Zabibu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zabibu!

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Mzee Mwanakijiji, Mar 8, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Mar 8, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Zabibu langu li tamu,
  Pekee lanipa hamu,
  Ni tamu tunda adhimu,
  La kale kama ya Shamu!


  Linaendelea...
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Mar 8, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Zabibu lako halizidi langu
  Utamu wake washika hatamu
  Kwa mbali lafanana na zambarau
  Lapatikana kule Lamu

  Kwingineko ni adimu
  Wengine wasema ni haramu
  Mimi na yeye latupa hamu
  Na sasa tu damu damu

  Nitarudi baadae........
   
  Last edited: Mar 8, 2009
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Mar 9, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Ni tamu hilo la kwangu,
  Nafyonza kivyanguvyangu,
  Ni tamu kuliko Changu
  Nimelirundika chungu!

  ... litaendelea...
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Mar 9, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Ni tamu hilo la kwangu,
  Nafyonza kivyanguvyangu,
  Ni tamu kuliko Changu
  Nimelirundika chungu!

  Siyo tunda la kizungu,
  La Uru siyo Marangu,
  Nalamba vidole vyangu,
  Naruka kama kulungu!

  ... litaendelea...
   
 5. Suki

  Suki JF-Expert Member

  #5
  Mar 9, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 373
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Si kwamba nawapa shua,
  Ni kweli ilotukuka
  Matunda tunayojua
  Ni mengi yasiyolika

  Toka kule misituni
  Hadi hapo bustanini
  Yanolika milimani
  Au yale ya mwambaoni

  Hata kama lamegeka
  Si lazma lakuvundikwa
  Dodo linalonyonyeka
  Tayari l'meshikwashikwa

  ...Ha!...
   
  Last edited: Mar 9, 2009
 6. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #6
  Mar 9, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Nimerudi nimerudi
  Kama Nilivyoahidi
  Wauliza toka wapi
  Gulioni mchikichini

  Kufanya nini nilienda
  Kutafuta tunda nalolipenda
  Tunda lile lenye kulika
  Wengine hukataa kulila

  Ni chachu kama ukwaju
  Utamu wake kama changu
  Ni kama umenyweshwa sumu
  Ulionjapo japo kiduchu
   
  Last edited: Mar 9, 2009
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Mar 9, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Suki nimekusikia
  Na Nyani nakubalia,
  Tungo zilizotulia
  Matunda mnayosifia!

  Bado hamjafikia,
  Zabibu ninalosifia,
  La kwangu lilivyotulia,
  Jinsi linaning'inia!

  Jekundu lililoivia,
  Utamu najisikia,
  Ulimi najing'atia,
  Jinsi ninalibugia!

  Kicheko najiachia
  Mguno najisikia
  Raha ninajipatia,
  Zabibu namumunyia!

  ... litaendelea...
   
 8. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #8
  Mar 9, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  hahahaahh auwiiiiiiiii! you all people are killing me with mashairi yenu for god sake sikujua kama cupcake wangu yupo so creative na yeye kwenye mambo ya mashairi..dang cuzin upo hapo so far?....
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Mar 9, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Nimeona vitu vyake si utani anajitutumua.. we have to keep him if for no other reason..
   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  Mar 9, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Heheheheee....ndio bana imenibidi na mimi nitunishe kidogo vimisuli vyangu....lol
   
 11. M

  Mundu JF-Expert Member

  #11
  Mar 9, 2009
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Zabibu kweli ni tamu
  kulisifia muhimu
  ni tunda la humu humu
  hata mimi nalijua

  ila sikutarajia
  kilingeni kuingia
  mzee kulisifia
  usijute kumegewa

  kizuri kina gharama
  tena huwa nicha ngama
  utakuja kulalama
  tutapojinyofolea

  ni angalizo nakupa
  ndugu yangu tupatupa
  huna haja ya kufupa
  kwanini watuzingua?

  fyonza hadi katikati
  ninakupa mkakati
  hatuta kushika shati
  kimya kimya ukilila

  nyani ngabu ni hatari
  vya watu hujivinjari
  ili kuepusha shari
  usirudie makeke.
   
 12. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #12
  Mar 9, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kabisa we sure do!...inabidi you two muandike lyrics mtauza sana me i will be yur manager...maana i am good kwenye hiyo industry....Cuzin naona Suki yupo naye kwenye line uh.....unamtrain taratibu siyo mchedho.


  Naona mambo yako pumkin siyo mabaya kabisa wee i am impressed kwa kweli! haya mbona hujawahi kuniimbia miye live kihivyo?....you need to do that tonite.
   
 13. Suki

  Suki JF-Expert Member

  #13
  Mar 9, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 373
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Redefining the word?
   
 14. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #14
  Mar 9, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  mtrain =swanglish...In perfect english = Training.....
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Mar 9, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  u c it pays off to go to that gym! now I know my cuz is good hands..
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Mar 9, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  cuz.. mchokozi.. Suki mtaalamu kivyake vyake, miye kwake styudenti!

  Ila Mundu naye yumo, si unaona vitu vyake hapo juu!
   
 17. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #17
  Mar 9, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  I see kuna watu wana talent cuzin kumbe uh!.... ila i am proud of my cupcake! maana sijawahi kumsikia kabisa akiimba hayo mashairi hahahah!...

  Alafu hivi what happend unakumbuka back in 2002 tulikuwa tutengeneze ile single yetu what happen>?...
   
 18. Suki

  Suki JF-Expert Member

  #18
  Mar 9, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 373
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Not exactly what I was getting at.
  All good though.
   
 19. Suki

  Suki JF-Expert Member

  #19
  Mar 9, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 373
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Strike two!
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Mar 9, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  I know... didn't I say I'm a first learner too?

  Zabibu ukijapewa
  Hilo utalichukuwa
  La bure ukimegewa
  Utalila kama muwa?

  Vipi kama bado bichi,
  Tena kijani kibichi,
  Utasusa kuwa mbichi
  Au hata hivyo huliachi?

  Vipi ukilingishiwa,
  Kinywani kupitishiwa
  Ulimini kuonyeshwa
  Kisha likaondolewa?
   
Loading...