Yussuf Manji, Omba Toba

Bado sijaona ambako manji amefanya kosa,ila wewe mtoa hoja una nafasi ya kutupatia jibu juu ya hoja yako je bakwata ndio wezi wenyewe?tujibu hapo kwanza ndio tuanze kumnyooshea manji kidole.
 
Asante kwa ukumbusho mubashara
Manji hajawakosea waislamu chochote, bakwata walimuuzia viwanja kwa madharti awatafutie kiwanja kikubwa ili wajenge chuo kikuu, kafanya hivyo kawapa kiwanja kilicholipiwa kila mitu, leo mnsema nini jamani
 
Mambo mengine nayo ni matatzo, vp hao walo muhuzia hicho kiwanja wao wamepata mapigo gan?
 
hivi wewe hunaga kazi za kufanya? wewe ni mama wa nyumbani? unapata wapi muda wa kuandika haya mambo ya kigaidi?
 
Waislamu kwa kuombeana mabaya hamjambo! kila kukicha albadirr! hivi mnafikiri Mungu ni wa kuhukumu tu? kazi kubwa ya Mungu ni kusamehe jamani. Ndio maana ktk Ukristo tunaambiwa tusamehe 7 mara 70
 
Kwakweli kutokana na umri wangu, mambo haya nilikuwa siyafahamu , hakika mama yangu umenifumbua macho , kwakweli huyu jamaa anatakiwa alete toba kwa dhulma aliyowafanyia waislam!.
 
FaizaFoxy Mimi nimiongoni kwa mwawatu walioguswa saaana na huu ujumbe
Yaani umempa uhalisia kamili,,kwamaana ya kua HAKUNA KAMA KUMREJEA ALLAH..
Dua ya aliodhulumiwa IPO wazi kabisa kwa Allah
Hongera saaana Dada yangu kwa ukumbusho huu uliompa ndugu yako muislam mwenzio

Sent from Calculator Phone vesion007
 
Kumuomba Mwenyezi Mungu hakuna ubaya.

Tumewashtakia kwa Mwenyeezi Mungu wote waliohusika, anayesikika ni Manji kwa umaarufu wake, yanayowakuta hao wengine anayajuwa tuliomshtakia.
 
Hakuna binadamu mwenye uwezo wa kumuombea mabaya binadamu mwigine.
Hakuna katika sisi aliyeomba mabaya, watu wameshtaki kwa Mwenyezi Mungu.

Wapo wanaoomba mabaya, tena wengi tu. Hiyo ni mada nyengine.
 
Laana imekuisha nini?Si wewe ulikuwa unapambana kuwa ni mwenzenu kipindi wana mgogoro na Mengi?Kweli unafiki upo karibu na wewe kuliko jugula vein. Kotekote unafaa kuwa kafara nyie. Ni rahisi sana kukumezesha haramu wewe provided itaiweka upande tofauti na umchukiaye uchague moja.Utakula tuu haramu kuliko kumpa umchukiae haki yake.For the moment umeahimishia majeshi kitalu kingine ch akupotosha watu, hujatubu hata kazi nzuri uliyomfanyia manji hapa ktk hili jukwaa.Kesho zamu ikibadilika utahamia kumshutumu aliyemnyoosha Manji .Miss you ajuza wangu.....mwaaaaaah
 
Mtoa mada apuuzwe, Hana hoja, Unamlalamkia aliyeuziwa? Kwanini usiwalalamikie waislam wenzako waliouza eneo huku wakijua ni Viwanja vyenu vya Wakfu? Hiyo dual Kwanini hamkwasomea hao Waislam wenzenu kwa kuuza Viwanja vyenu vya Wakfu? Kwa hiyo ulitaka Manji awarudishie eneo lenu alilokwishalinunua kihalali kabisa Halafu pesa alizonunulia na muda alioutumia alipwe na nani? Ungekuwa wewe ungekubali ununue kitu Halafu umrudishie muuzaji Halafu pesa zako na muda uliotumiwa usirudishiwe gharama hizo? Au mliwatumia hao Waislam wenzenu wamuuzie Manji eneo LA Wakfu ili baadae mumtake Manji alirudishe kwenu ili akigoma mumtishie kumsomea dua hadi alirudishe bila kulipwa Fidia ili pesa zake mjinufaishe Nazo? MTOA MADA TOA PUMBA ZAKO HUMU.
 
wauzaji hawakupigwa albadir? mbona hadi leo ndiyo wenye jukumu la kutangaza mwezi umeandama nakugawa tende za msaada toka arabuni?
 
Manji hataomba chochote fedha zitamwongoza kushinda kesi zake, akiongeza mwezi tu atapona alosto arudi kuihudumia yanga.
 
Yussuf Manji ni Muislam na aliwakosea Waislam na ni wajibu wetu kukumbushana.

Toba ni kwa yeyote.
Kwanza kesi ya Manji inayomkabili sasa hivi wala haihusiani na dua zenu mlizomsomea, Manji anatuhumiwa kukutwa na Sare za Jeshi, Kwahiyo unataka kusema kama Manji angewarudishia kile Kiwanja chenu cha Wakfu hizi kesi asingekamatwa nazo?Hivyo Mungu wenu angeweza kumlinda Manji aendelee kuhujumu Nchi? Usiusianishe kesi ya Manji na Zile Dua zenu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…