Yupi kilaza hapa?

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
31,663
48,440
Nimeipata hii kwenye Facebook...

Kuna kijana mmoja alikua anaitwa Said. Kijana huyo shuleni kwao, wanafunzi wenzake hata mwalimu wake hakuna aliyekua anampenda kwa sababu alikua kilaza sana.

Siku moja mama yake alikwenda shuleni kwao kufuatilia maendeleo yake, mwalimu wake hakumficha, akamwambia ukweli kuwa tangu aanze kufundisha hajawahi kufundisha mtoto kilaza kama huyo.. Mama yake akamuhamisha shule na kumuhamisha mji kabisa.

Miaka 25 baadae, yule mwalimu alikua anaumwa na madaktari walimshauri kuwa njia pekee ya yeye kupona ni kufanyiwa operation ya moyo na dr pekee ni mmoja anaeweza fanya hiyo... Mwalimu akafanyiwa operation vizuri na alipozinduka alimuona daktari akitabasamu mbele yake.

Ghafla daktari alianza kushangaa mwalimu akianza kubadilika, ghafla akakata roho. Yule daktari alipoangalia kujua nini tatizo akamuona Said aliyekua mfagiaji pale akichomoa waya wa oxygen na kuchomeka simu yake chaji ...

Kama ulifikiri doctor alikua Said nawe ni kilaza.
 
Mimi ni kilaza, nilijua mwisho wake ni kuwa Said kawa daktari..., story zetu na za wanigeria huishaga hivyo mara zote:redface::redface::redface:
 
Mleta uzi ni kilaza kweli, inakuaje akaajiriwa saidi hospital wakati alikuwa kilaza? Kazi ya ufagiaji si ya vilaza.
 
Ukitaka uonekane ww ni kilaza, tafuta maana ya hii story!
 
vilaza wote mnaohisi kuwa unaweza chomoa mpira wa oxygen na kuchomeka simu!
 
Kilaza ni mtu yeyote anayefikiri kuwa mfagiaji anaweza kuingia chumba cha upasuaji (theatre) wakati upasuaji ukiendelea
 
Kilaza ni mtu yeyote anayefikiri kuwa mfagiaji anaweza kuingia chumba cha upasuaji (theatre) wakati upasuaji ukiendelea

Hapo umeelewa Vibaya baada ya OP mgonjwa huhamishiwa Wodini kwa ajili ya uangalizi sio chumba cha upasuaji.
 
vilaza wote mnaohisi kuwa unaweza chomoa mpira wa oxygen na kuchomeka simu!

Mashine ya Oxygen inahitaji umeme ili kuiendesha. Hivyo Kilaza alichokifanya ni kuchomoa source ya umeme wa mashine na kuweka simu yake. Mipira ni kwa ajili ya kuizungusha hewa kati ya mwili wa mgonjwa na mashine
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom