Zaidi ya asilimia 60 ya Watanzania wanatumia tiba asili kujitibu

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,069
10,012
KAIMU Mkurugenzi wa huduma za tiba Wizara ya Afya Dk. Caroline Damiani, amesema, zaidi ya asilimia 60 ya Watanzania wanatumia tiba asili kwa ajili ya kujitibu magonjwa mbalimbali kabla ya kwenda katika vituo vya kutolea huduma za afya au baada ya kupata huduma katika vituo vya kutolea huduma za kisasa

caroline asili ed.jpg

Kaimu Mkurugenzi Idara ya tiba Dkt. Caroline Damian.

Amesema hayo leo Februari 17, 2022 Jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo kwa Waganga wa tiba asili yenye lengo la kubadilishana uzoefu na kujadili changamoto na mikakati mbalimbali ya kuikuza taaluma ya tiba asili na tiba mbadala ili iendelee kuwanufaisha Watanzania.

“Watanzania zaidi ya asilimia 60 kwa wakati mmoja ama mwingine wanapata tiba asili kwa ajili ya maradhi mbalimbali kabla ya kwenda katika vituo vya kutolea huduma au baada ya kwenda katika vituo ama hospitali zetu zinazotoa huduma za kisasa” amesema Dk Caroline.

ganga.jpg

Baadhi ya Waganga wa tiba asili walioshiriki mafunzo ya kujengewa uwezo yaliyotolewa na Wizara ya Afya ili kuboresha huduma za tiba asili kwa wananchi, Jijini Dodoma.

Amesema, dhima kuu ya mafunzo haya ni kuhakikisha dawa zinazotengenezwa na Wataalamu zinakuwa bora kuanzia katika hatua ya uoteshaji, uvunaji, utengenezaji, uhifadhi mpaka hatua ya kumfikia mlaji ili isilete madhara kwenye afya ya mtumiaji.

Dk Caroline amesema, mpaka sasa Wizara ya Afya kupitia Baraza la Tiba asili na Tiba mbadala limefanikiwa kusajili dawa za tiba asili 73, huku akiweka wazi kuwa kati ya dawa hizo 73, dawa 20 zilileta mafanikio makubwa sana katika kipindi cha mapambano dhidi ya UVIKO-19.

Chanzo: Nipashe
 
Gharama za matibabu haziko affordable
Bima ya Afya hawana msaada wowote,
Dawa asilia zingine ni bora hata kuliko zile za hozpitali maana hizo za viwandani zinachakachuliwa sana
Utaalamu unazidiana, kwa mfano, kule Ilula Iringa kuna mganga wa jadi ni mzuri kuunga mifupa ambayo hata hospital kubwa wameshindwa, sasa unawalaumu wananchi kwa lipi?
 
Back
Top Bottom