa darasa la 4 mwaka 2000 ila shairi la sizitaki hizi mbichi sikubahatika emu weka mistari yake!
 
Umenichekesha sana mkuu na kunikumbusha mbali. Unakumbuka madaftari hayo juu yalikuwa na nembo ya Taifa (Bibi na Bwana)? Nyuma yake kulikuwa na metric conversions pamoja na Table ya kuzidisha kuanzia table ya kwanza hadi kumi?
 
Nyuma ya hapo ilikuwa kama tuko mbinguni...magari ya serikali yakiwa na namba GT,zimamoto na redcross tuliwaita wanyonya damu au chinjachinja,tulipewa uji wa njano na maziwa kutoka USA,tulipewa tanga shoes bure,kulikuwepo shule za wazazi zikiitwa TAPA,kulikuwa na PWD ..public works dapartment..school inspectors,enzi za kilimo cha kufa na kupona Mzee Kawawa aliamrisha viwanja vya Agakhan vilimwe lakini mwalimu akabadilsha uamuzi kwa njia za kibisara...
 
Kumbe zamani hamkuwa na raha yeyote...., uzuri ni kwamba, baada ya miaka 20 leo pia itaitwa zamani.
 
Mmhh those were good days when life style was contrary to the current one..you could use centi and shilling to buy all the basic needs and still get an extra money ...
Those were the days when dating someone's daughter for Four years and yet you couldn't get sex...ha ha haa
 
siku za sikukuu kulikuwa na tamaduni za kupeana chakula hasa pilau, kama mimi ni mkristo na ni krismass lazima pilau ipikwe na niwagawie jirani zangu hasa ambao sio wakristo, na wao vileviile ikifika sikukuu yao wanafanya hivyo hivyo....

yeh umenikumbusha mandazi ya idd aisee ilikuwa tunaletewa sufuria nzima
 
chakachaka alipokuja dar mwaka 90 kiingilio laki moja pale makondeko nje ya jiji siku hizi diamond akiweka kiingilio elfu 50 mlimani city inakuwa matangazo kila kona
 
-Matibabu ilikuwa bure. Hospitali za binafsi hazikuwepo labda za misheni.
-Ukivaa chupi ilikuwa ni dili kubwa!
-Hakukuwa na skini taiti
-Viatu ilikuwa tunanunua Bora
-Nyumba 10 alikuwa anaheshimika kama hakimu. Ukigombana na mkeo anakwenda kushitaki na kulala kwa mjumbe
-Ukimwi ulikuwa hakuna zaidi ya kisonono na kaswende
-Wasichana wa kazi walikuwa bwerere siku hizi ni shida!
-Hakukuwa na magril kwenye milango na madirisha
-Nyerere alikuwa kama Mungu
-Kawawa alikuwa alionekana kama kichekesho kwa stori za "Kawawa funika kikombe"
-Tulifanywe tuamini kuwa Kambona ni adui wa nchi yetu na nyimbo tuliimba
-Wakati ule wanafunzi kwenda kufanya kazi za mwalimu nyumbani kwake ilikuwa ni heshima kubwa, sasa hivi ni kesi
-Mashairi ya "Karudi baba mmoja" na "Sizitaki mbichi hizi" yalikuwa kichwani kwa kila mwanafunzi
-Jioni zilikuwa ni nyakati za kupiga hadithi na vitendawili au michezo ya kujificha. Siku hizi ni kuangalia TV
Nitaendelea......

Hapo kwenye Red panahitaji ufafanuzi ile wanetu waelewe vyema by the way nitaongeza hapa;

  • Kuhamishiwa Mtwara au Sumbawanga kwa mfanyakzi ilikua laana tosha
  • Tulitishwa kupelekwa Mafya (kisiwani)
  • Ukivaa chumpi mpya hasa za Zabron au 007 lazima kale ka chuma kaonekane ili washikaji wajue umenunuliwa mpya
  • Matozi waliitwa magwangwe na maranyingi walikua hawatawazi
  • Wakuu wa wilaya waliweza kukutandika bakora mbele ya mkeo
  • Ubakaji ilikua tendo la kawaida tuuu lilitwa Mande au mtungo
  • Tulisafiri kwa juma kwenda Mtwara
  • Wakazi wa Kigoma walijivunia biasha ya homela homela wenyewe wakiita pia BIZE
  • Form 4 alikua msomi na angeweza oa mtoto wa mwenyekiti wa kijiji
  • Ma bwana mifugo walitutibu GONO pia kwa sindano za ng'ombe na tulipoa
  • Tulipanda foleni ili tupate kipande cha sabuni ya Ilula
  • Chai walikunywa waungwana wa town sis zetu uji kwa asali
 
Kumbe zamani hamkuwa na raha yeyote...., uzuri ni kwamba, baada ya miaka 20 leo pia itaitwa zamani.
Wanaposema raha yaani level of happyness among the people ilikuwa juu yaani pamoja na yote hayo watu walikuwa na furaha na wanaheshimiana na wanaishi kama ndugu
 
Zaman wale wa born town kucheki movie Avaron,Empress,New Chox au Drive Inn,wale wapenzi wa movie za kihindi Cameo ndio ilikuwa mpango mzima,kabla ya movie mangoma ya wanyamwezi yalikuwa yanapolomoshwa,wanyamwez kama wakina Billy Ocean,Cool n the Gang wengineo ndio ilikuwa stata kabla ya movie kuanza,da!miaka ile ilikuwa bomba kuwai kutokea katika maisha yangu na nina uhakika kwa wale vijana wa 90s na waliopitia viwanja vile,watakuwa wanamiss kipndi kile,da!kwa bahati mbaya vyote vimekufa.

Aaaaah! Yaani 90s ndo zamani yako hiyo Mkuu?
 
-Matibabu ilikuwa bure. Hospitali za binafsi hazikuwepo labda za misheni.
-Ukivaa chupi ilikuwa ni dili kubwa!
-Hakukuwa na skini taiti
-Viatu ilikuwa tunanunua Bora
-Nyumba 10 alikuwa anaheshimika kama hakimu. Ukigombana na mkeo anakwenda kushitaki na kulala kwa mjumbe
-Ukimwi ulikuwa hakuna zaidi ya kisonono na kaswende
-Wasichana wa kazi walikuwa bwerere siku hizi ni shida!
-Hakukuwa na magril kwenye milango na madirisha
-Nyerere alikuwa kama Mungu
-Kawawa alikuwa alionekana kama kichekesho kwa stori za "Kawawa funika kikombe"
-Tulifanywe tuamini kuwa Kambona ni adui wa nchi yetu na nyimbo tuliimba
-Wakati ule wanafunzi kwenda kufanya kazi za mwalimu nyumbani kwake ilikuwa ni heshima kubwa, sasa hivi ni kesi
-Mashairi ya "Karudi baba mmoja" na "Sizitaki mbichi hizi" yalikuwa kichwani kwa kila mwanafunzi
-Jioni zilikuwa ni nyakati za kupiga hadithi na vitendawili au michezo ya kujificha. Siku hizi ni kuangalia TV
Nitaendelea......
Shule ilikuwa ukipata Division 4 wewe ni kilaza na division 0 ndio zilikuwa chache kuliko division zote ikifuatiwa na Division one
 
Nakumbuka laba za njano,zilikuwa na lebo ya DH,watu walisema Dingi Hana Uwezo,nakumbuka kunyoa nywele kama Shaba Lunx (mwana mziki wa Laga)
 
Mkuu shairi la karudi baba mmoja nililiimba nikiwa darasa la 4 mwaka 2000 ila shairi la sizitaki hizi mbichi sikubahatika emu weka mistari yake!

Weee Mtoto utakuwa umesoma kitabu cha maktaba! Maana hilo shairi tumeliimba miaka ya 80s! Kwa vitabu vyenu vya Ben & Co Ltd hamwezi kuyakuta hayo mashairi!!

Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali
kavimba yote mapaja na kutetemeka mwili
watoto wake wakaja, ili kumtaka hali
wakataka na kauli, iwafae maishani
 
Back
Top Bottom