Zaidi ya bilioni 25 zatafunwa; Watendaji waanza kuwajibishwa!

Labda unieleweshe
Unaongelea muundo ama mfumo?

Kwanza si kweli wabunge wote wanafadhiliwa na mfumo kuupata ubunge, na mara nyingi wanaofadhiliwa ndo hao baadae unawaona ktk nyadhifa maana wanakuwa wameshajipanga tangu mwanzo.

Nauhakika hakuna mfumo uliomweka Magufuri kuupata ubunge wala mfumo uliomweka seleli. Sasa mfumo unaoongea hauko bayana unaongelea nini.? wewe vipi hiyo chadema ni mfano mbona waja juu.teh teh teh teh huo mfano wa chadema ndo mfumo huo.


Mfumo/system kwa mujibu wa encarta;
  1. complex whole formed from related parts: a combination of related parts organized into a complex whole
  2. set of principles: a scheme of ideas or principles by which something is organized
  3. way of proceeding: a method or set of procedures for achieving something
Angalizo:Nilichokuwa nikijaribu kukuelewesha kinaangukia kwenye point namba 3 ambayo ni way of proceeding;Kabla ya uchaguzi wabunge hawakusanyi pesa nk?
Vitu vingine vyepesi hadi utafuniwe na hapo hapo unagangamala ukiwa hata huelewi....Eti hakuna mfumo uliowaweka Magufuli wala Seleli,are you kidding?Pia Inawezekana hata hayo uliyoyasema kuhusu muundo wa uongozi yakawa pia ni part ya mfumo,ukitizama kwa makini unaweza ona namba 1 na 2 zinaweza kuwa applicable,umeelewa?
 
Mfumo/system kwa mujibu wa encarta;
  1. complex whole formed from related parts: a combination of related parts organized into a complex whole
  2. set of principles: a scheme of ideas or principles by which something is organized
  3. way of proceeding: a method or set of procedures for achieving something
Angalizo:Nilichokuwa nikijaribu kukuelewesha kinaangukia kwenye point namba 3 ambayo ni way of proceeding;Kabla ya uchaguzi wabunge hawakusanyi pesa nk?
Vitu vingine vyepesi hadi utafuniwe na hapo hapo unagangamala ukiwa hata huelewi....Eti hakuna mfumo uliowaweka Magufuli wala Seleli,are you kidding?Pia Inawezekana hata hayo uliyoyasema kuhusu muundo wa uongozi yakawa pia ni part ya mfumo,ukitizama kwa makini unaweza ona namba 1 na 2 zinaweza kuwa applicable,umeelewa?

!. System /tree diagram/mfumo
2.organization/flow chart/structure/muundo
1==2 ??

Mhh
 
Kwa hali hii wakubwa. Nadhani kilimo kwanza ni kuwashibisha tu hawa jamaa. Hapa jamani ni kuomba mapinduzi ya wananchi. Mass revolution na hii tunaiweza mwezi wa kumi!
 
Wakulima walalamikia uchakachuaji wa vocha
Imeandikwa na Fadhili Abdallah (Habari Leo), Kigoma; Tarehe: 19th January 2011


NAIBU Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza ameanza ziara ya siku tatu mkoani Kigoma kwa kukumbana na kadhia ya uchakachuaji wa vocha za ruzuku ya pembejeo unaofanywa na mawakala kwa kushirikiana na kamati za mbolea za vijiji.

Chiza aliyeanza ziara katika Kijiji cha Mwamila, Kigoma Vijijini alikumbana na kilio kutoka kwa baadhi ya wakulima wa kijiji hicho, waliokuwa wakilalamikia kunakiliwa kwa saini zao zikionesha wameshachukua vocha zao za pembejeo wakati si kweli.

Mmoja wa wakulima hao, Mussa Thomas alimweleza Waziri Chiza kwamba alipofuatilia jina lake kutaka kupatiwa vocha zake kwa ajili ya kupata mbolea ya ruzuku, alikuta saini inayoonesha ameshachukua vocha hizo.

Mkulima huyo alidai jambo hilo limekuwa likifanywa na wakala wa mbolea ya ruzuku kijijini hapo kwa kushirikiana na Ofisa Mtendaji wa Kijiji na hivyo ameshindwa kupata mbolea.

Mkulima mwingine wa kijiji hicho, Florida Leonidas alidai mbele ya Chiza kwamba baadhi ya mawakala huwasainisha wakulima vocha na baadaye kuwapa Sh 10,000 badala ya vocha na uongozi wa Serikali ya Kijiji umekuwa ukishuhudia mambo hayo.

Wakulima hao pia wamelalamikia hali ya kijiji chao kutotembelewa na wataalamu wa ugani, hali iliyowalazimu kutotumia mbolea ya minjingu msimu huu licha ya watu wengi kuchukua mbolea hiyo.

Chona Kiloloma, mkulima wa mahindi kijijini hapo alidai kwa misimu mitatu sasa hawajawahi kutembelewa na mtaalamu yeyote wa ugani, hali inayowalazimu kushindwa kutumia mbolea hiyo kwa kuhofia kuharibu mazao yao.

Hofu hiyo kwa mujibu wa madai ya Kiloloma inasababishwa na kushindwa kujua kipimo na mahitaji mengine ya mbolea hiyo ili ifanye kazi vizuri.

Kwa upande wake Ofisa Kilimo na Mifugo wa Wilaya ya Kigoma, Daniel Kamwela alisema yapo baadhi ya matatizo katika suala hilo na kwa kiasi kikubwa yanafanywa na mawakala kwa kushirikisha kamati za mbolea za vijiji.

Kamati hizo zimepewa jukumu la kudhibiti hali hiyo na Ofisa Mtendaji wa Kijiji anahudhuria kama mjumbe ili kudhibiti matukio hayo.

Kamwela alisema ili kuhakikisha mbolea inafika kwa mkulima, kamati za vocha za mkoa na wilaya ziliamua kuweka utaratibu wa kuwepo wakala na uongozi wa Kamati ya Mbolea ambapo mkulima anasaini vocha ambayo inabaki kwa wakala na kupewa mbolea.

Alisema pamoja na utaratibu huo, ameshangazwa na wakala na kamati za mbolea za vijiji kufanya mambo mengine na kuhujumu mkakati wa kilimo wa matumizi ya mbolea.

Chiza alisema anazo meseji nyingi za simu zinazomuelezea kuwepo kwa matatizo mbalimbali ya vocha hizo mkoani Kigoma.

Alisema madhumuni makubwa ya ziara hiyo ni kujifunza matatizo yanayotokea kwenye ugawaji wa vocha za pembekeo za ruzuku.

DC aonya magendo vocha za ruzuku
Imeandikwa na Mwandishi Wetu, Tarime; Tarehe: 11th January 2011


MKUU wa Wilaya ya Tarime ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Pembejeo, John Henjewele ameonya mawakala wa pembejeo za ruzuku watakaopewa mgawo Januari 15 mwaka huu, kuepuka kuvusha pembejeo hizo kwa magendo.

Akizungumza jana katika kikao elekezi, Henjewele alisema watakaobainika kuvusha kimagendo pembejeo hizo kwenda kuziuza nchi jirani ya Kenya, watafikishwa katika vyombo vya sheria kujibu mashitaka ya uhujumu uchumi.

"Mawakala wote wabandike majina ya wakulima wao waliokubaliwa kupewa pembejeo nje ya ofisi za vijiji mapema, ili kuondoa dukuduku la kubaini majina bandia na kuwazuia kupata pembejeo hizo.

Ili kudhibiti bei halali ya pembejeo kutoka kwa mawakala kwenda kwa mkulima, Henjewele aliagiza na bei hizo zibandikwe.

Alisema katika msimu uliopita kulikuwa na udanganyifu ulioleta malalamiko mengi yakiwemo mawakala kuchukua pembejeo za vituo vingine.

Naye Meneja wa Benki ya NMB Wilaya ya Tarime, Mathias Nkulu alisema mawakala wanatakiwa kuwa makini wakati wa kujaza fomu za vocha zinazopelekwa benki kwa madai kwamba mwaka jana benki hiyo ilipata usumbufu mkubwa kutokana na baadhi ya mawakala kutofuata taratibu.

Mbaroni kwa udanganyifu vocha za ruzuku
Imeandikwa na Joachim Nyambo, Mbeya; Tarehe: 10th January 2011


POLISI mkoani Mbeya inawashikilia maofisa watendaji wawili akiwemo wa kata na mawakala wawili wa usambazaji wa pembejeo za kilimo za ruzuku wilayani Mbozi, kwa tuhuma za udanganyifu katika ugawaji wa vocha za pembejeo za msimu huu.

Maofisa hao ni pamoja na wa kata ya Chilulumo, Visenti William na wa kijiji cha Itontela, Raison Sichizya huku mawakala wakiwa ni wa kijiji cha Chilulumo, Joseph Mhume na wakala wa kijiji cha Kaonga, Musa Zambi.

Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Gabriel Kimolo alisema jana kuwa watuhumiwa hao walikamatwa baada ya kamati ya ulinzi na usalama kuwatuhumu kwa kushiriki kuwarubuni wakulima kwa kuwapatia fedha na mbegu kidogo, ili kujipatia faida kubwa.

Kimolo alidai watendaji na mawakala hao, walikuwa wakiwarubuni wakulima ambao hawana uwezo wa kumudu kulipia fedha za kifurushi cha pembejeo ya ruzuku, kwa kuwapatia Sh 10,000 ili watie saini vocha yenye thamani ya Sh 70, 000.

Alidai baadhi ya vijiji vya kata ya Chilulumo, wakulima walirubuniwa kwa kupewa Sh 10,000 na kilo mbili za mbegu ya mahindi, badala ya kifurushi chenye mfuko wa mbolea ya kupandia na mbegu kiasi cha kilo 10.

Kwa mujibu wa Kimolo, kutokana na taarifa hizo aliagiza kuvunjwa kwa kamati za usambazaji wa pembejeo na kuwasimamisha kazi watendaji hao hatua ambayo imewapa fursa polisi kuwakamata na kuanza uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo.

Mkuu huyo wa wilaya alidai kuwa kata ya Chilulumo ilipata mgao wa vocha 597 na kata ya Mkulwe ilipata vocha 465 na kila vocha moja ikiwa na thamani ya Sh 70,000.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Advocate Nyombi alithibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao lakini akasisitiza kuwa Polisi itatoa taarifa kamili baada ya uchunguzi kukamilika.

RC Moro awashtukia wabadhirifu wa vocha, asitisha usambazaji
Imeandikwa na John Nditi, Mvomero; Tarehe: 4th January 2011


SERIKALI mkoani Morogoro imesimamisha kwa muda kazi ya usambazaji wa pembejeo za ruzuku za vocha kwa wakulima, baada ya kubaini ubadhirifu na wizi unaofanywa na mawakala kwa kushirikiana na watendaji wa serikali za vijiji na kamati za vocha.

Uwamuzi huo umekuja baada ya kufanyika kwa uchunguzi katika vijiji mbalimbali vya Wilaya ya Mvomero, kikiwamo cha Maharaka ambako wakulima 219 kati ya 225, walisainishwa vocha hizo kwa kurubuniwa na kupewa Sh 10,000 ili wasamehe kuchukua mbegu na mbolea ya ruzuku.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya ndiye aliyetangaza uamuzi huo juzi katika kikao cha dharura kilichoshirikisha baadhi ya mawakala, wenyeviti wa kamati za vocha, maofisa watendaji wa vijiji na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa pamoja na mwakilishi wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.

Alisema uamuzi huo unaoanza kutekelezwa kwa wilaya zote tano kuanzia Januari 3 mwaka huu, una lengo la kuandaa utaratibu mpya, ili kuhakiki mawakala kutoka sehemu husika na kama wana vigezo vilivyowekwa.

“Tunarudi nyuma sana kwa siku mbili au tatu hizo za kusimamisha usambazaji lakini potelea mbali, nafikiri tutakapoanza tena tutakwenda vizuri, hii ni aibu kubwa kwa Mkoa wa Morogoro ambao umepewa jukumu la kuzalisha chakula kwa wingi kwa kujitosheleza na kusaidia mikoa mingine,” alisema.

Machibya alisema udanganyifu umeifanya Serikali kuanza upya kwa mchakato wa kuwapata mawakala watakaothibitishwa na watakaoonekana wameingia kwa njia ya rushwa, watachukuliwa hatua za kisheria.

Alisema mbali na mawakala hao, pia watumishi waliowasaidia kupata nafasi hiyo nao watawajibishwa.

Machibya alisema Mkoa wa Morogoro umepewa upendeleo maalumu kwa pembejeo za vocha za ruzuku, kutokana na jukumu la kuzalisha chakula kwa wingi ili kufanikisha mpango wa kuufanya kuwa Ghala la Chakula la Taifa (FAMOGATA) ndani ya azma ya Kilimo Kwanza.

“Msimu wa kilimo wa 2010/11, mkoa umepewa fedha nyingi za pembejeo na kwenye
umwagiliaji hivyo viongozi wa mkoa na wilaya zake ni lazima wasimamie fedha hizo za Serikali kwa umakini zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa na nitakuwa mkali katika jambo hilo,” alisema Machibya.

Mkuu huyo wa Mkoa alibainisha katika msimu uliopita kuwa tatizo la kupotea vocha lilijitokeza kwa kiwango na pia kulikuwa na tuhuma za kughushi, vocha hewa pamoja na matukio mengine ya hujuma, lakini msimu huu Serikali imelazimika kutoa elimu kwa wakulima ili kuwe na ufanisi kabla ya usambazaji.

Mkurugenzi Msaidizi wa Pembejeo za Kilimo na Ruzuku ya Mazao ya Chakula kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Dk. Mshindo Msolla alielezea kusikitishwa na vitendo vilivyofanywa na mawakala hao kwa kushirikiana na wakulima.

“Hii ni kesi mbaya na mimi kama mmoja wa wakuu wa mpango mzima wa vocha nchini kwa niaba ya Wizara, tunaunga mkono uamuzi wa Serikali wa kusitisha kwa muda kazi hii, kwanza wasafishe nyumba yao na watatueleza watakapokuwa tayari,” alisema Dk. Msolla.

Aliitaka Serikali kuchukua hatua kuwa waliobainika kuhusika kwa hujuma hizo bila kujali nyadhifa zao ikiwemo kufikishwa mahakamani kwakuwa jambo hilo halina msamaha.

My Take:

We were right two years ago when we exposed this unfolding scandal of the ill conceived and poorly managed voucher system. Inaonekana kashfa hii ni kubwa zaidi kuliko ambavyo mwanzoni tulifikiria.
 
Malalamiko ruzuku ya mbolea yahamia Mbulu (Mwananchi)
Send to a friend Wednesday, 12 January 2011 19:57 0diggsdigg

Happy Lazaro, Mbulu
SAKATA la wizi wa vocha za bembejeo za kilimo lililokumba Mkoa wa Mbeya, sasa limehamia wilayani Mbulu, mkoani Manyara baada ya wananchi wa Kata za Dongobeshi, Haydom na Maretadu kumlalamikia Mbunge wa Mbulu, Mustafa Akunaay, kuhusu wizi huo.

Wananchi hao walitoa malalamiko yao kwenye mikutano ya kwa nyakati tofauti, walisema maofisa watendaji wa kata na maofisa kilimo, wakishirikiana na mawakala wa bembejeo wamekuwa wakijinufaisha na vocha za mbolea.

Wananchi hao ambao muda wote walikuwa wakitoa malalamiko yao kwa kutumia lugha zao za asili; kifyomi na kibarabaigi, walisema kamati za ugawaji mbolea za kata zilizoteuliwa zimekuwa kikwazo kwao.

Waliongeza kuwa kamati hizo zimekuwa zikishirikiana na mawakala hao kufuja vocha hizo.

Mbunge wa Mbulu, Akunaay aliagiza maofisa watendaji wa kata na kamati za ugawaji vocha za ruzuku za mbolea, Wilaya ya Mbulu, kuhakikisha majina ya waliopewa vocha za pembejeo majina yao yanabandikwa ukutani kuondokana na wizi wa vocha za pembejeo.

Akunaay aliwataka wakulima wilayani humo kutambua kuwa, ruzuku inayotolewa na serikali ni kidogo kulingana na mahitaji.

Alisema ruzuku hiyo inatolewa kwa ajili ya eka moja ya shamba, hivyo wanatakiwa kila msimu kujiandaa kwa sababu, haiwezi kuwa tegemeo la mkulima wa kijijini.

Hata hivyo, Akunaay alisema anakusudia kufanya ziara ya kukagua jinsi maofisa ugani wanavyosaidia wananchi kulima kilimo chenye tija, badala ya kuendelea kulima kilimo cha zamani ambacho kimewadumaza kwa mapat
 
Kwa mtindo wa CCM wa kutotaka mushkeli wakati wa uchaguzi, hii ni kagoda nyingine. It will just be paused or silenced forever. By the way hao waliofisadiwa moja kwa moja si ndio wapiga kura wakubwa wa CCM? Kazi ipop serikali ya awamu ya nne...........uozo after uozo!!!!!!! 25bn ni hela nyingi sana kama tungekuwa na leadership ya kueleweka. Ikiwa properly invested inaweza kuzalisha chakula ya kutosha probably nusu ya nchi!!!!!!!

That country just make me sick!!!!!!!!

Halafu aliyekuwa Waziri wa Kilimo amehamishiwa Ikulu kuongea na Masheikh na Maaskofu na hataguswa. Hongera Mzee Wassira. Ulikuwa fukara sana kabla ya Dec 2005!
 
Katika hotuba yake jana JK alisisitiza kuwa ili nchi yeyote ile duniani iendelee kimaendeleo inahitaji watu wa daraja la pili...na kwa Tanzania watu hao ni wale waendesha ma-baloon na wenye elimu ya sekondari.....
Bila kujali ma-baloon haya yanapatikana kwa wizi wa vocha za ruzuku kwa wakulima na si kufanya kazi kwa bidii.
 
sasa kwa ishu hii alaumiwe nani?kama mpaka mfanyakazi wa ngazi ya chini kahusika!kila kukicha tunazidi tu kuharibikiwa!
 
Mimi nina uzoefu ktk Local govt, hizi fedha zinaliwa kwa kushirikiana na Hazina, Wiazara ya kilimo [whatever the name], pale halmashauri mhusika mkuu ni Afisa Kilimo akishirikiana na mkurugenzi, Afisa Mipango, na Mweka Hazina. Pia mtendaji wa kata, mbunge diwani, mwenyekiti wa halmashauri/Meya. Haishangazi CCM kuua hata watu ili wapate Umeya Arusha, sasa eleweni ni kwanini.
 
Kwa staili maendeleo tutakua tunayaona kwenye tv ya nchi za wenzetu tu....Mbona watu hawanyongwi kama nchi nyingine??
Mzee mwanakijiji nadhani habari kama hizi mngeziweka kwa lugha ya kingereza ili donor countries wote wajue kinachoendelea maana hatuna sababu ya raisi wa nchi kukimbilia nchi nyingine kila wakati kuomba misaada ya vyakula na vyandarua vya mbu wakati tunafanya misuse of tax money kiasi hiki.
Mi siku zote hua nasema we dont need any foreign aid to tanzania coz kama budget deficit ni 30% ambayo inafadhiliwa na donor countries wakati ukifanya utafiti mtu unakuta zaidi ya 30% hiyo ya badget kwa mwaka inaishia kwa mafisadi na rushwa.....hakuna haja ya kuomba misaada nje....maana ndo inafanya tunakosa uwajibikaji.
 
mkuu, siamini kama kilimo kwanza kiliwalenga wakulima. nadhani with time tutaona mambo yanajifungua kidogo kidogo kuanzia uagizaji wa machinery, pembejeo, mafunzo, na usambazaji. hili la vocha ni premature, pengine the real story is around the corner. thank you for keeping an eye
 
Hizo pesa zilitoka EPA zikagawiwa kwa kuendeleza kilimo kwanza sasa kilimo akijaanza wakazirudia mapema wakazirudi, kitu kikizaliwa gizani nilazima kiliwe gizani, EPA ilizaliwa gizani na wana GIZA CCM, wakaigawa kwa watendaji GIZA, watendaji wakaona pesa za giza aziwezi kupita hivi hivi nao wakoonja, naona wacha wale tu kwani waliokula walifanywa nini? na zilizobaki mbona bado zinatafunwa, angalau waliozila zitasaidia maendeleleo kidogo maana hazikufichwa ulaya kama za Chenge na Mramba
 
Wache nao wale kile kinachopitia mbele yao na hakuna wa kuwawajibisha la sivyo watahama CCM!..maana wameshaona kuwa Mkwere anawalinda Mafisadi PaPa wakati wao (WATENDAJI KATA/HALMASHAURI) ndio waliomuweka madarakani...

Heshima ya fedha za umma itakuwepo pindi wale Mafisadi PaPa watakaposhughulikiwa kwanza!.
 
Kaka nchi imeishauzwa, inawezekana hata watanzania pia wameuzwa ila hawajitambui, siku akitokea aliyeuziwa anataka figo zake usiny'ake kaka :frusty:
 
Kwa staili maendeleo tutakua tunayaona kwenye tv ya nchi za wenzetu tu....Mbona watu hawanyongwi kama nchi nyingine??
Mzee mwanakijiji nadhani habari kama hizi mngeziweka kwa lugha ya kingereza ili donor countries wote wajue kinachoendelea maana hatuna sababu ya raisi wa nchi kukimbilia nchi nyingine kila wakati kuomba misaada ya vyakula na vyandarua vya mbu wakati tunafanya misuse of tax money kiasi hiki.
Mi siku zote hua nasema we dont need any foreign aid to tanzania coz kama budget deficit ni 30% ambayo inafadhiliwa na donor countries wakati ukifanya utafiti mtu unakuta zaidi ya 30% hiyo ya badget kwa mwaka inaishia kwa mafisadi na rushwa.....hakuna haja ya kuomba misaada nje....maana ndo inafanya tunakosa uwajibikaji.


mzee tukiziweka habari kama hizi kwa kimombo na donors wakaanza kuzifuatilia tunaambiwa "tunalichafua taifa"! na kuwa si wazalendo! Na tunahojiwa "unafikiri wakisitisha misaada ni nani ataathirika?"
 
mzee tukiziweka habari kama hizi kwa kimombo na donors wakaanza kuzifuatilia tunaambiwa "tunalichafua taifa"! na kuwa si wazalendo! Na tunahojiwa "unafikiri wakisitisha misaada ni nani ataathirika?"

Sasa mkuu kuna haja gani ya kupewa huo msaada kama hauwafikii walengwa?
Chukulia mfano mzuri jirani zetu kenya baada ya kibaki kuleta upuuzi wa kungangania madaraka walikatiwa misaada yote na mikopo.
Sasa huoni wamechangamsha akili na kupunguza matumizi now wanajitegemea??
MKUU kama ni kuchafuka tushachafuka siku nyingi na tunanuka sasa!!! Nchi gani inaongozwa na mtu asiyejua kwanini nchi yake ni maskini?

Halafu je OPRAS imefikia wapi kwenye serikali yetu wakuu?
 
Back
Top Bottom