Zaidi ya bilioni 25 zatafunwa; Watendaji waanza kuwajibishwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zaidi ya bilioni 25 zatafunwa; Watendaji waanza kuwajibishwa!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mzee Mwanakijiji, Feb 17, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Feb 17, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,737
  Likes Received: 7,507
  Trophy Points: 280
  Wednesday, 17 February 2010

  Uchunguzi wa awali wa vyanzo vyetu mbalimbali unadokeza kuwa hadi hivi sasa zaidi ya shilingi bilioni 25 za vocha ya manunuzi ya pembejeo za kilimo (hususan mbolea na mbegu) zimetafunwa katika mikoa ipatayo 20 iliyopewa mfumo huo wa ruzuku ya serikali. Watendaji mbalimbali wa serikali kuanzia mkoa hadi vijijini kwa kushirikiana na watumishi wa ngazi mbalimbali wameshirikiana katika kutumia vibaya vocha hizo ambayo karibu nusu ya fedha zilizotengwa katika kusaidia upatikanaji wa zana na pembejeo za kilimo zinaonekana kutumiwa vibaya.

  Tangu tuliporipoti juu ya wizi wa vocha za zaidi ya bilioni 7 huko Rukwa uchunguzi wetu wa awali kwa mikoa ya Mbeya, Ruvuma, Morogoro, Kigoma na Iringa unaonesha kuwa serikali ya Rais Kikwete imejilundikia kashfa nyingine kubwa.

  uchunguzi wetu huu wa awali ambao tutaufunua siku chache zijazo unaonesha kwa mara ya kwanza mfumo wa ufisadi umeweza kutawanywa hadi ngazi za chini kabisa ambazo zamani zilionekana kukingwa. Katika mtindo huu wa sasa inaonekana hadi watumishi wa ngaza za chini sana wamehusishwa katika kushiriki katika kufanikisha mtandao wa uchotaji wa fedha hizi kwa kutumia mbinu ambayo imekuwa ikitumika katika manunuzi mengine.

  Watu ambao wanaendelea kuumizwa ni wakulima wa kawaida ambao sasa wanataka mbolea (ambayo ipo) lakini hawana vocha za kununulia na hivyo wengine kulazimika kulipia ununuzi wa pembejeo hizo katika bei yake halisi na hivyo kudefeat kabisa lengo zima la vocha.
   
 2. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #2
  Feb 17, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,373
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Jamani hivi tutafika kweli? Hivi kweli muungwana anayajua haya? :mad:
   
 3. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #3
  Feb 17, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,609
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Kilimo kwanzaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa! Sijui tumelogwa/?
   
 4. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #4
  Feb 17, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  wanatafuta pesa kwa ajili ya uchaguzi mkuu, maana kila mtendaji sasa hivi anatafuta jimbo la uchaguzi ili either akamng'oe mmbunge, Diwani wa eneo hilo...
  nachoka kusoma ufisadi, ila inakwaza.......pamoja na kuchoka bado sikati tamaa, na tusikate tamaa, kuwalani hawa wezi wa raslimali zetu.
   
 5. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #5
  Feb 17, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 655
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Hatua za kisheria zishike hatamu, vinginevyo Chukua Chako Mapema.
   
 6. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #6
  Feb 17, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,699
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Matukio kama haya ni mazuri sana kwenye mustakabali wa Taifa letu... maana tutajua kwa uhakika zaidi kwamba adui yetu ni akina nani, na wako wapi?

  Baada ya kung'amua maadui wa Taifa hili, then tutachukua hatua muafaka kuwaondoa, kwa sasa silaha zetu zinalenga at least 45% from the actual enemy!

  Sio sasa muda wote tunavyodhani ati adui yetu ni akina RA? sasa hapo napo alikuwepo...????
   
 7. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #7
  Feb 17, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,548
  Likes Received: 1,927
  Trophy Points: 280
  Tulipofika, kila kukicha afadhali ya jana. Sijui tunajua athari ya haya tunayoyafanya? au tunaona kwamba nchi yetu ina immune haiwezi kufanana na nchi nyingine zilizoanguka!
  Hii ndio nchi inayojengwa na Chama Chetu kitukufu. Nchi ya watu wezi kuanzia ngazi za juu kabisa mpaka vijijini kwa watumishi wa chini kabisa.
   
 8. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #8
  Feb 17, 2010
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Mwaka wa uchaguzi huu mkuu,
  Hiyo fweza ya ruzuku ya pembejeo za kilimo ndio mbadala wa EPA, Kagoda na deep green finance!!
  Suala la kashfa kwa serikali ya Kikwete ni kitu kidogo sana kwao, after all sh. bilioni saba ni kitu gani, si vijisenti tu hivyo.
   
 9. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #9
  Feb 17, 2010
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160

  Acha mchecheto wewe,

  umefanya uchunguzi na kuthibitisha kwamba hakuhusika? au ndo umepata pa kumsafishia?kama mnasema lowasa ni safi haitakuwa ajabu kusema RA nae ni malaika.
   
 10. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #10
  Feb 17, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,457
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145

  Kwani wewe ulitegemea mradi ungeenda kama ulivyopangwa kwenye makaratasi? Fedha zote zinazoliwa kifisadi hapa nchini hazichotwi hazina moja kwa moja, bali uhalalishwa kupitia miradi mbalimbali kama hii. Labda tukumbushane mfano wa hivi karibuni...mabilioni ya Kikwete ambayo hata Mh. mwenyewe anaogopa kuyaongelea mpaka leo!!
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Feb 17, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,737
  Likes Received: 7,507
  Trophy Points: 280
  Hivi sisi tuna utajiri gani? kwa sababu wakati mwingine naelewa kwanini Kikwete alishindwa kuelewa kwanini Watanzania ni maskini. Yawezekana ni kwa sababu ni matajiri sana kiasi kwamba tumekubali kuwa maskini?
   
 12. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #12
  Feb 17, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 16,187
  Likes Received: 2,712
  Trophy Points: 280
  Kilimo kwanza = Ufisadi kwanza
   
 13. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #13
  Feb 17, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,699
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Let direct problems/challenges to the appropriate owner.... hii sio kazi ya Rais ni Kazi ya Waziri Mkuu!!!!
   
 14. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #14
  Feb 17, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kwa mtindo wa CCM wa kutotaka mushkeli wakati wa uchaguzi, hii ni kagoda nyingine. It will just be paused or silenced forever. By the way hao waliofisadiwa moja kwa moja si ndio wapiga kura wakubwa wa CCM? Kazi ipop serikali ya awamu ya nne...........uozo after uozo!!!!!!! 25bn ni hela nyingi sana kama tungekuwa na leadership ya kueleweka. Ikiwa properly invested inaweza kuzalisha chakula ya kutosha probably nusu ya nchi!!!!!!!

  That country just make me sick!!!!!!!!
   
 15. W

  WildCard JF-Expert Member

  #15
  Feb 17, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,494
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  Naweza kuanza kuelewa kwa nini Wassira anazitetea sana vocha hizi.
   
 16. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #16
  Feb 17, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,457
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145

  Huwezi kwepa kumlaumu mwenye nyumba, hata kama urafiki wenu umetoka mbali na 'hamjakutana barabarani'. Yeye ana jukumu la kuhakikisha anateua wasaidizi ambao ni wasafi kiutendaji, na anahakikisha anafuatilia performance zao on regular basis na sio bla bla za kwenye TV. If you cant be on top of the events, why run for presidency? Hatutaki visingizio vya kitoto kwamba rais ni mzuri na mwadilifu ila wasaidizi wake ndo wenye matatizo!
   
 17. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #17
  Feb 17, 2010
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,158
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Hakuna usimamizi wowote kny fedha /vocha za Ruzuku pembejeo! Wajanja wengi sana wametajirikia kny vocha hizi, nimeona kwa macho yangu, watendaji wa vijiji, kata, wilaya, mikoa wakicollude na wafanyabiashara na kuwapa vocha wafanyabiashara, ambao wakishazipata vocha hizo, huchukua mbolea na kuilangua kwa wakulima at market price or higher depending on demand!

  Nakumbuka mwaka 2007, IR demand ya mbolea aina ya DAP ilikuwa kubwa sana kwa ajili ya kupandia viazi.....mbolea ya ruzuku ilikuwa inatakiwa iuzwe kati ya Tshs 30,000 mpk 40,000! Lakini mbolea yote iliishia kwa wajanja, vijiji kwa mfano vya Njombe kila kimoja kiliambulia only 0.3tons (300kgs=6bags)....??? mbolea nyingine yote walipewa walanguzi na kuiuza kwa zaidi ya Tshs 90,000 per bag!

  Hali kadhalika mkoani Morogoro mambo yalikuwa hivyo hivyo kwa mbolea ya Ruzuku, ambapo ma-agent wakubwa wa kusambaza mbolea hiyo walikuwa wacollude na watendaji wa serikali na pembejeo kuwapa walanguzi ambao waliipeleka mikoa mingine eg IR na kuilangua huko! Pia huko Mtwara, mwishoni mwa mwaka jana wafanyabiashara walikuwa wanamiminika kutoka mikoa ya nyanda za juu kusini kwenda kufuata mbolea ya ruzuku, kwani demand ya mbolea Mtwara ni ndogo kulinganisha na mikoa ya Mbeya, Rukwa na Iringa.

  Nchi hii mfumo mzima wa utawala kuanzia ngazi ya juu mpaka chini kabisa kny serikali za mitaa, upo kifisadi fisadi. Utawala wa nchi hii, haupo kwa ajili ya kuleta maendeleo ya wananchi bali kujiletea maendeleo yao binafsi. Nchi hii watu watakuja kuuza mpaka anga, barabara na hata wanachi tutakuja uzwa mambo yakiachwa yaendelee hivi hivi......!
   
 18. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #18
  Feb 17, 2010
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,465
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280
  Kasheshe,
  Hatumchagui Waziri Mkuu, tunamchagua Rais; kwa hiyo 'appropriate owner" ndiyo Rais.
   
 19. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #19
  Feb 17, 2010
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,851
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145

  Wajinga ndio waliwao ila wakiamka kutoka usingizini ni balaaaaaaaaaa
  Yote yana mwisho.
   
 20. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #20
  Feb 17, 2010
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,465
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280
  Mwanakijiji,
  Wizi, Rushwa na ufisadi vikwisha kuwa ndiyo "system"; virus, ukiambukizwa na "virus" maana yake organ iko pamoja. you cannot kill a virus without killing an organ. Hapa ndipo kwenye ngoma. Nani msafi? wewe fikiria nani atamrekebisha nani? We are already dead as a nation.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...