Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
- Thread starter
- #101
Vocha za mil. 330 zimeibwa
Imeandikwa na Fadhili Abdallah, Kigoma; Tarehe: 24th January 2011
POLISI mkoani Kigoma wamemkamata Ofisa Kilimo wa Wilaya Kasulu, Benard Kazaura kwa upotevu wa vocha za pembejeo za ruzuku zenye thamani ya Sh milioni 330 na watu wengine wanne kwa kukutwa na noti bandia.
Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma, George Mayunga alisema juzi kuwa Kazaura na wenzake wanatuhumiwa kuhusika katika wizi wa vocha za ruzuku zenye thamani ya Sh milioni 330 zilizokuwa kwenye gari walilokuwa wakisafiria.
Mbali na ofisa huyo, wengine waliokamatwa kwa tuhuma hizo ni dereva wa Halmashauri ya Kasulu, Dauson Alfred na askari Polisi wawili, Sajenti Kididu na PC Jacob waliokuwa wakisindikiza gari lililokuwa na vocha hizo.
Kamanda huyo alisema kuwa watuhumiwa hao, walikuwa wakisafirisha vocha hizo kutoka Dar es Salaam kwenda Kasulu mkoani Kigoma, na waligundua upotevu wa sanduku moja la vocha hizo wakiwa mkoani Dodoma.
"Watuhumiwa wote mara baada ya kuanza safari kutoka Dar es Salaam walifika Dodoma na kuamua kulala, lakini asubuhi wakati wakiingia kwenye gari kwa ajili ya kuendelea na safari, dereva aligundua moja kati ya maboksi mawili yaliyokuwa na vocha halipo," alisema Kamanda Mayunga.
Alifafanua kuwa baada ya watuhumiwa kugundua upotevu huo, waliamua kutoa taarifa Polisi Dodoma na kuendelea na safari na baada ya kufika Kasulu, walikamatwa kwa tuhuma hizo.
Watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi na kwa hao askari polisi hatua za kinidhamu za jeshi hilo zinaendelea kabla ya kufikishwa mahakamani.
Wakati huo huo, wakazi wawili wa Mwanga mjini Kigoma, Mengi Rajab na Taus Said wamekamatwa mjini Kibondo na noti bandia za Sh elfu kumi zenye thamani ya Sh 960,000 wakati wakitaka kununua bidhaa katika duka moja mjini humo.
Kamanda Mayunga alisema watu hao walifika katika duka la Erick Jacob kutaka kununua bidhaa mbalimbali ambapo baada ya kukusanya walichohitaji, walitoa fedha ambazo zilitiliwa shaka na muuzaji ambaye aliwataarifu polisi ambao walifika na kuwatia mbaroni watuhumiwa.
Mkazi mwingine wa mjini Kigoma Zarina Hamisi amekamatwa na noti bandia zenye thamani ya Sh 220,000 wakati akitaka kununua mafuta ya mawese kwa wakulima.