Yutong Vs scania Vs ud

UD ni moja ya engine yenye roho ngumu sana hata mwendo zinazo pia.
Kwa kigezo kipi? Kama ni Speed basi Scania yupo juu, labda UD ni ule uwezo wake wa kwenda safari ndefu kama kina Taqwa zile za Mombasa to Lusaka au Harare. Ila mwendo hapo Scania hana mpinzani
 
Yutong hakuna kitu, likifika kwenye speed ya 105 bus linayumba, halitulii barabarani wakati Scania hata likiwa kwenye speed ya 120 bado bus linakuwa limetulia barabarani.
scania ziko vizuri sana kwenye high speed nmewah kupanda dar express kwenda nairobi kile kipande cha kuingia namanga jamaa nmeshuhudia speed 150 gari linaunguruma kama linadai gear vile i wondered yutong tupa kule
 
620.jpg

546.jpg


SCANI NI GLOBAL BRAND WAKUU, Na iko Dunia nzima kuanzia sourh America, USA, ULAYA NA ASIA, ila YUTONG ZIKO AFRICA TU
Nimempenda huyu mnyama wa pili.
 
Ijapokuwa tokea mwaka wa 2000 scania zinazoingia Afrika mashariki ubora wake ni duni, mabovu na kibaya zaidi scania tz wala hawaweki vipuli na wakileta ni vipuli vya kutoka china ambayo bei inastahili iwe nafuu lakini scania tz wanawararua wa bongo.

Tunazisikia na kuzijua mbinu hizi. Na ndio maana wananaonunua mabasi ya scania kwa mikopo wanashindwa hata kulipa mikopo hiyo kwa sababu ya ughali wa magari, gharama kubwa ya uendeshaji na ubovu usiohimili.

Kwa hali hiyo tuweni wa kweli kwa kusema Yutong ni mabasi mazuri na yakiundwa China kwa technologia ya Europe na yanatumia Engine za Cummins ambayo ni technologia ya kimarekani iliofaulu, na pamoja na hayo bei ya Yutong ni nafuu mno na ni sawa na ni asilimia 30% TU ya bei ya scania, na isitoshe vipuri vipo kwa wingi tu na vya asilia pia ambavyo hutengenezwa na Yutong wenyewe kutoka China, na ulaji wa mafuta ni pungufu kuliko scania na bodi zake Yutong zimeundwa kwa kuzingatia viwango vya usalama duniani na kuzingatia hali ya barabara ya Tz na Afrika mashariki na kwa hivyo BODY zake za Yutong zina usalama kuliko scania marcoplo na irizar.

Kwa hivyo kama kuna watu wanaponda Yutong, basi hao ama wanadanganywa na wauzaji wa scania na ud kwa kufikiria kuwa kila cha china ni kibovu JAMBO AMBALO NI UZUSHI maana hata hao scania na ud hutengeneza vipuli vyao huko huko china. Na kama mtu atafatilia maintenance za Yutong vizuri na kutumia vipuli asilia UTAKUTA NA KUTHIBITISHA KUWA YUTONG NI bora na ndio suluhisho kwa usafiri na uchumi wa Tz. Wa Tz tuzinduke, si kila kitu cha ulaya ndicho kizuri, HAPANA, wakati umebadilika,

scania ishapitwa na wakati, scania hawatujali u Tz wetu wala uchumi wetu, bali wanachojali wao ni mishahara yao na maslahi yao binafsi tu. Ikiwa wanajali, iweje scania wako tz takriban miaka 40 lakini hata vipuli vya kutosha hawana, ukienda pale kwenye karakana yao utakuta vipuli vingi hawana, na ama hawana wanakuagizia kutoka aduka ya mjini ambayo ni mali ya taiwan iio na uboira na hata hizo vipuli walio navo utavikuta ni vya china huko huko au vya brazil na vya brazil ni vya uhafifu mno. Sasa iweje tukubali kudanganya kuwa scania ni bora kuliko Yutong kwa kisingizio kuwa yuong imeundwa China ili hali scania ni jina tu maana vipuli vyote ni huko huko China na afadhaliYuyong inaundwa China na Yutong wenyewe na hutoa Guarantee sembuse scania wanatengeneza china kwa kisiri na kwa hivyo huwezi hata kupata Guarantee.

wa tz tuamkeni na tuangalie maslahi yetu Kiuchumi, ikiwa ni wasafirishaji ni vema tununue Yutong ambayo ni asilimia 30% ya bei ya scania, na vipuli vyake tutumie genuine ambayo ni vipo vingi tu Tz na yenye bei nafuu na yana usalama kwa abiria wetu na ikiwa tunataka kuhakiki basi tuzitumie miaka 5 na tuuze tununue mpya maana muda huo fedha yetu tumerudisha, Lakini scania utanunua ghali sana sawa na mara 3 bey ya Yutong, inakula nafuta mengi, gharama yake ya uendeshaji ni mkubwa, na utatengeneza kila siku, na hata ikitembea miaka 3 mpaka 5, wakati bado hukurudisha fedha yako maana umenunua ghali abiria anaona basi lako kuukuu na hapandi tena, maana utamaduni wa abiria wetu kila miaka 3 wanataka bus mpya kwa hivyo utakuta scania wapende wasipende hawana nafasi.

Yutong ni suluhisho,

Mbongo mwenye uchungu na tz
umenena kwel mkuu
 
Back
Top Bottom