Yutong Vs scania Vs ud

allys_bus__-ok_2.jpg

Mkuu, kabla hajaahirisha kwa muda safari za Dar - Mwanza, hakuna mtu aliyekuwa anagusa huu moto! Sio Yutong, UD, Nissan...walikuwa wanaunga tela...kabla ya tochi na ratiba maalum za muda wa safari, ngoma hii Dar saa 12 na kwenda mwanza saa 1 usiku... SCANIA is another thing boss, yutong, they are trying.
Kwa barabara ya mwanza hakuna aliyekwa anagusa ALLYS Sport na ni scania,uliza utaambia,ukiona yutong inachomoka wanafunga injini,gear box na diff za scania,kwa kuwa body yake ni nyepesi lazima ipepee,inakuwa na body ya yutong but injini ,gearbox na diff ni scania
 
Hahahahahaaaaaa dah!!! Mkuu umenichekesha sana lol

Haya sasa,kumbe mpaka ifungwe difu ya scania!nilitaka kushangaa scania inyanyaswe na yutong!labda huko mwanza,manake route ya mbeya happynation huwa anafanya kuzitanguliza greenstar,muro,saibaba,new force na super Feo kwa kuhofia kupigwa torch na trafiki wanoko wa Iringa,ila akiingia stand ya makambako akichomoka anawatoroka yaani mnaingia mbeya yeye ndo anatoka kuosha gari kwa ajili ya safari ya kesho.
 
Hivi sasa universally watengenezaji wa magari, ndege n.k kutokana na ughali, uhitaji mkubwa wa bati, wepesi wa vifaa hivyo ili viweze kubeba tonage kubwa wanatumia technology ya aina mbalimbali [hakuna technology ya china] wengine hutumia fibreglass.
kuhusu kuharibika kwa mara kwa mara kwa mabasi inawezekana kuwa sababu kubwa ni maintenance culture hatuna kwani wacha mabasi ya yutong hata sumri yanalaza watu barabarani kutokana na culture hiyo.
kwenye engine sasa mahitaji makubwa ni kwa fuel efficiency na more torgue engines ambazo huwa more powerful na more fuel efficiency
 
Hapo kwenye DIFF ndipo tatizo lilipo , zaidi ya hapo hakuna tatizo jingine cha muhimu ni kuzipumzisha tu, na service kwa wakati, safari ndefu hizi gari haziwezi.

Gearbox pia ni tatizo !Unafahamu kuwa youtong zinafungwa 8speed gearbox ya scania?
 
Upuuzi mwingine bana, misuli ya shingo imewatoka kisa mnabishania aina ya magari yenye mbio! Khhhaaaaaaaaa!:nimekataa
 
Upuuzi mwingine bana, misuli ya shingo imewatoka kisa mnabishania aina ya magari yenye mbio! Khhhaaaaaaaaa!:nimekataa
Hii ni sehemu ya kuelimishana kwa hoja topic ziko nyingi sana unachangia unayoona ina tija kwako , usidharau hoja za wenzako kama wewe unaona ni upuuzi kwa wenzako vina maana!
 
wakuu naombeni mnisaidie Scania bus zenye engine nyuma zinaweza fanya kazi kwetu? kama naleta kwa kuuza inawezekana nikauza kama pesa ngapi? labda tuseme basi ya abiria 49, choo ndani, nitashukuru kwa majibu yenu mazuri
 
...Kwa hiyo kwa mujibu wa JF nikitaka kupeleka basi kwetu Lushoto ambako kutoka Mombo hadi Mlalo unapanda mlimatu japokuwa ni lami tupu, natakiwa kuchukua Scania ama Yutong??
kwanza Mombo to mlalo sio lami tupu, lami inaishia magamba, pili Isizu ndo zenyewe kwenye kupanda milima, utafikiri manyani,
 
Best Buses by ranking:
Mercedes Benz
Scania
MAN
UD
DAF
Iveco
Yutong or Zonda

Nikukumbushe
1,VOLVO
2.SCANIA
3.NISSAN UD
4.DAF
5.YUTONG
6.IVECO.
Wadau wanaosema yutong,waambie waende Moshi Arusha,Mnyama Ngorika,Dar exp
Mwanza miaka nenda rudi Alikuwa Scania Super Najmunisa,Yutong good but shortly,kama Big G vile hizi yutong,scania utatumia hata miaka 10 na zaidi,
wadau wa yutong Mchina wameshasikia SCANIA MODELS HIZI?
SCANIA 91
SCANIA 92
SCANIA 93
SCANIA 94
SCANIA 111
SCANIA 112
SCANIA 113
SCANIA 114
SCANIA 124
SCANIA 524 Hii bado haijafika Bongo bado,kila design hapo ina maana yake ktk mbio,ubebaji wa mizigo,wepesi,uimara nk
Utaipenda kwenye milima,kama ina shuka vile,ikiwa na gia 16.
 
kwanza Mombo to mlalo sio lami tupu, lami inaishia magamba, pili Isizu ndo zenyewe kwenye kupanda milima, utafikiri manyani,

Asante kwa ufafanuzi kuwa Lami inaishia Magamba.Tatizo ni Kuwa mi naishi Bumbuli na Lami kwangu inaishia Soni!!
Sawa kuhusu Isuzu lakini 'Nani Zaidi' hapa Leo ni kati ya Scania na Yu Tong! Huyu Isuzu tutamtafutia mpinzani wake 'Jumapili' Ijayo...!!!
 
wakuu naombeni mnisaidie Scania bus zenye engine nyuma zinaweza fanya kazi kwetu? kama naleta kwa kuuza inawezekana nikauza kama pesa ngapi? labda tuseme basi ya abiria 49, choo ndani, nitashukuru kwa majibu yenu mazuri

Zitakusumbua kwa sababu ya hali ya hewa kwani engine mbele ni kwa ajili ya upepo system ipoe vizuri, achana na hiyo kiti.
 
wakuu naombeni mnisaidie Scania bus zenye engine nyuma zinaweza fanya kazi kwetu? kama naleta kwa kuuza inawezekana nikauza kama pesa ngapi? labda tuseme basi ya abiria 49, choo ndani, nitashukuru kwa majibu yenu mazuri

Mabasi yenye injini nyuma, yakiwemo ya Scania, hayafai kwa barabara na mazingira yetu ya Afrika, hasa kwa nchi kama Tanzania. Itakumbukwa kuwa Scania waliwahi kuleta mabasi ya modeli K93 na K113 yenye injini nyuma katikati ya miaka ya 1990 lakini hayakuwa na mafanikio katika soko kutokana na kuchakaa haraka na kusumbua katika matengenezo. Miongoni mwa makampuni ya usafirishaji yaliyokuwa na aina hii ya mabasi ni Kiswele, Scandinavia, Abood, Matema Beach, Air Msae na Royal Sumayi.
 
Well...ninachokumbuka mimi kuhusu hizi Yutong hasa tukiangalia suala la uwezo na uimara wa injini (labda na diff na gear box) niliwasikia hawa makonda wakisema kuwa wengi wanafunga injini za scania ,maana orijino injini zake hazivumilii masafa marefu kwa muda mrefu.

That said, lazima tusifie haya Mayoutong kwa kuleta mapinduzi kwen sekta ya usafirishaji....comortability na iile hali kuwa unapanda walau gari jipya...kiyoyozi, (baadhi), TV screens na kadhalika, hivyo kuondoa ukiritimba wa 'malori' ambayo kimsingi yamejengewa tu mabodi ya mabasi ila ni injini za malori na zaina nguvu balaa...ila kwa injini kubwa za scania kama 114 matajiri wanasema zinakuwa zinakula amfuta uklinganisha na 94 japo ndo ivo unawahi kufika.

Kuna hizi scania za dar espress mpya, kusema ukweli ni nzuri na comofrtable sana. ila wasi wasi wangu ni bei zake kulinganisha na youtong
 
Twende mbele turudi nyuma,yutong zinakimbia sana,ni nyepesi
kuhusu uimara sifahamu,ila scania marcoppollo zinateswa sana na hawa wadudu
ukitaka kupata ukweli waulize ABOOD na HOOD wanavyonyanyaswa na mayutong ya BM COACH
Nimepanda recently kwenda moro,nimejionea mwenyewe:A S 39::A S 39::A S 39:
 
Back
Top Bottom