Sijutii kusoma ingawa sijapata ajira

Mkulima na Mfugaji

JF-Expert Member
Jul 26, 2013
1,013
1,634
Habari za weekend wanajanvi

Siku hizi kumekua na kelele nyingi mitaani na mitandaoni watu wanajuta kusoma na kusema bora nisingepoteza muda kwa kusoma, maana ajira zimekua changamoto
Ngoja nitoe kisa changu huenda kitafundisha wengi
Nilibahatika kumaliza Diploma ya kilimo,ila changamoto za ajira ilikua kubwa ila nikabahatika kufundisha kama mwalimu wa part time, ila pale shuleni niliona wenzangu waliokua wameajiriwa wanavyohangaika kwa jinsi maisha yalivyokua magumu kwao na ukiwaangalia wengi walikua wanafundisha ila kwenye mioyo yao kazi yao walikua hawaipendi kutoka moyoni, mimi nikajiuliza kama maisha yenyewe ya ajira yako hivi mbona ni magumu sana?
Yaani mwalimu na Bachelor yako ya Education unagombea mihogo na wanafunzi kila siku,
Ghafla ile hamu ya ajira ikaanza kupungua,
Muda si mrefu nikapata kazi kwenye shirika moja linalojishugulisha na kilimo, hapo ndio nikapata hamasa ya kutimiza ndoto zangu
Ilikua project ya miaka minne nikajibana mwaka wa kwanza tu nikafanikiwa kununua pori langu la ekari 4 nikawa naishi maisha magumu kazini ila kila ninachokipata nakipeleka shambani ,nilifanikiwa kupanda miti aina ya michungwa ya Valencia shamba lote
Nilikua na malengo mawili pindi mradi ukiisha
1.niwekeze kwenye mradi wa kilimo cha michungwa
2. Niwe na biashara angalau ya kuniendeshea maisha yangu pindi nikisubiri shambani kukae vizur

Kweli mradi ulivyoisha nilifanikiwa kufungua biashara ndogo ya miamara ila kwa upande wa shambani kulikua bado sana hakujakaa vizuri
Kipindi hiki niliamua kuweka usomi wangu pembeni nikauvaa ukulima kwenye biashara nilikua namuacha wife
Kwenye Kipindi hiki ndio niliona chungu tamu ya marafiki na ndugu, marafiki wengi sana walikimbia nikabaki na wachace tena ni wa mitaani
Ndugu wengi walikua mbali na mimi niliobaki nao ni wazazi,mke wangu na wanangu wadogo
Nilikua mfano mitaani ,yaani nilikua natolewa mfano kwamba fulani kasoma lakini mpaka leo hana ajira
Ingawa nafasi za kazi zilikua zinatoka ila wala sikujisumbua kuomba ,nilitaka kusimamia msimamo wangu wa kutotaka ajira ya mtu
Wazazi wangu nilikua naona jinsi wanavyoumia kwa kijana wao kukosa ajira
Mimi kwa upande wangu nilijiona niko sawa huku moyoni nikisema kama nikipata ajira ndio kabisa nitashindwa kuwasaidia wazazi wangu kwa mishahara hii ya local Government
Mke wangu nilimueleza na nikamuelewesha tofauti ya kuajiriwa na kujiajiri
Nilimueleza kwamba kama nikiajiriwa nitalipwa kiasi kadhaa, ambacho hicho ndio nikigawanye kwetu, kwa wazazi, kusomesha watoto, na kufanya mambo ya maendeleo
Alinielewa sana na akanipa support kubwa sana
Nifupishe story kwa sasa shamba peke yake kunanipa hela nzuri
Yaani kwa msimu mmoja wa machungwa napata mara mbili ya kiasi ambacho kama ningekua mtumishi kwa level yangu ningekua na kopa na kukatwa Mshahara kwa miaka minne au mitano
Biashara yangu ya miamara nimeongeza na library ya movie ambayo kwa pamoja vinanipa zaidi ya Mshahara ambao ningeupata kama ningekua mtumishi

Note
Safari ya kujiajiri ni ngumu tena ngumu sana inatakiwa kwanza usimamie unachokiamini na pia ziba masikio usisikilize ya mitaani .
Ila pia kumbukeni binadamu ni wanafiki sana yaani wale waliokua wananikejeli chini chini leo hii wananipongeza na kusema ajira sio issue kwa maisha ya siku hizi.

Marafiki wanataka kurudi ila nawakazia kwani kwa sasa shughuli za kilimo na biashara zinaniweka busy
Kikubwa ni kuweka malengo na kumuomba Mungu
Ila pia wake zetu wana mchango mkubwa kwenye mafanikio yetu,
 
Nisipo comment chochote hapa ntakua INSANE,

Asante mkuu Kwa hii inspirational words for us

#YCMB
 
Haya ni machungwa ambayo hayaharibiki mapema kwa hiyo hayakulazimishi mapema unaweza ukasubiri mpaka kufikia bei nzuri huwa yanauzwa mpaka Tsh 100 kwa chungwa moja shamani
Thanks sana mkuu.
Nawezaje na mimi kupanda kwenye compound yangu atleast miche 3?
Time required for them to start yielding???
Their life span???
 
Upo mkoa gani, mimi niko Tanga huku tunaanza kupanda miche ya limao halafu tunafanya badding na kuwa michungwa ila kama unahitaji michungwa ya nyumbani panda Early valencia huku wanaita msasa kwa sababu inawahi kuwa tamu, inawahi kukomaa, kama ukihitaji miche ya limao hiyo michache nitakupa bure ukapande halafu nitakuelekeza kufanya badding kwani hata hiyo miche ni Miongoni mwa miradi yangu niliyoianzisha
 
Back
Top Bottom