Kiranja wa jamii
JF-Expert Member
- Jan 2, 2023
- 1,208
- 2,890
Watu wengi kwasasa wana matatizo mengi sana ya kiafya na wengine wametibiwa hospitali kwa muda mrefu bila mafanikio
Hali hii imepelekea kuzuka watu wasiowaaminifu mtaani wakijitanabaisha kuwa na tiba mbadala kwa magonjwa mbali mbali jambo ambalo kwa asilimia kubwa limejaa utapeli.
Ni kweli kabisa tiba mbadala za asili zipo na zinaaminika na zimewasaidia wengi sana na kwa kweli mimi naona wanasayansi wetu walitakiwa kutumia muda wao mwingi katika tasnia hii kuliko kiendelea kukariri maandiko ya ulaya ambao kiuhalisia dawa inayofanya kazi kwao si rahisi ifanye kazi kwetu kwa ubora ule ule kwasababu za kibaiolojia na kimazingira
Ni vigumu sana hawa wauza dawa asili huku mtaani kukosa dawa ya ugonjwa wowote. Kila dawa wanayo
Serikali haioni kama hapo kuna udanganyifu?
Mtu mmoja aweze kutengeneza dawa ya kisukari, presha, kifafa, kaswende, homa, kikohozi, kansa, vikojozi, ukimwi, kifua, uric acid, vidonda vya tumbo, chango, nguvu za kiume, nguvu za kike, mvuto wa wapenzi, kuponya mashetani nk.....
Haya yanafanyika mitaani ambapo watu wanaona, serikali za mtaa zinaona, taasisi husika zinajua lakini hawafanyi lolote.
Binafsi naamini wale wanaoweza kutibu ugonjwa fulani au magonjwa mawili matatu yanayoshabihiana lakini sio kila kitu
Badala ya kutibu hizi dawa wanazojishindilia wananchi zitakuja kuzalisha magonjwa mengine kwasababu zinaenda kuua figo halafu watu waje kusingizia pombe