SoC03 Mpendwa adui muda umeisha

Stories of Change - 2023 Competition

Sayl

New Member
Jul 17, 2023
1
1
Katika kijiji cha Dhahabu, kijiji kilichajaa fursa nyingi za kibiashara na kilimo, ina ardhi yenye rutuba na mimea mingi ama kweli jina lake linaakisi uzuri wa kijiji hiko, japokuwa nyumba zao nyingi zimejengwa kwa miti na udongo na kuezekwa kwa majani.

Siku moja kwenye nyumba moja ndogo ya hodi ilisika na mwanamke alitoka na kumsalimia mgeni mwanaume, mgeni alijitambulisha "Mimi naitwa Kongolo nimekuja kulima, lakini nahitaji vijana wa kunisaisia, nimesikia hapa anaishi kijana mkubwa, naweza kuongea nae", Mama akasema " Asante kwa fursa, lajini hayupo, akiludi nitamwambia", mgeni aliaga na kuondoka.

Upande wa pili kijana anatembea kwenye msitu mkubwa peke yake, ghafla akasikia sauti kutoka nyuma ikisema "Bungo geuka, bungo geuka", Bungo kwa woga akasema."wewe ni nani, kwanini bado unanisumbua tu, sitaki kugeuka labda kitu kilicho nyuma yangu kinatisha", sauti iliendelea kumuita tena huku ikijiludia kwa mwangwi kama ya mzimu, bungo aliogopa na kuzimia, ghafla bungo akakulupuka kutoka usingizini kumbe hiyo yote kuwa polini na sauti ya ajabu ni ndoto, bungo akamuona mama yake ambaye ndo yule mwanamke aliyesema kuwa kijana wake hayupo, mama alifungua dirisha dogo kama la jela lililopo mbele ya kitanda cha kamba cha bungo, mwanga makali wa jua ukaingia na kumchoma bungo usoni, Bungo alilalamika kwa kuguna huku akijinyoosha, mama akasema "Bungo hivi unataka kulala mbaka saa ngapi, saa sita hii bado upo kitandani, kitanda chenyewe cha kamba si unaumia mbavu tu, wenzio wako wanafanya kazi saa hii, na kuna kazi imekuja ya kulima lakini nimemwambia haupo kwasababu najua mvivu wewe hautoenda", mama akandoka.

Bungo akaamka na kutoka nje, nje akakutana na wadogo zake wawili mamebeba mitungi ya maji, Bungo akawapita wadogo zake kama hawajui huku akipiga miayo na kujikuna kichwa, safari ni kwenda kuzurura, njiani Bungo akaona kundi kubwa la watu wakubwa na watoto wamemzunguka kijana mmoja akiwa amevalia koti jeupe na inaonekana kama anawaelekeza kitu, Bungo alitaka kujua kinachoendelea, alisogea mbaka pale huku akiwa mkono wake mmoja ameweka ndani ya suruali yake anajukuna kalio ambalo liliacha alama ya makucha na mkono mwengine ameweka kidole puani, kwa tabia hizo inaonyesha Bungo ni kijana mvivu, mchafu na asiye na aibu kufanya hayo yote mbele za watu, bungo akajipenyeza katikati ya watu na kusimama mbele ya kijana wa koti jeupe.

Yule kijana alivyomuona bungo alishangaa na kuita "Bungo ni wewe, Bungo akajibu "Umenijuaje", kijana akamjibu "Ni mimi Sami rafiki yako wa utotoni, nilienda kwenye ule udhamini wa masomo, nakumbuka we ulikataa, lakini ulilia sana nilipoondoka kwasababu mi ndo nilikuwa rafiki yako wa pekee", bungo kwa aibu akajibu "Unakumbushia hayo yote ya nini, naona sasa umekuwa mwanamazingaombwe, umevaa nguo nyeupe na umekusanya watu wengi hapa", Sami akajibu " Hapana nimekuwa Daktari, unakumbuka tulivyokuwa wadogo nilikuchoma na kijiti hadi ukatoka damu, nilisema ndo sindano, lakini nashukuru Mungu ndoto zangu zimetimia na sasa nachoma watu sindano kweli, vipi wewe unafanya nini?",Bungo alishindwa kujibu hilo swali na akaondoka.

Siku zilipita na bungo aliendelea kuota ile ndoto ya kutisha, mama yake alimshauri Bungo afuatilie ile ndoto kwasababu ilianza kumsumbua tangia miaka mingi na huo msitu anaoota upo kweli, lakini bungo hakumsikiliza mama yake, Mama Bungo aliwaambia wazee wa kijiji kuhusu ndoto ya bungo na wazee walimshauri bungo lakini bungo alilalamika kwa kusema "kwanini kila mtu anataka mimi niende huko msituni, hiyo ni ndoto tu sio kweli, vipi kama ni mzimu huyo na akanipoteza hukohuko au nikaliwa na wanyama wakali, mtampata wapi Bungo kama mimi ", wazee wa kijiji walikasirika kwa maneno yake kwasababu hana faida yoyote kwa familia na kjiji, waliamua kuachana nae.

Siku moja jioni mama na wadogo wa Bungo wakiwa wanapika jikoni Bungo alienda na kusimama mlangoni, hawakumtambua kama ni bungo kutokana na moshi mkubwa uliotanda hapo jikoni, nama alibahatisha kwa kuita "Bungo?", Bungo alijitokeza, Bungo alimwambia mama yake kuwa amekubali kwenda msituni kufuata ndoto.

Siku aliyofuata bungo mama Bungo akaingia chumbani kwa bungo kumuuliza kama ameshajiandaa na kumpa vitu atakavyohitaji katika safari yake, mama bungo akamwangalia bungo sana mbaka bungo akajishitukia, Bungo akainama uvunguni ya kitanda na kutoka na kipande cha kioo chenye kona zilizochongoka kama ukishika vibaya unaweza kujichoma, kioo kilikuwa na vumbi kiasi kwamba bungo hakujiona vizuri, alikifuta kioo kwa mkono na kujiangalia, akaona michirizi kwenye pembe za midomo yake, akafuta kwa mkono, Bungo akaanza safari, ghafla njiani akamuona simba, bungo alishituka sana, Simba akamuuliza bungo "Unaenda wapi", Bungo alishituka kuona simba anayeongea, Bungo akauliza "Ni wewe uliyeongea?", simba akamjibu "Ndio ni mimi na nimekuuliza, unaenda wapi?", Bungo kwa woga akajibu "Naenda kufuata ndoto yangu", simba alicheka sana na kusema "wewe pia una ndoto?

Hebu achana nayo kwenye huu msitu kuna ndoto mbaya tu, hakuna ndoto nzuri, nakushauri bola uludi tu", Bungo hakusikiliza ushawishi wa simba na akaendelea na Safari yake, kabla hajafika mbali akasikia sauti kama ile ya kwenye ndoto yake ikisema "Bungo geuka, bungo geuka" huku ikijiludia, Bungo aliogopa na kusema "Najua wewe ni ndoto tu nikifumba macho nikifumbua sittosikia sauti yako tena", Bungo akafumba macho, alivyofungua macho akaona vitu vingi vya ajabu ikiwemo kompyuta, simu na televisheni, vitu hivi ni vya kawaida kutokana na teknolojia lakini kwa mjinga Bungo vilikuwa ni vitu vya ajabu, Sauti ya ajabu ilimfundisha bungo jinsi ya kutumia hivyo vitu, na ikampa kama zawadi aludi navyo kijijini bungo alifurahi na kusema ataenda kuwalingishia kijijini.

Bungo alivyofika kijijini kwao aliona kijiji kimebadilika, nyumba zilikuwa si za udongo tena na zimeezekwa kwa bati, kasoro nyumba yao tu, pia akaona vijana wengi wameshika sim za kupangusa, Bungo alishangaa na kusema "Kwanini kila mtu ana kitu cha ajabu kama nilichopewa na sauti ya ajabu kule msituni, au hii bado ni ndoto?" Bungo aligundua haikuwa ni ndoto tena bali ni kweli na hayo yote yalikuwa tangia zamani ni yeye tu ndo aliyekuwa gizani, Tangia siku hiyo bungo akaanza kufanya kazi kwa bidii, akigundua kuwa vijana wote kijijini walikuwa na mafanikio isipokuwa yeye tu.

Kwenye hii story baadhi ya vitu haviwakilishi kitu kama kilivyo bali kimetumika kuwakilisha kitu kingine kama, Ndoto inawakilisha majukumu yaliyomuandama Bungo lakini hakutaka kuyatimiza, Simba inawakilisha vikwazo katika safari ya maisha, simu,kmpyuta na televisheni inawakilisha elimu.

Elimu inabadilisha mtazamo wa mtu, mtu aliyesoma ni tofauti na asiyesoma kabisa, tunaenda shule sio kusoma masomo tu lakini pia tunakutana na watu wengi kutoka tamaduni na wenye mtazamo tofauti, hii inatufanya upeo wetu kuwa mkubwa zaidi.

Fursa zipo kama zotee kwenye jamii ni wewe tu kuwa mbunifu, na kama unaona haufaniniki geuka nyuma, sijamaanisha ugeuke na kuangalia nyuma bali angalia mambo yako ya nyuma labda matokeo ya hayo mambo ya nyuma ndo yanakufanya ukwame mambo yako ya mbele.

Mtu mvivu na asiyewajibika ni mzigo kwa familia na Taifa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom