Chimunguru
JF-Expert Member
- May 3, 2009
- 10,678
- 4,350
scania ndo gari wadau asikudanganye mtu!!!
kama yutong ni bora kuliko scania, mbona mayutong mengi yaliyo dar wametoa diff iliyokuja nayo na wamefunga ya Scania, umeshapata jibu heehe
kama unataka kujua yutong inakimbia kuliko scania panda haya mabus ya greenstar dar-mwanza route,utapata jawabu,inshort yutong zinatembea mkuu,dont try kushindanisha scania na yutong
umeona eeh nilipanda siku moja,kutokana na speed ikabidi niwaulize wahusika wamefunga nini kwenye zile bus,kumbe wameweka difu ya scania 124Lnilitaka kuandika kama wewe..ile njia hizi marcopolo na scania mpya huwa tunaziacha mbali sana na yutong za green sema tatizo huwa hazitulii njiani na driver asipokuwa mwangalifu mkipata ajali kwa speed ile na kwa bodi ile ya karatasi hatoki kiumbe anayepumua.
Kwa uimara Scania inaonoza kwa mbali kuliko Yutong, Zipo bus za 1990 zinatembea bila tatizo. mchina hadumu barabarani, nadhani mnakumbuka zila bus zenye rangi ya bendera ya Marekani zimekaa barabarani miaka 3 na sasa hazipo. Pia zile buffalo za kichina zilifanya kazi kwa miaka 2 zikafa. Scania ni moto, usipime.
... Nina Maswali kuhusu hii Mada.
Haya mabasi ya Scania tunaoyaona ya akina Dar Express yanatoka moja kwa moja Sweden, Brazili ama Afrika Kusini?
Tunasema Yutong ina bei nafuu kuliko Scania, Bei ya Wastani ya basi la Scania single/double deaf ni shillingi ngapi as opposed to bei yaYutong?
Unaponunua basi la Snania kwa mfano, unakwenda mwenyewe Afrika Kusini ama unakwenda tu pale Kibaha kwenye karakana yao na wao ndio wanakuagizia na we unalipa kwa pesa ya madafu hapa hapa?
Kama umenunulia Afrika kusini kwa mfano, Basi lako linaendeshwa kutoka huko hadi hapa ama linapakiwa ndani ya Meli na wewe unaenda kulichukulia KIbaha??
Nitashukuru kwa kueleweshwa:
Haya sasa,kumbe mpaka ifungwe difu ya scania!nilitaka kushangaa scania inyanyaswe na yutong!labda huko mwanza,manake route ya mbeya happynation huwa anafanya kuzitanguliza greenstar,muro,saibaba,new force na super Feo kwa kuhofia kupigwa torch na trafiki wanoko wa Iringa,ila akiingia stand ya makambako akichomoka anawatoroka yaani mnaingia mbeya yeye ndo anatoka kuosha gari kwa ajili ya safari ya kesho.umeona eeh nilipanda siku moja,kutokana na speed ikabidi niwaulize wahusika wamefunga nini kwenye zile bus,kumbe wameweka difu ya scania 124L